HUU NDIO UKWELI KUHUSU UGONJWA WA KIFAFA NA MATIBABU YAKE..[EPILEPSY}
Ugonjwa wa kifafa ni nini?
Huu ni ugonjwa amabao unasabababishwa na seli za mishipa ya
fahamu zilizopo kwenye ubongo kutoa
umeme[impulses] mwingi kuliko kawaida kwenda kwenye misuli na sehemu zingine za
mwili, na matokeo yake mtu huanza kupata degedege ya mwili mzima, kukakamaa,
kuanguka chini na kupoteza fahamu..
mwaka 2013 ugonjwa huu uliua zaidi ya watu laki moja duniani, 80% wakiwa waafrika.
Mgonjwa huyu huweza kuanguka mara kadhaa kwa mwezi lakini
anaweza asianguke kabisa kama anafuata masharti na utaratibu mzuri wa matibabu…
Chanzo cha ugonjwa huu ni nini?
chanzo kikuu cha ugonjwa huukwa watu wengi hua hakifahamiki lakini baadhi ni moja ya sababu za kuugia kifafa.
Kurithi; familia na koo zingine zinakua na ugonjwa huu hivyo
watoto na wajukuu huzaliwa tayari na ugonjwa huu.
Kuumia kichwa: ajali zinazohusisha kuumia kwa kichwa huweza
kusababisha kuumia kwa mishipa ya fahamu na mtu kuugua kifafa.
Ulaji wa nyama ya nguruwe; nyama ya nguruwe ina mnyoo kitaalamu
unaitwa taenia solium ambao hushambulia mishipa ya fahamu ya ubongo na kumfanya
mtu kuugua kifafa hivyo ni vizuri ipikwe kwa muda mrefu ili iive kabisa.
Magonjwa mengine; kuna magonjwa mtu akiugua maishani mwake
baadae huweza kupata kifafa kwasababu magonjwa hayo yanavyoharibu mfumo wa
ubongo.. mfano homa ya uti wa mgongo kitaalamu kama meningitis.
Uvimbe kwenye ubongo: matatizo ya uvimbe kwenye ubongo kama
kansa huweza kusababisha mtu kuugua kifafa.
Kiharusi; huu ni ugonjwa ambao husababishwa na damu
kushindwa kupita vizuri kwenye ubongo au kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo
hali hii husababisha mtu kupooza nusu ya mwili wake na huweza kuugua kifafa
baadae.
Matatizo wakati wa kuzaliwa: wakati mwingine mototo huzaliwa
kwa shida sana kwa njia ya kawaida kiasi kwamba kichwa chake hubanwa
sana wakati wa kupita na hali hii huweza kumsababishia kifafa kwanzia
utotoni.
Matatizo ya utengenezaji wa mtoto tumboni; wakati mwingine
ile miezi mitatu ya kwanza ambayo mtoto ndio anapata viungo tumboni huweza kutokea
kasoro kwenye mfumo wa fahamu za kwenye ubongo na kumfanya apate kifafa
akizaliwa.
Magonjwa ya uzee yanayoathiri ubongo; kuna magonjwa huharibu
ubongo wakati wa uzee na magonjwa haya huweza kusababisha kifafa kipindi hicho.
Kuna aina mbili za kifafa…
Grand ma seizures
Hii ni aina ya kifafa ambayo inanawatokea watu wengi sana,
mtu huanza kwa kuchanganyikiwa, huanguka na kupoteza fahamu wakati mwingine kutoa povu mdomoni,
hii huendelea kwa dakika kadhaa mpaka saa nzima.
Petit ma seizures
Hii ni aina ya kifafa ambayo mtu anaacha kuongea ghafla,
mawazo yanatoka pale alipo kisha anaacha kuongea na baadae anarudi katika hali
yake ya kawaida kama hakuna kilichotokea hapo katikati na aina hii hutokea kwa
sekunde chache tu.
vipimo vinavyofanyika kugundua kifafa...
Ugonjwa huu unaweza kutambulika kwa dalili tu lakini mara
nyingi mgonjwa hupimwa vipimo tofauti ili kuweza kujua chanzo cha ugonjwa… mfano
- Uwezo wa kufanya kazi figo
- Uwezo wa kufanya kazi maini
- Kupima maji ya uti wa mgongo
- Kupima Kaswende
- X ray ya kifua
- Picha ya ubongo mfano CT SCAN..
matibabu
Kama kawaida chanzo cha ugonjwa kikipatikana mgonjwa
huanzishiwa matibabu lakini kama mgonjwa alikua tayari ameshapata madhara
kwenye ubongo kulingana na chanzo husika ataendelea kua na kifafa.
Ugonjwa wa kifafa hauponi kabisa, USIMALIZE FEDHA ZAKO KWA
WAGANGA WA KIENYEJI naomba nisisitize hili, ukishaambiwa una kifafa au mgonjwa wako ana kifafa fuata utaratibu wa
matibabu yaani kumeza dawa siku zote za maisha yako na kufuata baadhi ya
masharti na utaishi maisha ya kawaida kabisa.
Matibabu yasiyo ya dawa wakati mgonjwa amekamatwa na kifafa:{non pharmacological treatment}
- Mzuie mgonjwa asijiumize kwa kuweka kitu laini chini ya kichwa chake, ondoa vitu vikali karibu yake kama kisu, sindano au vyuma.
- Usilazimishe kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa.
- Usimshike kuzuia mizunguko yake
- Weka kichwa alale anaangalia upande mmoja ili kutoa mate mdomoni.
- Kaa na mgonjwa mpaka degedege ziishe
- Usiweke chochote mdomoni kwa mgonjwa kama dawa au chakula mpaka apate fahamu zake.
Mtu mwenye kifafa hali hii ya kukamatwa na degedege za kifafa sio ya ajabu sana ila ukiona
dalili hizi mkimbize hospitali..
- Degedege za kifafa zaidi ya dakika kumi
- Kutapika sana
- Kushindwa kuona vizuri
- Kupoteza fahamu
- Kichwa kuuma sana.
matibabu ya dawa..
Mgonjwa akishagundulika na kifafa ataanzishiwa dawa kama
carbamizapine, phenorbabitone au zingine za kifafa na atakua anameza kila siku
ili kuzuia hali hiyo ya kuanguka na kuoteza fahamu na akifuata masharti ataishi
maisha ya kawaida kabisa.
mambo yanayofanya kupata degedege za kifafa mara kwa mara..
- Kukosa usingizi kwa muda mrefu
- Mianga na miale ya disco
- Unywaji wa pombe
- Kuishiwa sukari mwilini wakati wa akisikia njaa kali.
- Kutomeza dawa kama ilivyoelekezwa.
MWISHO; katika matibabu ya kifafa njia zote yaani za dawa na
zisizo za dawa hutakiwa kutumika, kutofuata masharti na kutomeza dawa
huleta matatizo makubwa ya
kiafya hata kupelekea kifo. Pia ni vizuri kutoa taarifa kuhusu hali ya
ugonjwa
husika kwa majirani au watu unaoishi nao waweze kukusaidia unaposhikwa
na hali
hii. watu wengi hufa kwa ugonjwa huu kwa kudhani wamerogwa au kuacha
dawa baada ya kuombewa kwa imani za kidini na kudhani wamepona hivyo
jamii ni vizuri ikachukua tahadhari kwani ugonjwa huu ni hatari sana ila
ni wa kawaida sana masharti yake yakifuata.
kwa maelezo zaididi na matibabu tufikie lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini
VITUO VYETU
TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA
NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI
MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA
LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA
PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL,
MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,
kwa maelezo
zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na
0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni