Jumanne, 25 Aprili 2017

                           FAHAMU JUU YA HEDHI YA KAWAIDA NI IPI?



Hedhi ya kawaida ni ile ambayo;
 Hutoka mara moja kwa mwezi .
 Hutoka kwa muda wa siku 3,4 au 5 tu.
 Hutoka bila maumivu makali
 Hutoka kwa kiasi cha kati cha damu yaani kubadili pedi mara moja tu kwa siku.
AINA TATU (3) ZA MZUNGUKO WA HEDHI
• Mzunguko wa siku 24 (mfupi)
• Mzunguko wa siku 28 (wa kati)
• Mzunguko wa siku 30 au 32 (mrefu)
SIKU ZA KUBEBA MIMBA (OVULATION DAY)
 SIKU 24 (MFUPI)
Huu ni mzunguko mfupi ,Hivyo hesabu kuanzia siku unapoanza hedhi siku ya kwanza hadi ya 9 hizi ni siku salama, kuanzia siku (10,11,12,13,14) Hizi ni siku za kubeba mimba.
 SIKU 28 (KATI)
Huu ni mzunguko wa kati, hivyo hesabu kuanzia siku ya kwanza unapoanza hedhi hadi siku ya 11 ni siku salama, siku ya (12,13,14,15,16,17). Hizi ni siku za kubeba mimba.
 SIKU 30 (MREFU)
Hesabu kuanzia siku ya kwanza unapoanza hedhi hadi siku ya 12.Hizi ni siku salama. Kuanzia siku ya (13,14,15,16,17,18). Hizi ni siku za kubeba mimba.
DALILI ZA KUPEVUKA KWA MAYAI
1. Joto la mwili kuongezeka 0.2 – 0.58C
2. Ute kuvutika.
3. Siku za mzunguko wa hedhi
4. Mlango wa mji wa mimba (cervix) kulainika kuwa mwekundu zaidi
5. Maumivu kidogo ya tumbo kulia au kushoto
6. Chuchu kuuma na kutoa majimaji au maziwa.
NB: Kwa maelezo zaidi juu ya mada hii naomba unipigie kwa namba yangu ya mknoni ya 0759324414 au 0719097574 karibu kwa swali lolote juu ya mada hii.







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni