Jumatano, 27 Januari 2016

FAHAMU KUHUSU DALILI, MADHARA NA MATIBABU YA UGONJWA WA KISONONO






Baada ya kufahamu kuhusu ugonjwa wa kisonono namna unavyoenezwa sasa ni wakati mzuri wa kuweza kufahamishana dalili, matibabu na namna ya kukabiliana na ugonjwa huo

Dalili za kisonono huweza kuanza kuonekana siku 2 mpaka 10 toka mhusika anapopata maambukizi.

Hata hivyo, kuna baadhi ya watu wengine wenye ugonjwa huu ambao huwa hawaoneshi dalili zozote,.

Wanaume ambao hupata ugonjwa huu wao dalili zao huwa ni kutoka usaha kwenye uume wenye rangi ya njano na mtoki wa kwenye paja kuvimba au kuuma pamoja na maumivu ya kitovu.

Kwa upande wa wanawake wao dalili zao ni kuwa na maumivu ya kuungua wakati wa kukojoa, kutoka uchafu sehemu za siri na majimaji kutoka yasiyo ya kawaida.

Baadhi ya wanawake hupata maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi pamoja na maumivu chini ya kitovu.

Kwa wale ambao hujihusisha na ngono za mdomo wao huweza kupata dalili za maumivu kwenye koo na usaha kwenye tonsili.

Ngono za kinyume na maumbile huweza kupata maumivu na kuwashwa na kinyesi chenye damudamu wakati wa kujisaidia.

Ugonjwa huu wa kisonono usipotibiwa huweza kuleta madhara kwa mhusika hususani maambukizi kwenye mirija na tumbo la uzazi, maambukizi kwenye mirija ya mbegu za kiume, mimba pamoja na kuharibika kwa mimba endapo mwanamke ni mjamzito. Hivyo ni muhimu kuhakikisha unawahi matibabu wewe na mpenzi wako pale ambapo unaona dalili kama hizo zinazoashiria ugonjwa wa kisonono.

Ikumbukwe kwamba kisonono ni ugonjwa ambao unaweza kuzuilika, pale ambapo utawahi matibabu, lakini njia nyingine za kujikinga na kisonono ni kupunguza idadi ya wapenzi na kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu ambaye umepima naye afya na kutumia kondomu kila mara ambapo unafanya ngono pamoja na kutojiingiza katika ngono, kwani ndio njia kuu ya maambukizi.

kwa msaada zaidi wa kimatibabu juu ya ugonjwa huo wa kisonono basi unaweza kuwahi mapema lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoani,

 
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni