YAFAHAMU HAYA MAMBO MUHIMU KUHUSU UGONJWA WA KIFAFA
Kifafa ni ugonjwa unaosababishwa na matatizo katika mfumo wa fahamu ya mwili na mara nyingi ugonjwa huu huambatana na mhusika kuanguka huku akitetemeka na mara nyingine hutokwa na povu mdomoni au kutokwa na haja ndogo (mkojo) bila kujitambua kujielewa na oia mgonjwa huweza kung’ata midomo au ulimi pale anapokumbwa na tatizo hili.
Kimsingi chanzo cha ugonjwa huu hakifahamiki vizuri kitaalamu lakini
miongoni mwa vihatarishi au mambo yanayoweza kumfanya mtu apate ugonjwa
huu ni pamoja na kuwa na historia ya kifafa katika familia yaani
(Kurithi), matatizo ya mishipa ya damu katika ubongo, maambukizi katika
ubongo mfano homa ya uti wa mgongo, mtoto kuzaliwa kabla ya umri wake,
Chanzo kingine ni ajali mbaya katika eneo la ubongo, kukosekana kwa
hewa ya kutosha katika ubongo, mtoto kupatwa na degedege mara kwa mara
katika miezi ya mwanzo ya kuzaliwa kwake, uvimbe katika ubongo na sababu
nyinginezo.
Pamoja na visababishi hivyo hapo juu, wakati mwingine kumekuwepo na vitu vinavyochochea mtu apatwe na dalili hizo (kuanguka kifafa), mfano wa vichochezi ni pamoja na kutokula vizuri, hali ya hewa, msongo wa mawazo pamoja na mazingira yenye kelele.
Utambuzi wa kifafa hufanyika kitaalamu kwani siyo kila mtu anayeanguka na kutetemeka basi huwa na kifafa, inawezekana likawa ni tatizo lingine. hivyo ni vyema kuwaona wataalam inapotokea tatizo hili.

Mtu mwenye kifafa huweza kukumbwa na madhara mbalimbali ikiwa ni
pamoja na kupoteza viuongo vyao muhimu ikiwa pale atakapoanguka ataumia,
hivyo ni vizuri pale unapojihisi kuwa na tatizo hili ukawashirikisha
ndugu na jamaa zako wa karibu kwa lengo la kupata ufumbuzi wa tatizo
lako.
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu
namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni