Alhamisi, 14 Januari 2016

UTI, UGONJWA UNAOATHIRI MFUMO WA NJIA YA MKOJO.

UTI(Urinary tract infections) ni uambukizi wa njia ya mkojo ambao huwasumbua watu wengi siku hizi. Uambukizi huu unaweza kusababisha maumivu na kukosa raha, na ugonjwa waweza kudumu kwa siku chache kama utawahi kutibiwa kwa kutumia dawa za antibiotiki.Kuna uwezekano pia wa kuchukua hatua kuhakikisha unaepukana na maambukizi haya ya njia ya mkojo.

UTI ni ugonjwa ambao huwaathiri zaidi wanawake ukilinganisha na wanaume, na sababu kubwa ikiwa ni ya kimaumbile, ingawa kuna sababu nyingine kama kufanya ngono na historia ya kifamilia.

Watoto pia waweza kuathirika na ugonjwa huu wa UTI, husani watoto wa kike walio chini ya umri wa miaka miwili na watoto wa kiume wasiotahiriwa. Dalili kuu kwa watoto wenye ugonjwa huu ni homa, ingawa vipimo huhitajika ili kuhakikisha uwepo wa ugonjwa. Wazee nao pia huweza kuathirika na
ugonjwa huu.

Mfumo wa mkojo ni ule ambao miili yetu hutengeneza na hata kuutoa mkojo nje ya mwili. Na unahusisha sehemu kuu nne:-
  • Figo(Kidney), ambazo ni ogani zilizo na umbo la haragwe na zinakuwa mbili, na ukubwa wake ni kadirio la unavyokunja ngumi yako. Kazi ya figo ni kuchuja damu na matokeo yake ni mkojo unaotengenezwa na hutolewa kama uchafu  mwilini.
  • Mirija ya kutoka figo kwenda kwenye kibofu( ureters), huwa ni miwili na hupeleka mkojo kwenda kwenye kibofu.      
  • Kibofu, ambacho kazi yake ni kukusanya na kuhifadhi mkojo unaotoka katika figo,mkojo hutolewa pale mtu anapoamua kukojoa.      
  • Mrija wa kutoa mkojo kutoka kwenye kibofu(urethra), huu ni mrija mmoja ambao hutoa mkojo nje mtu anapoamua kukojoa.

UTI husababishwa kwa kiasi kikubwa na bakteria ambao huingia katika mrija wa kutoa mkojo kutoka katika kibofu. Asilimia kubwa ya ugonjwa huu katika jamii husababishwa na bakteria ajulikanaye kama Escherichia coli(E Coli), Pia asilimia ndogo yaweza kusababishwa na aina nyingine ya bakteria ajulikanaye kama Staphylococcus saprophyticus.Lakini pia kwa uchache sana ugonjwa waweza kusababishwa na fangasi au virusi.

Ugonjwa huu ambao hauko katika kundi la magonjwa ya zinaa, lakini kufanya ngono wakati mwingine husababisha kuambukizwa kwa ugonjwa huu
Dalili za UTI hutofautiana kulingana na sehemu ya njia ya mkojo iliyoathirika.
Jedwali
Sehemu iliyoathirika
Dalili
Figo

  •  Kichefuchefu.
  • Kutapika.
  • Maumivu ya mgongo wa juu.
  • Homa kali.
  • Kutetemeka na kusikia baridi
Kibofu

  • Damu katika mkojo.
  • Maumivu ya nyonga.
  • Maumivu chini ya kitovu.
  • Kukojoa mara kwa mara na kupata maumivu wakati wa kukojoa.

Mrija wa kutoa mkojo kutoka kwenye kibofu (urethra)

  • Mkojo wa kuunguza wakati wa kukojoa(maumivu njia ya mkojo)

Siyo mara zote ambazo mtu hupata dalili za ungonjwa huu, lakini zinapotokea huwa ni kama ifuatavyo:- Kujisikia haja ya kukojoa mara kwa mara, kusikia maumivu wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara mkojo kidogo, mkojo wa rangi ya mawingu mawingu, mkojo mwekundu au pink, pia wa rangi ya brauni, mkojo unaotoa harufu, maumivu ya nyonga kwa wanawake na maumivu kwenye njia ya haja kubwa kwa wanaume. Endapo utakuwa na dalili hizo zilizotajwa awali ni vyema kupata ushauri wa daktari.

Uambukizi wa njia ya mkojo hutokea kama bakteria wataingia katika mrija wa kutoa mkojo kutoka katika kibofu, na huzaliana na kuongezeka katika kibofu. Ingawa bakteria hawa waweza kuishi katika kibofu bila kuleta madhara, lakini wakati mwingine kinga ya mwili hushindwa kufanya kazi ipasavyo na uambukizi hutokea. Uambukizi unapotokea ndipo mgonjwa anaweza kuona dalili mbalimbali tulizoziona awali.

Kama tulivyoona awali mara nyingi ugonjwa huu huwaathiri zaidi wanawake na sababu kubwa ikiwa ni ya maumbile.
  • Uambukizi katika mrija wa kutoa mkojo kutoka katika kibofu (Infection of the urethra)-Aina hii ya UTI hutokea endapo bakteria wanaopatikana tumboni watasambaa kutoka njia ya haja kubwa na kuingia katika mrija wa mkojo. Na kwa kuwa mrija wa kutoa mkojo uko karibu uke mwanamke anaweza pia kuambukizwa UTI kwa kufanya ngono, ambapo vijimelea kama gonococcus na chlamydia vinaweza kusabisha aina hii ya UTI.
  • Uambukizi katika kibofu- Aina hii ya UTI mara nyingi husababishwa na bakteria aina ya  E coli,  bakteria hawa hupatikana tumboni.Maumbile ya uke kuwa karibu ya njia ya aja kubwa huchangia sana bakteria hawa kuweza kuingia kwa urahisi katika njia ya mkojo na kusababisha uambukizi.


Walio katika hatari ya kupata ugonjwa.
  • Wagonjwa walioingiziwa mpira wa kusaidia kutoa mkojo(catheter) huwa katika hatari kubwa ya kupata UTI. Hii inajumuisha wagonjwa waliolazwa, wenye matatizo ya magonjwa ya fahamu na hawawezi kutoa mkojo, pia wagonjwa  waliopooza.
  • Wagonjwa walio na kinga ya mwili iliyoshuka, mfano wale wenye kisukari na magonjwa mengineo yanayoshusha kinga ya mwili dhidi ya vijimelea vya magonjwa, wanakuwa katika hatari ya kupata ugonjwa huu.
  • Wagonjwa walioziba njia ya mkojo, hii inaweza kusababishwa na mawe ya kwenye figo na kukua kwa tezi dume kwa wanaume, hii husabisha mkojo wenye bakteria kushindwa kutoka na kusababisha uambukizi katika kibofu na figo.
  • Hitilafu katika njia ya mkojo- inawezekana mtoto kuzaliwa na hitilafu hii ambayo husababisha mkojo kushindwa kutoka kwa urahisi na kuchochea maambukizi haya ya UTI.
  • Ukomo wa hedhi, hii ni kwa sababu homoni ya ostrogeni hupungua na kusababisha mabadiliko katika njia ya mkojo.
  • Matumizi ya njia za uzazi wa mpango, ambayo vipandikizi huwekwa katika njia ya kizazi(diaphragm).Yaweza pia kuchochea kupata maambukizi haya.
  • Kuwa katika umri wa matamanio ya kufanya ngono. Wanawake walio katika umri wa matamanio ya ngono wameonekana kuthirika zaidi ya wale wasio na matamanio ya ngono.
  • Kuwa mwanamke, wanawake wana mrija mfupi wa kutoa mkojo kutoka katika kibofu ukilinganisha na wanaume. Kwa hiyo huwa ni rahisi kwa bakteria kufikia kibofu kwa wanawake, na kupata uambukizi.


Ugonjwa wa UTI unapotibiwa mapema, hupona kwa urahisi na hakuna madhara yeyote atapata mgonjwa. Lakini ugonjwa usipotibiwa na kuwa sugu madhara huweza kutokea. Madhara haya ni kama kuharibika kabisa kwa figo endapo mgonjwa ataishi na ugonjwa kwa muda mrefu bila kutibiwa. Athari hizi huwa ni zaidi kwa watoto ukilinganisha na watu wazima. Mwanamama mjamzito asiyetibiwa ugonjwa, anaweza kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo au aliye njiti.

Mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa hufanyiwa vipimo vya kimaabara. Kwa uchunguzi zaidi bakteria huoteshwa katika maabara ili kuweza kugundua ni aina gani ya bakteria waliosababisha ugonjwa  na uchunguzi huu husaidia katika kuchagua tiba iliyo sahihi.

Vipimo vingine vya picha za ndani ya mwili vyaweza kutumika ili kuchunguza endapo mgonjwa amepata madhara katika njia ya mkojo. Vipimo hivi ni kama CT scan, ultrasound na X ray .

Pia mkojo waweza kuchunguzwa katika maabara kuangalia uwepo wa chembechembe za seli nyeupe za damu, seli nyekundu za damu au hata uwepo wa bakteria. Ni vyema mgonjwa anapotoa mkojo wa uchunguzi kuhakikisha mkojo huo hauingii vijimelea kutoka katika mazingira ya anapotolea mkojo huo.

Kamwe usitumie dawa bila ya kupata ushauri wa daktari na vipimo kuhakikisha aina ya ugonjwa. Baada ya vipimo onana na mfamasia kwa ajili ya dawa na ushauri kuhusu matumizi ya dawa.

Kwa ugonjwa usio sugu dawa kama Sulfamethoxazole-trimethoprim (Septrin) yaweza kutumika, Amoxiccilin+clavulanic acid (Augumentin), Nitrofurantoin na Ciprofloxacin zaweza kutumika kutibu ugonjwa.

Kwa kawaida dalili za ugonjwa hutoweka siku chache baada ya kuanza kutumia dawa, lakini hiyo siyo sababu ya kuacha kutumia dawa. Unaweza hitajika kutumia dawa zako kwa muda wa zaidi ya siku saba ili upone kabisa. Tumia kozi nzima ya antibiotiki kama ulivyoelekezwa na mfamasia wako ili kuhakikisha uambukizi unamalizika kabisa. Pia waweza kupewa dawa za kuondoa maumivu katika njia ya mkojo.

Mgonjwa anaweza kutibiwa pia kwa kuongezewa ostrogeni kama UTI inaambatana na ukomo wa hedhi (postmenopausal UTI)

Uambukizi ulio sugu hutibiwa baada ya uoteshaji wa bakteria katika maabara ili kuweza kugundua antibiotiki ifaayo zaidi. Mara nyingi mgonjwa huwa na kozi ndefu ya antibiotiki, na mara nyingine huitajika antibiotiki za kutumia kwa njia ya mishipa ya damu (Sindano)

Jinsi ya kujikinga na UTI
  • Epuka bidhaa za wanawake zenye antiseptiki, bidhaa hizi huuwa bakteria wenye faida(normal flora) na wanaoimarisha kinga ya mwili kwenye uke. Bidhaa hizi kama dochi,poda, sabuni, deodoranti zaweza kusababisha upate uambukizi kwa urahisi.
  • Jifute kuanzia mbele kwenda nyuma, hii ni baada ya haja ili kuepuka kuwapeleka bakteria wa tumboni katika mrija wa mkojo.
  • Kunywa vimiminika kwa wingi, hususani maji,hii husaidia kupata mkojo mwingi na kukojoa mara nyingi na kuwaondoa bakteria kutoka katika kibofu na kuepuka uambukizi.
  • Hakikisha bafu na choo vinafanyiwa usafi wa hali ya juu.
  • Hakikisha vyombo na vifaa vya bafuni na chooni ni visafi na maji yanayotumika pia ni safi. Waweza kutumia water guard kuhakikisha maji ya bafuni na chooni ni safi.
  • Matumizi ya tamponi yahitaji usafi wa hali ya juu, kwa kuwa waweza kuingiza katika uke bakteria wasababishao ugonjwa.
  • Wanawake waepuke nguo zinazobana, Nguo zisizobana husababisha uke kupata hewa na kuwa mkavu na kuepuka uvamizi wa bakteria. Epuka suruali za jeans zinazobana hususani katika maeneo yenye joto. Chagua nguo za ndani zenye fiba za asili, mfano nguo za pamba.
  • kama unasumbuliwa na tatizo hilo na umetibiwa maeneo mbalimbali bila mafanikio tufikie haraka lupimo sanitarium clinic tukutibu kwa kutumia matunda na mimea 

    VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,


    kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni