Alhamisi, 10 Desemba 2015

MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA   NDOA (DYSPAREUNIA)



Tatizo hili huwasumbua baadhi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa, yaani kuanzia miaka 18 hadi 40. Tatizo huweza kuanza ghafla au taratibu pale mwanamke anapofanya tendo.
Maumivu haya hutokana na hali ya mabadiliko ukeni ambapo uke huwa mkavu daima au mwanamke anapata vipindi vya ukavu ukeni na katika mlango wa kizazi pia husababisha tatizo hili.
Maumivu yanaweza kuwa ndani ya kizazi, yaani wakati wa tendo unahisi kuna kitu kinasukumwa na ukahisi maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kiuno wakati wa tendo.

Maumivu pia yanaweza kutokea baada ya tendo la ndoa, mwanamke akafanya tendo la ndoa vizuri lakini anapomaliza tu akijigeuza anahisi maumivu chini ya kitovu na kiuno na wakati mwingine hata kichefuchefu.
Chanzo cha tatizo
Tumeona vyanzo vitatu vya maumivu wakati wa tendo ambavyo ni ukavu ukeni. Huu unatokana na maandalizi hafifu kabla ya tendo. Endapo hakuna maandalizi yoyote basi uke unakuwa mkavu na unashindwa kufanya tendo au linafanyika kwa nguvu.

Ukavu unaweza kusababishwa na kutokuwa na hamu ya tendo au kutojisikia kufanya tendo, hili linaweza kusababishwa na matatizo ya kisaikolojia au katika mfumo wa homoni.
Michubuko ukeni na katika mdomo wa kizazi husababishwa na maambukizi, kansa au kufanya tendo la ndoa kwa nguvu bila maandalizi au ubakaji.

Maambukizi ukeni huambatana na kutokwa na uchafu wenye harufu na muwasho. Maambukizi yanaweza kusababishwa na fangasi, bakteria na magonjwa ya zinaa.
Maumivu ya ndani hutokana na maambukizi katika viungo vya uzazi mfano, ndani ya kizazi, mirija na vifuko vya mayai.

Maambukizi haya huanzia ukeni na kusambaa hadi ndani ya kizazi, lakini pia yanaweza kuanzia kwa ndani hasa baada ya kuharibika au kutoa mimba.
Dalili za tatizo
Maumivu wakati wa tendo la ndoa yanaweza kuanza mara tu tendo linapoanza, au tendo linapoendelea. Vilevile maumivu yanaweza kutokea baada ya tendo kumalizika.
Mwanaume pia anaweza kupata maumivu wakati wa tendo au baada ya tendo kutokana na michubuko katika uume, matatizo katika misuli ya uume, maambukizi ndani ya njia ya mkojo na matatizo ya korodani.

Maumivu ya kiuno kwa wanaume na wanawake pia ni mojawapo ya tatizo kubwa.
Uchunguzi
Tatizo hili la maumivu wakati wa tendo la ndoa huchunguzwa hospitali ambapo vipimo mbalimbali hufanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa. Vipimo vya kuangalia ukeni, damu, mkojo na Ultrasound hufanyika kutegemea na ukubwa wa tatizo.

Ushauri
Ni vema uwahi hospitali kwa uchunguzi wa kina na tiba. Tatizo likiwa sugu yaani kukusumbua mara kwa mara husababisha upotevu wa hamu na raha ya tendo.
Kwa mwanaume hata uwezo wa kufanya tendo la ndoa hupotea. 


Inawezekana kabisa tatizo hili linakusumbua na umejaribu kutafuta tiba hospitali mbalimbali bila mafanikio na suluhisho la afya yako, tufikie lupimo sanitarimu clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini tukitoa huduma nzuri ya kiafya kwa kutumia mimea na matunda na clinic yetu ni ya tiba mbadala, na clinic yetu hatufanyi upasuaji wala kukutoa damu bali tunavyo vipimo vya kupima  mwili mzima  na kubaini tatizo hilo limekuathiri kwa kiasi gani, ewe mama au baba usiendelee kuteseka na hiyo hali piga hatua tufikie lupimo.


VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni