Jumatano, 13 Januari 2016

 Msomaji wetu wa blog hii ya lupimo sanitarium clinic karibu katika mwendelezo wa makala mbalimbali zinazohusu afya yako zinazoletwa kwako na tabibu john lupimo wa lupimo sanitarium ambapo leo anakuletea makala inayohusu "Maumivu chini ya kitovu kwa wanawake na wanaume"

 , lakini kama unaswali unaweza kuuliza kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.

basi mara baada ya kukupatia mawasiliano yetu twende moja kwa moja katika makala yetu,

Msomaji wetu wa blog hii ya lupimo sanitarium clinic karibu katika mwendelezo wa makala mbalimbali zinazohusu afya yako zinazoletwa kwako na tabibu john lupimo wa lupimo sanitarium ambapo leo anakuletea makala inayohusu "MADHARA YA UTOAJI MIMBA" , lakini kama unaswali unaweza kuuliza kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic. au unaweza kutufikia katika vituo vyetu vilivyopo mikoani: IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA, Msomaji wetu mara baada ya kukumbusha mahali na mawasiliano yetu tunapopatikana sasa moja kwa moja twende kwenye makala yetu juu ya madhara ya utoaji mimba;

Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu

Maumivu chini ya kitovu kwa wanawake na wanaume. (Lower abdominal Pain)


 
Tatizo hili huwakumba watu wengi sana kwenye jamii yetu lakini kwa bahati mbaya watu wengi huchukulia ni jambo la kawaida kitu ambacho baadae hupelekea watu wengi kuingia kwenye matatizo makubwa ya kiafya hasa kwenye mfumo wa uzazi na mfumo wa chakula.

Maumivu chuni ya kitovu hutokea kama ifuatavyo:
 Yapo yale ya chini ya kitovu katikati, kushoto na kulia. Kwa wanawake maumivu ya kushoto na kulia yapo ya aina mbili. Kuna yale ambayo yanakuwa upande mmoja lakini husambaa kwa urefu wa sentimita mpaka nne na inaweza ikawa upande mmoja au pande zote mbili lakini yapo mengine chini ya kitovu ambayo yanaweza yakawa upande mmoja au pande zote mbili bila kusambaa kwa marefu.
Kuna maumivu mengine chini ya kitovu huwapata wanawake wakati tu wanaposhiriki tendo la ndoa kwa ndani ya uke au chini ya kitovu. Pia yapo ambayo huwapata wanawake wakati wameinama, wakati wa kunyanyua vitu vizito, wakati wa kucheka au kuimba na wakati mwingine wakiwa wamelala kifudifudi.
Maumivu chini ya kitovu yanaashiria matatizo gani kwa wanawake?
(i)                 Mirija ya uzazi kujaa maji mazito na machafu ambayo huzuia yai kutembea kwenye mirija ya uzazi. Mwanamke ambaye amewahi kuambiwa na daktari kwamba anatakiwa asafishwe kizazi chake/mirija ya uzazi na wakati huo huo anasikia maumivu chini ya kitovu kushoto na kulia au upande mmoja kuna uwezekano akawa na tatizo la mirija ya uzazi kuziba kutokana na kujaa maji machafu.
(ii)               Kutokukomaa kwa mayai ya uzazi. Hii husababisha vifuko vya mayai ya uzazi kuvimba(ovaritis) na kumletea mwanamke maumivu chini ya kitovu mithili ya kichomi. Mwanamke ambaye anamaumivu chini ya kitovu na wakati huo huo ana matatizo ya hedhi mfano hedhi kukoma au kutokuwa na mpangilio maalum kunauwezekano mkubwa akawa na tatizo la vifuko vyake vya mayai ya uzazi kutokomaza mayai na hivyo mayai kutotoka kwenye vifuko hivyo na kusababisha kuvimba na hatimaye kumsababishia mwanamke maumivu makali mithili ya kichomi.
(iii)             Kuvimba kwa kuta za mji wa mimba na kuta za mirija ya uzazi (PID/Pelvic Inflamatory Disease). Mwanamke anayesikia maumivu chini ya kitovu katikati na pembeni kwa wakati mmoja na wakati huo huo akawa anatokwa na uchafu mzito mithili ya maziwa mtindi kunauwezekano akawa na PID hasa hasa kama amewahi kukumbwa na tatizo la kuharibika kwa mimba kabla haijafikisha miezi mitano.
(iv)              Afya mbovu ya kibofu cha mkojo ikiambatana na matatizo ya maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo (UTI). Maumivu chini ya kitovu yanayohusisha afya mbovu ya kibofu cha mkojo huambatana na mgonjwa kutoa haja ndogo kidogo sana ila mara kwa mara. Itaendelea wiki ijayo
Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume huashiria nini?
Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume huashiria pia tatizo la tezi dume liitwalo Prostatitis yaani kuvimba kwa tezi dume. Maumivu haya hujikita kwenye shina la uume na huashiria tatizo hili  hasa kama mwanaume anakwenda haja ndogo mara kwa mara nyakati za usiku na umri ukiwa  unaelekea miaka 50 au zaidi. Dalili nyingine ambatano ni kutoa haja ndogo ambayo ina kasi ndogo sana tofauti na kawaida, ikiambatana na maumivu ya kiuno na mgongo, kuvimba kwa korodani, haja ndogo inayoambatana na usaha na damu, maumivu ya uume wakati wa kufika kileleni, na  damu katika maji ya uzazi (semen)
Kwa wanaume, maumivu haya ya chini ya kitovu huashiria pia tatizo ambalo kitaalamu hujulikana kwa jina la Hernia ambapo waswahili tunaita ngiri. Mwanaume anaposikia maumivu haya ya chini ya kitovu ikiambatana na maumivu ya korodani, korodani moja kupungua na nyingine kukua zaidi au zote mbili kukua au kupotea, ni dalili ya ugonjwa huu ambao huharibu ubora wa uzalishwaji wa mbegu za kiume ambazo zaweza kuzalishwa chache au ambazo hazina kasi ya kutosha kusafiri kwenye via vya uzazi vywa mwanamke na hivyo mwanaume kupoteza uwezo wake wa kutungisha mimba.
Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume kama ilivyo kwa wanawake huashiria tatizo la maambukizi katika mfumo wa haja ndogo yaani (Urinary Track Infection/UTI) ambapo dalili zake ni kama zile za mwanamke hapo juu.
Hitimisho.
Vipimo na tiba vyahitajika mapema bila kuchelewa ili kuepuka madhara makubwa katika mfumo wa uzazi, mkojo na hata wa chakula.






kwa msaada zaidi unaweza kutufikia lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini tutakutibu ambapo lupimo clinic ni clinic ya tiba mbadala, tunatibu kwa kutumia mimea na matunda, tufikie katika vituo hivi,


IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni