Jumamosi, 30 Januari 2016

JE UNAUJUA UGONJWA WA BAWASIRI(HEMORRHOIDS),JE UNATIBIKA ?LUPIMO SANITARIUM CLINIC NDIO SULUHISHO LAKO.


Bawasiri ni mojawapo ya matatizo ambayo mara nyingi inapotokea humfanya muathirika kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba.Bawasiri husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

A.KUNA AINA MBILI ZA BAWASIRI(HEMORRHOIDS)

1
.Ya nje ya puru-      Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa       na mara nyingi huambatana na maumivu na muwasho katika sehemu hiyo.Mara nyingi mishipa hiyo ya damu(vena)hupasuka na damu huganda na kusababisha hali iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS kitaalamu.
2.Ndani ya puru/tupu/duburi-Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa na haiambatani na maumivu hivyo kuwafanya wengi kutotambua kuwa wana tatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika sehemu zifuatazo;

       i.Bawasir kutotoka katika mahali pake(iliyosimama)
       ii.Bawasir inayotoka wakati wa haja kubwa kurudi yenyewe baada ya kumaliza kujisaidia
       iii.Bawasir inayotoka wakati wa haja kubwa na hairudi yenyewe baada ya kujisaidia mpaka mwathirika            airudishe mwenyewe.
       iv.Bawasir inayotoka wakati wa haja kubwa na ni vigumu mtu kuirudisha baada ya kumaliza kujisaidia.

B.NINI KINASABABISHA BAWASIR ?

        Miongoni mwa visababishi vya bawasir ni;
       -Tatizo sugu la kuharisha
       -Kupata haja kubwa(kinyesi)kigumu
       -Ujauzito
       -Uzito kupita kiasi(OBERSITY)
       -Ngono ya njia ya haja kubwa(ANAL SEX)
       -Umri mkubwa na mambo yanayoongeza shinikizo katika tumbo.

C.DALILI ZA BAWASIR 

        -Kinyesi kuchanganyika na damu wakati wa kujisaidia CHEMATOZECHEZIA
        -Maumivu au usumbufu katika njia ya haja kubwa
        -Kutokwa na kinyesi bila kujitambua(kuvuja kinyesi)
        -Kijiuvimbe katika eneo la tundu(mlango)wa kutolea haja kubwa.
        -Ngozi katika eneo la tundu la haja kubwa kuwasha.
        -Bawasir kutoka wakati wa kujisaidia haja kubwa.

D.ATHARI ZA BAWASIR

        -Upungufu wa damu mwilini(ANEMIA)
        -STRAGULATED HEMORRHOID
        -Kinyesi kutoka na kuvuja bila kujitambua na kusababisha kunuka kinyesi saa zote.
        -Kukupunguzia morali ya kufanya kazi kutokana na maumivu hasa watu wanaokaa muda mrefu maofisini.
        -Kuathirika kisaikolojia
        -Kukosa hamu ya tendo la ndoa.
        -Kupungukiwa nguvu za kiume

E.JINSI YA KUZUIA BAWASIR

         -Kula mboga za majani na matunda na nafaka zisizokobolewa kwa wingi
         -Kunywa maji mengi lita sita hadi kumi na mbili kwa siku
         -Punguza kukaa kwa muda mrefu sana ukiwa chooni(unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa)

F.DAWA

        1.Mara nyingi dawa iliyo kubwa ni kukatwa kinyama na uendelee kula vyakula vinavyolainisha choo ingawa mara nyingi ugonjwa hurudi tena. zaidi tufikie blupimo sanitarium clinic kwani sisi hatufanyi upasuaji kuondoa hicho kinyama bali tutakupa dawa ya kumaliza tatizo hilo
         

KWA MASWALI,USHAURI TUWASILIANE TUFIKIE KATIKA VITUO VYETU VILIVYOPO MIKOANI
 
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.


 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni