Jumapili, 27 Machi 2016

TANGAWIZI NI MKOMBOZI WA MATATIZO MBALIMBALI YA KIAFYA LIKIWEMO HILI LA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME



Tangawizi ni kati ya kiungo mahili chenye uwezo wa kuchochea ladha nzuri katika vyakula vya aina mbalimbali na hata kuwavutia walaji kula chakula husika.


Tangawizi pia inapowekwa katika vyakula vigumu kama nyama kwa muda fulani husaidia kulainisha na hivyo kuweza kuiva haraka zaidi.

Kutokana na tangawizi kutumiwa sana na wanawake hususani wanapoandaa vyakula mbalimbali kwa ajili ya familia au biashara, wengi wanaifahamu zaidi kama kiungo na si vinginevyo.

Wakati tangawizi ikiwa imekuwa maarufu kama kiungo, matabibu wa tiba asili wao wanasema tangawizi inasaidia kuondoa maumivu kwa magonjwa zaidi ya 72 yanayozisumbua jamii nyingi.

Miongoni mwa magonjwa ambayo mgonjwa anaweza kupata nafuu kutokana na kutumia tangawizi ni pamoja na kuondoa gesi tumboni kwa wenye tatizo hilo.

Tabibu wa tiba asili, John Lupimo anasema tangawizi inapotumiwa vizuri husaidia kuwezesha mmeng’enyo wa chakula tumboni na hivyo kuondoa changamoto mbalimbali za matatizo ya matumbo.

  Tabibu John Lupimo anasema, tangawizi pia husaidia kwa wenye kifafa au msongo wa mawazo kupata nafuu na kuondokana na matatizo hayo.

Mtaalam huyo anafafanua kuwa, kifafa kinasababishwa na mishipa kuvimba na kukandamiza ubongo na kwamba tangawizi inapotumika husaidia kuondoa mafuta katika mishipa hiyo.

Tabibu John Lupimo anaendelea kusema kwamba, kwa wanaume wenye tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na hivyo kupoteza hamu ya tendo la ndoa wanapotumia tangawizi wanaweza kupata nafuu ya tatizo hilo.

Anasema  tangawizi inauwezo mkubwa wa kuongeza joto katika mwili wa binadamu na hivyo kuamsha mishipa ya fahamu katika mwili wa mwanaume mwenye tatizo hilo.

Aidha, kwa upande wa kinamama wanaonyonyesha tangawizi inachochea ongezeko la maziwa na hivyo kumuondolea mama changamoto ya uhaba wa maziwa unaowakabili baadhi ya kinamama wanaonyonyesha.

Tabibu John Lupimo anaeleza kuwa mara nyingi vyakula vinavyosindikwa protini zinakuwa zimekufa na kusababisha tumbo kujaa gesi na hivyo kupungua hamu ya kula, lakini matumizi ya tangawizi husaidia kuondoa changamoto hiyo.

Pia wenye uzito mkuwa wanashauriwa kutumia tangawizi kwa sababu inasaidia kupunguza hali hiyo kwa kiwango kikubwa. 

Hali kadhalika tangawizi ni msaada mkubwa kwa wanawake wenye tatizo maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi.

“Chukua kijiko kidogo cha chai chenye unga wa tangawizi kisha changanya na maji au chai kikombe kimoja halafu mtumiaji atumia asubuhi na jioni,” anasema mtaalam huyo.
 
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni