Jumamosi, 26 Machi 2016

     TUMIA FURSA HII KUJUA FAIDA ZA ZABIBU





Matunda haya inaelezwa kwamba yalianza kulimwa huko nchini Uturuki, lakini kwa hapa kwetu nchini yanapatikana sana mkoani Dodoma.

Matunda haya huwa na rangi nyekundu iliyoiva, nyeusi, bluu ya kukoza , njano, kijani na hata pinki, licha ya kwamba hapa kwetu Tanzania wengi tumezoea yale ya rangi nyeusi.

Zabibu ni moja ya tunda lenye sifa nyingi na nzuri zaidi kutokana na uwezo wake wa kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hususani ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo.

Pia zabibu husaidia damu kuwa nyepesi na kuifanya isigande  ndani ya mishipa ya damu, hivyo mtumiaji wa zabibu hupunguza hatari ya kupata kiharusi (stroke)

Tunda hili pia husifika kwa kutibu tatizo la upungufu wa damu, hususani kwa wale wanaotumia mara kwa mara tunda hili huwasaidia kuepukana na ugonjwa wa bawasili pia.

Hali kadhalika zabibu pia husaidia katika tiba na kinga dhidi ya magonjwa ya ini kutokana na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi.

Mbali na faida hizo, pia zabibu kutokana na kuwa na sukari yake ya asili hivyo huweza kumsaidia mtu katika kupunguza uchovu wa mwili na kutibu maumivu yasiyokuwa na sababu za moja kwa moja.


Sambamba na hayo, juisi ya zabibu (divai) husaidia tumbo na utumbo kufanya kazi kwa ufasaha zaidi na kuzuia ukavu wa haja kubwa , lakini pia divai huimarisha afya ya mishipa ya damu katika mfumo wa kumeng’enya, kusaga na kusharabu chakula na viini lishe.

Lakini pia kutokana na madini yaliyomo ndani ya zabibu huifanya divai kuwa ni dawa nzuri inayopunguza maumivu ya tumbo yanayotokana na kujiminya kwa misuli ya kuta za matumbo (antispasmodic effect)

Hizo ndio baadhi ya faida za zabibu ambazo mtumiaji huweza kuzipata pale anapotumia tunda hili mara kwa mara.
 
 kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni