TABIBU JOHN LUPIMO WA LUPIMO SANITARIUM CLINIC |
WAKATI
mwingine, hasira na kuchanganyikiwa kwetu kunasababishwa na matatizo
yasiyozuilika katika maisha yetu ya kila siku.
Si
kila hasira haina mpangilio, na mara nyingi inatokana na mambo ya kiafya, ni
hali ya asili inayojitokeza katika mambo tunayokutana nayo.
Njia
sahihi ya kukabiliana na tatizo linalokukabili, ambalo linakusababishia hasira,
si tu kulenga katika kutafuta muafaka, lakini zaidi ni jinsi gani ya kulichukua
na kukabiliana nalo.
Kutatua
matatizo yanayokusababishia hasira kutaleta matokeo mazuri, lakini pia si
kujiadhibu mwenyewe kama jibu halitakuja kama
ulivyotarajia.
Watu
wenye hasira mara nyingi hurukia jambo na kulifanyia maamuzi, lakini baadhi ya
maamuzi hayo yanaweza yasiwe sahihi.
Kitu
cha kwanza cha kufanya kama upo kwenye
majadiliano makali ni kupunguza hasira na kufikiri juu ya majibu yako
unayoyatoa.
Katika
majadiliano hayo, kamwe usiseme kitu cha kwanza kinachokujia kichwani pako,
bali tuliza hasira na fikiri kwa uangalifu juu ya kile unachotaka kukisema.
Wakati huo huo, sikiliza kwa makini mtu mwingine anachokisema na jipatie muda
kabla ya kujibu.
Pia sikiliza kwa makini, jambo lile linalokusababishia hasira. Kwa mfano, wakati mwingine unahitaji uhuru wako binafsi, wakati huo mke au mume wako anahitaji mawasiliano ya karibu na wewe.
Pia sikiliza kwa makini, jambo lile linalokusababishia hasira. Kwa mfano, wakati mwingine unahitaji uhuru wako binafsi, wakati huo mke au mume wako anahitaji mawasiliano ya karibu na wewe.
Kama
ataanza kulalamika kuhusu tabia zako, usilipize kisasi kwa kumfananisha na
mfano usio mzuri, kwani hali hiyo italeta uharibifu katika uhusiano wenu.
Ni jambo la kawaida kwa mtu yeyote kujilinda wakati anapokosolewa, lakini akumbuke kuwa makini, asiruhusu hali ya kupigana.
Ni jambo la kawaida kwa mtu yeyote kujilinda wakati anapokosolewa, lakini akumbuke kuwa makini, asiruhusu hali ya kupigana.
Badala
yake asikilize kinachojili juu yake. Ujumbe wa mtu huyo unaweza ukaudharau na
kutoupenda.
Utahitaji uvumilivu kwa upande wako, na inahitaji kuvuta pumzi, lakini usiruhusu hasira yako au ya mshirika wako aache majadiliano yawe katika udhibiti. Kutulia kutaifanya hali kutokuwa ya uharibifu.
Utahitaji uvumilivu kwa upande wako, na inahitaji kuvuta pumzi, lakini usiruhusu hasira yako au ya mshirika wako aache majadiliano yawe katika udhibiti. Kutulia kutaifanya hali kutokuwa ya uharibifu.
Wakati
mwingine, ni vizuri kutumia ‘vichekesho’ kwani vinaweza kukusaidia kupunguza
hasira katika njia mbalimbali. Kwa jambo moja la uhakika, ni kwamba vinaweza
kukusaidia kuwa na mawazo yaliyo sawa.
Hivyo, wakati unapokuwa na hasira halafu unamwita mtu fulani jina au kumfananisha na kitu fulani, acha na ufikirie neno hilo linafananaje.
Hivyo, wakati unapokuwa na hasira halafu unamwita mtu fulani jina au kumfananisha na kitu fulani, acha na ufikirie neno hilo linafananaje.
Fanya
hivi pale jina linapokujia kwenye kichwa chako kuhusu mtu mwingine. kama
unaweza, fikiria picha ya kitu halisi kinavyokuwa.
Hali hii itakuondolea hasira uliyokuwa nayo, na vichekesho mara zote vinakuondolea hali ile ya ghadhabu uliyonayo.
Ujumbe muhimu kwa watu wenye hasira kali, Dk.
Hali hii itakuondolea hasira uliyokuwa nayo, na vichekesho mara zote vinakuondolea hali ile ya ghadhabu uliyonayo.
Ujumbe muhimu kwa watu wenye hasira kali, Dk.
Deffenbacher
anasema, watu wenye hasira wana tabia ya kujihisi kuwa wana haki, lakini mwisho
wao hujikuta wakiwa wamejishushia heshima mbele ya jamii, lakini hawakutakiwa
kutaabika kwa njia hiyo.
Labda watu wengine wangeweza kufanya hivyo lakini si wao.
Labda watu wengine wangeweza kufanya hivyo lakini si wao.
Wakati
unahisi kuwa unataka kuwa na hasira, mtaalamu huyo anashauri, jifikirie
mwenyewe kama ungekuwa ni Mungu au kiongozi mwenye mamlaka ya juu, ambaye
unamiliki mitaa, maduka na maeneo ya ofisi, mwenye maendeleo ya haraka na kuwa
na taratibu zako katika hali zote wakati wengine wanatofautiana nawe.
Jambo
unaloweza kulijua zaidi katika mawazo yako, unajiona kuwa wewe si mtu wa maana,
unaanza kuona vitu ulivyonavyo havina umuhimu hivyo unakuwa na hasira kutokana
na ukweli huo.
Kuna
tahadhari mbili za kutumia vichekesho. Kwanza, usijaribu kuondoa aibu yako kwa
kucheka, badala yake tumia kichekesho ili kujisaidia kukabiliana na hali hiyo.
Pili, usifanye jambo lisilopendeza, kichekesho cha kejeli, hiyo ni aina
nyingine ya mwonekano wa hasira isiyo na afya.
Hasira
ni hisia ya kuiangalia kwa umakini, lakini mara nyingine inakwenda na wazo kuwa
kama utaichunguza, itakuwezesha ucheke.
Wakati mwingine hasira Inabadilisha mazingira yako.
Wakati mwingine hasira Inabadilisha mazingira yako.
Kwa
mfano mazingira yetu yanatufanya kuwe na misuguano pamoja na ghadhabu. Matatizo
na majukumu yanaweza kukuongezea uzito na kukufanya upatwe na hasira.
Ipe
nafsi yako mapumziko. Hakikisha una muda wako binafsi na ratiba inayokuongoza
kwa siku nzima. Mfano moja ni kwa mama anayefanya kazi, ambaye amekuwa na
sheria yake kwamba, wakati anarudi nyumbani kutoka kazini, kwa dakika 15 za
kwanza hakuna yeyote atakayezungumza naye, baada ya muda huo mfupi wa mapumziko
anajisikia vizuri na kuanza kuwaandalia watoto wake mahitaji yao kwa furaha.
Njia
nyingine za kukupa ahueni katika maisha yako, ni kuwapo matukio tofauti tofauti
ambayo yatakuondolea tatizo la hasira ulilonalo.
Muda -
Kama wewe na mke au mume wako mmekuwa na tabia ya kutofautiana wakati mnajadili
mambo mbalimbali muda wa usiku, Inawezekana mnakuwa mmechoka, au mna mawazo, au
labda ni tabia yenu halisi, jaribu kubadilisha muda wakati mnaongea mambo
muhimu, badala ya usiku iwe asubuhi au mchana.
Epuka
- kama watoto wako wanaonekana wana fujo kwenye chumba chao, hali ambayo
itakufanya ukasirike, inabidi ulifanyie kazi suala hilo kwa kukaa kimya na kufunga mlango wa
chumbani kwako.
Tafuta njia muafaka - kama kila siku asubuhi unakutana na msongamano wa foleni, hali inayokusababishia hasira, ipe nafsi yako kazi ya kusoma ramani ya kujua barabara nyingine zisizokuwa na foleni. Au tafuta njia nyingine muafaka.

njia mbalimbali za kukuonyesha kuwa una hasira. Mwili wako utakujulisha kuwa
una hasira, kwa kuhema kwa nguvu, kubadilika uso wako, kukaza kwa misuli yako
pamoja na kuonekana unaongea kama unanguruma, hata kwa mtu unayempenda.
Watu
wengine wanazika hasira zao ndani. Kama unafanya hivi, utapata maumivu ya
kichwa au tumbo. Na mara nyingine unaweza kuanza kulia peke yako.
Si
vizuri kuficha hasira yako, inakubidi utafute njia ya kuitoa pasipo kujiumiza
mwenyewe au kuwaumiza wengine.
Kuna njia za kufanya endapo utajikuta kuwa umepatwa na hasira.
Kuna njia za kufanya endapo utajikuta kuwa umepatwa na hasira.
Njia
hizo ni kuongea na rafiki yako unayemwamini, kufanya mazoezi, kucheza michezo
mbalimbali, kuimba, kupalilia bustani yako pamoja na kufikiria mawazo mazuri.
Kwa mtu yeyote mwenye afya, haiwezekani asipatwe na hasira. Badala yake ukumbuke kuwa, unapatwa na hali gani unapokuwa na hasira.
Kwa mtu yeyote mwenye afya, haiwezekani asipatwe na hasira. Badala yake ukumbuke kuwa, unapatwa na hali gani unapokuwa na hasira.
Je,
inafanya mazingira yako kuwa mazuri au mabaya? Usiruhusu hasira iwe bosi wako.
Fanyia kazi jambo hilo.
kwa msaada zaidi pia unaweza kutufikia lupimo sanitarium clinic kwa usahayri lakini pia kama tatizo hilo limekuathiri kwa kiasi kikubwa tutakutibu, tufikie katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini.
VITUO VYETU
TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA
NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI
MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA
LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA
PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL,
MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni