Tatizo la Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi(Uterine fibroid)
Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi hutokea kwenye misuli laini (smooth muscle)
ya mfuko wa uzazi. Ni uvimbe ambao siyo saratani(benign tumor). Majina
yalizoeleka ni myoma au uterine fibroid.
Myoma ni aina ya uvimbe ambao unaowaathiri wanawake wengi hasa katika umri wa miaka
ya uzazi.
Dalili
Uvimbe ukiwa mdogo unaweza usiwe na dalili zozote. Dalili hutegemea
sehemu ulipo kwenye mfuko wa uzazi na ukubwa wake. Hatahivyo dalili zake
ni kuvuja damu bila kufuata mpangilio wa mzunguko wa mwanamke, kutoka
damu nyingi au maumivu wakati wa hedhi, maumivu ya tumbo, maumivu ya
mgogo, kukojoa mara kwa mara au mkojo kujifungia na wakati mwingine
ugumba.
Pia mwanamke anaweza kusikia maumivu wakati wa kujamiiana, na huweza kusababisha mimba kutoka.
Ingawaje wanawake wengi hupata uvimbe kwenye mfuko wa uzazi lakini sio sababu hasa ya ugumba au utasa.
Uchunguzi
Daktari anaweza kuhisi uvimbe kwa kutumia mikono miwili anapokuwa ana
pima tumbo;hatahivyo kipimo cha Ultrasound ya nyonga hutumika kugundua
uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke. MRI pia huweza kutumika kupata
usahihi wa ukubwa na eneo uvimbe ulipo.
Tatizo hili mara nyingi huambatana na maradhi mengine.Maradhi hayo ni kama
.Upungufu wa damu
.Kufunga choo
.matatizo ya fingo
.mara chache huweza saratani
Matibabu
Matibabu ya tatizo hili yanaweza kulenga kutibu dalili, au kupunguza
uvimbe. Hata hivyo kama ugonjwa huu hauna dalili unaweza kutazamiwa tu
bila kuchukua hatua zozote. Mwanamke akikoma siku zake tatizo hili huwa
linatoweka.
kwa msaada zaidi na mawasiliano unaweza kutufikia lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni