Ijumaa, 1 Januari 2016

Lijue Tatizo la Kuvimba Ulimi na Ufizi
 (Thrush/Candidiasis)
 
Ugonjwa na kuvimba ulimi na ufizi husababishwa na viini vya ukungu (candida fungus). Watu wengi huwa na hali hii miliini mwao na huwa si hali ya kutia wasi wasi. Wakati mwingine hizi bacteria zikizaana sana bila kudhibitiwa, huweza kumsababishia mtu maradhi. Watu wengi hupata haya maambukizi kwa sababu tofauti tofauti lakini kwa watu walio na Ukimwi, hutokea mara kwa mara. Wakati mwinigine mgonjwa huhisi vibaya kidogo au kujisikia tu akiwa mgonjwa sana.
 
Dalili na matibabu

Kuvimba vipele kwenye ulimi na ufizi – Huwepo na mabaka mabaka meupe ndani ya mdomo. Kama uchafu mweupe kikatoka na hapo mahali hubaki pekundu sana. Pia kwenye kona za mdomo wako, kunaweza kutokea uvimbe na kukauka. Pia unaweza kutoka vipele vya mayai mdomoni mwako. Hutibiwa kwa dawa ya kuosha mdomo ya kuzuia hizo bacteria kuenea or antifungal systemic medication.

Kuvimba kwa vipele kwa koromeo – Uvimbe ukitokea kooni mwako hukufanya ushindwe kumeza chochote au ukimeza unahisi uchungu. Hutibiwa kwa dawa ya Traconazole ama Fluconazole antifungal systemic medication.

Uvimbe wa vipele kwa ngozi – Ngozi hugeuka na kuwa nyekundunyekundu na huwa na mabaka ya uvimbe ndani ambayo huwasha na huna machungu. Ngozi ya kazi ya vidole huweza kubambuka na pia sehemu ya kona kwenye makucha huwa chungu sana. Hutibiwa kwa dawa ya kupaka ya kumaliza hizi bacteria. Hizi sehemu ni lazima ziwekwe safi na kavu.

Uvimbe wa vipele kwenye mlango wa uzazi. Humfanya mtu ajikune. Pia hizo sehemu huvimba kukatokea harufu mbaya kwenye uzazi pamoja na usaha mzito mweupe unaosababisha hiyo harufu. Unaweza kuhisi uchungu na kukawa kujikuna kwenye sehemu zako za siri. Hutibiwa kwa dawa ya kujipaka ya kuzuia huo uchungu wa bacteria kuenea maambukizi yakitokea tena na teana, unaweza kupewa dawa ya kumeza ya kusafisha kila sehemu mwilini.

Uvimbe na upele unaotokea kwa nche ya sehemu ya mwanaume na kwenye hiyo ngozi ya mbele (Balanitis). Balanitis hufanya ncha ya sehemu ya siri ya mwanamume kuwa nyekundu na kuwa mabaka mabaka na sugamba kwenye ngozi ya mbele ya mboo. Mtu huhisi kujikuna na kuchomeka sehemu za siri. Hutibiwa kwa kupaka dawa ya kupaka ya kuzuia hivi vipele. Ni muhimu hizi sehemu zisafishwe vizuri. Maambukizi yakitokea tena na tena, daktari anaweza kumtaka mtu mzima atahiri.

Maambukizi kwenye damu (Systematic Thrush) Viini vya ukungu zikisambaa mwilini mwako, zinaweza kufanya viungo kushindwa kufanya kazi kabisa. Hutibiwa tu hospitalini kupitia kwa sind
ano inayodungwa kwenye mishipa ya damu.
 
kwa msaada zaidi tufikie lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoani
 
 
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni