Jumapili, 15 Novemba 2015

Vidonda Vya Tumbo, Ugonjwa Huu Ni Nini?

Vidonda vya tumbo (Peptic Ulcers) ni ugonjwa unaompata mtu ambapo kunatokea vijitundu au michubuko katika kuta za ndani za viungo vya mfumo wa uyeyushaji chakula. Michubuko hiyo huweza kutokea katika eneo la mfuko wa tumbo, katika duodenum au katika eneo la koo. Inakadiriwa kuwa asilimia 5 hadi 10 ya watu hupatwa na ugonjwa huu angalau mara moja katika maisha yao. Huu ni ugonjwa ambao unaweza kumrudia mtu baada ya kupona endapo chanzo chake hakikudhibitiwa. Kama ugonjwa huu utamrudia mgonjwa , mtu huyu atakuwa amejiweka kwenye hatari kubwa ya kupata madhara makubwa zaidi kama kutokwa na damu au kutokea tundu kubwa katika kuta za mfuko wa tumbo.

 Chanzo Cha Vidonda Vya Tumbo


Bacteria: Chanzo kikubwa cha ugonjwa wa vidonda vya tumbo ni bacteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori). Bacteria hawa huenezwa kwa kula chakula na kunywa maji. Katika mwili wa binadamu bacteria hawa wapo katika mate na katika ute unatanda juu ya kuta za duodenum na mfuko wa tumbo.
wadudu wa vidonda vya tumbo
H pylori hutengeneza enzyme (urease) ambayo hupunguza makali ya tindikali katika tumbo. Hilo likitokea, tumbo hutengeneza tindikali zaidi na hii ndiyo husababisha michubuko katika kuta za tumbo na duodenum. Bacteria hawa pia hudhoofisha kinga ya tumbo na kusababisha maumivu mbalimbali. Kwa sababu bacteria hawa wapo katika mate ya mgonjwa huyu, njia moja ya maambukizi ya ugonjwa huu ni tendo la kubadilishana mate wakati wa kubusiana.
Madawa: Matumizi ya madawa husababisha vidonda vya tumbo. Dawa nyingi ambazo huweza kusababisha vidonda vya tumbo ni zile za kupunguza maumivu ya kichwa na maumivu mengine madogo madogo. Dawa hizo ni kama aspirin, diclofenac, naproxen, ibuprofen n.k. Dawa hizi hupunguza uwezo wa tumbo wa kutengeneza utando wa ute wa kulikinga tumbo hivyo kulifanya liweze kuliwa kirahisi zaidi na tindikali. Dawa hizi pia hupunguza mtiririko wa damu kuelekea kwenye eneo la tumbo hivyo kupunguza uwezo wa tumbo wa kukarabati seli zilizoharibika.
 Urithi: Ugonjwa huu wa vidonda vya tumbo umeonyesha kuwa ni wa kurithishwa kwani wagonjwa wengi walibainika kuwa na ndugu wengi ambao wanaugua pia ugonjwa huu.
 Pombe Na Tumbaku: Watu wanaokunywa pombe na wale ambao wanatumia tumbaku wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu wa vidonda vya tumbo.
 Msongo Wa Mawazo: Haijabainishwa moja kawa moja kwamba msongo wa mawazo unaweza kusababisha vidonda vya tumbo, bali mtu mwenye vidonda vya tumbo atakuwa na hali mbaya zaidi pale atakapokuwa na msongo wa mawazo.

Dalili Za Vidonda Vya Tumbo


Maumivu Ya Tumbo: Dalili ya kwanza kabisa ya ugonjwa huu ni maumivu ya tumbo ambayo yanaongezeka pale tindikali inapogusa eneo lililoathirika. Maumivu haya yanaweza kutokea sehemu yoyote kuanzia eneo la kitovuni hadi kwenye mifupa ya mabega na yanaweza kuchukua muda mfupi au kuendelea kwa saa chache. Maumivu husikika zaidi wakati tumbo ni tupu na huwa makali zaidi nyakati za usiku. Maumivu hupungua kwa muda mfupi baada ya kula chakula. Mgonjwa anaweza kupata nafuu kwa siku au wiki chache halafu maumivu hurudi tena.
vidonda vya tumbo

Madhara Ya Vidonda Vya Tumbo
 Matatizo Wakati Wa Kumeza: Mtu mwenye vidonda vya tumbo hupata matatizo pale anapojaribu kumeza chakula au hujisika vibaya mara baada ya kupata chakula.
 Kutapika: Dalili nyingine ya tatizo la vidonda vya tumbo ni kujisikia kutapika au kutapika baada ya kupata chakula.
 Kukonda: Mtu mwenye vidonda vya tumbo hukosa hamu ya kula chakula na hukonda.
Dalili za ugonjwa huu  huweza kuwa mbaya zaidi kama vile kutapika damu, kutoa haja kubwa yenye rangi nyeusi au iliyochanganyikana na damu nyeusi na kusikia kichefuchefu.

 Tiba Ya Vidonda Vya Tumbo


Tiba ya vidonda vya tumbo hutolewa kulingana na chanzo kilichosababisha ugonjwa huo kama ni bacteria au matumizi ya dawa. Lengo kubwa ni kupunguza makali ya tindikali katika tumbo ili vidonda vipone au kuua bacteria wanaosababisha ugonjwa huu.

Mada yetu ya leo imeeleza maana ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo na vyanzo vya ugonjwa huo. Tukazungumzia dalili za kuweza kutambua kama unaumwa vidonda vya tumbo. Na mwisho tukaoorodhesha dawa za vidonda vya tumbo. Matumaini yetu ni kwamba umejifunza na kuuelewa ugonjwa huu. 
Tunaomba usisite kutoa maoni yako kuhusu uandishi wa mada hii au kutoa maswali uliyo nayo. Ni furaha yetu kuona kwamba tumekujibu vizuri pale ulipokuwa na swali.
Kama una tatizo la ugonjwa huu na bado hujapata tiba kamili, tufikie katika vituo vyetu vya lupimo sanitarium clinic vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini.

MIKOA TUNAYOPATIKANA:
 
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,  

kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni