Jumatatu, 28 Machi 2016

ZIFAHAMU FAIDA ZA LIMAO KAMA TIBA




Limao ni tunda dogo ambalo mara nyingi hutumika jikoni katika shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukata shombo katika vyakula mbalimbali mfano samaki. Asili ya tunda hili ni Asia.

zipo faida nyingi  za kutumia limao, hasa wakati wa asubuhi wakati mwili umekaa bila kula usiku kucha, miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuusaidia mwili katika suala la mmeng’enyo wa chakula na kulifanya ini liweze kufanya kazi vizuri.

  Limao pia huwasaidia wale wenye matatizo ya tumbo, malaria, dosari katika figo, kiungulia na kuongeza hamu ya chakula.

Limao husaidia wale wenye matatizo ya tumbo, kikohozi, mafindo findo, mafua, kisukari,  homa pamoja na kusaidia kuleta harufu nzuri kinywani hii ni kwa sababu aside iliyopo kwenye maji ya limao husaidia kuua bacteria walioko mdomoni wanaosababisha harufu mbaya ya kinywa, ni vizuri ukatumia limao baada ya kusafisha meno.

malimao yana asid, ambayo ni chanzo kizuri cha vitamin C, ambayo ni nzuri kuzuia baridi na homa, lakini malimao pia husaidia kuzuia saratani ya damu.

Pumu, malengelenge, uvimbe na vidonda pia vyote hivyo huweza kutatulika endapo mhusika atazingatia matumizi sahihi ya limao.

Pia maganda ya limao yanapotumika kwa kusugulia ngozi huwa ni dawa ya vipele, junjua na kuungua.

Pia maji ya limao huweza kuondoa makovu na mikunjo kwenye ngozi na kupunguza makovu makubwa kama ukinyunyizia kila mara. Hali kadhalika kutokana na uwezo wake wa kusafisha damu, maji ya limao huacha ngozi ikiwa inang’aa na yenye afya.

Hata hivyo, ni vizuri ukapata ushauri zaidi kutoka kwa wataalam kabla ya kuamua kuanza kutumia limao kama tiba ili uweze kutumia kwa usahihi zaidi pasipo kuwa na madhara kwako. Pia unaweza kufika lupimo sanitarium clinic kwa ushauri na matibabu zaidi, 


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni