Alhamisi, 20 Novemba 2014

UNAJUA KUHUSU TATIZO LA MWANAMKE KUVUJA DAMU NYINGI WAKATI WA HEDHI?


Mara nyingi ni vigumu kujua kama mwanamke anatoka damu nyingi au kawaida  ikilinganishwa na wanawake wengine wakati wa hedhi. Baadhi ya wanawake ambao wanahisi kuwa huvuja damu nyingi wakati wa siku zao hakika   wanapoteza damu kiasi cha wastani.Baadhi ya wanawake ambao wanaona kuwa wanapoteza kiasi cha  kawaida  huwa wanapoteza  damu nyingi.



Ufafanuzi

mzunguko wa  kawaida - upotevu wa  damu hukadiriwa kuwa kati ya mls 20 na 60 (vijiko vya chai 4-12 ). Kutokwa na damu inaweza kudumu hadi siku nane, lakini wastani ni siku tano . 

Kutoka damu nyingi - upotevu wa  damu  ni kati ya mls 60-80 au zaidi. Hii ni kama nusu kikombe au zaidi. Hata hivyo, ni vigumu kupima kiasi cha damu ambacho  kinapotea wakati wa mzunguko. Lakini  unaweza kutambua kama  unavuja damu nyingi iwapo : 
-Damu zinafurika na  kulowanisha  nguo au matandiko. 
-Unahitaji kubadilisha mara kwa mara  kitambaa au pedi. 
-Unahitaji vitambaa au pedi mbili au zaidi. 
-Unapata damu zenye mabonge .

Menorrhagia  ni hali ya  kuvuja damu nyingi    kila mwezi mwanamke anapokuwa kwenye hedhi. Pia, damu inayovuja inaweza kuathiri ubora wa maisha . Kwa mfano,hufanya mwanamke kushindwa kufanya shughuli zake za kawaida kama vile kufanya kazi au kwenda shuleni. 

Sababu.
Mara nyingi sababu haijulikani. Lakini magonjwa yafutayo yanaweza kusababisha mwanamke kuvuja damu nyingi
-Dysfunctional uterine bleeding-katika tatizo hili mwanamke huvuja damu bila kuwepo ugonjwa wowote katika mfuko wa mayai. Inadhaniwa kuwa chemikali iitwayo prostaglandin inaweza kuchangia tatizo hili. Linatokea katika miaka ya mwanzo baada ya kuvunja ungo.
-Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi
-maambukizi kwenye  kizazi
-matatizo ya hormoni
-saratani ya kizazi hasa kwa wanawake wenye umri mkubwa.
-kitanzi(IUD)-hiki ni kifaa kinachowekwa kwa utaalamu kwenye mfuko wa kizazi. 
-Dawa mfano dawa za kutogandisha damu,matibabu ya saratani nk

Uchunguzi
Vipimo mbalimbali vinaweza kuhitajika ili kujua sababu ya kuvuja damu nyingi wakati wa hedhi mfano ultrasound,kipimo cha hormoni na wakati mwingine uchunguzi hufanywa kuangalia kama kuna tatizo lolote wakati mwanamke amepewa dawa za usingizi.

Matibabu
Matibabu ya msingi hutegemea dalili na chanzo cha tatizo. Hata hivyo daktari anaweza kuanza kutibu dalili wakati akiendelea na uchunguzi.


wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0754301115
pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic

Maoni 1 :

  1. Mysuru Casino - The HERZAMMAN
    Mysuru Casino - The Home of the Best of the Slots! Visit us to Play 바카라 사이트 the best slots and enjoy the best table games in bsjeon.net our casino. 바카라사이트 Visit septcasino.com us 도레미시디 출장샵

    JibuFuta