Jumatano, 9 Novemba 2016



MVURUGIKO WA HOMONI (HORMONE IMBALANCE) KWA WANAWAKE


DALILI ZA MVURUGIKO WA HOMONI (HORMONE IMBALANCE) KWA WANAWAKE

 wasiliana sasa na tabibu john lupimo juu ya makala hii kwa namba 0759324414

UPUNGUFU WA HOMONI YA PROGESTERONE

Hii ndio aina kubwa zaidi ya mvurugiko wa homoni inayowasibu wanawake wengi sana wa rika zote. Vyanzo mara nyingi huwa ni mfumo wa ulaji pamoja na matumizi ya njia mbalimbali za uzazi wa mpango. Dalili zake ni pamoja na:
— Premenstrual syndrome (Hali inayomkumba mwanamke wiki moja hadi mbili kabla ya kuona siku zake kama uchovu, miwasho sehemu za siri, vipele vyekundu au vyeusi hasa usoni, pamoja na mabadiliko ya mood)
— Kutoka kwa mimba
— Kuongezeka uzito ghafla
— Wasiwasi (Anxiety)
— Kukosa usingizi
— Maumivu au Vimbe kwenye maziwa
— Kupata Kizunguzungu mara kwa mara
— Ugumba

UPUNGUFU WA ESTROGEN

Aina hii ya mvurugiko wa homoni ipo zaidi kwa wanawake wanaopitia ukomo wa hedhi kutokana na umri (menopause). Wanawake wembamba huathiriwa zaidi na upungufu huu wa homoni ya estrogen kuliko wanawake wengine. Dalili zake ni :
— Ukavu ukeni
— Maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa— Bladder Infections
— Homa za vipindi
— Kuvuja jasho usiku
— Matatizo ya kukumbuka
— Kujisikia mvivu na mzito kufanya mambo au kazi

ONGEZEKO LA ESTROGEN

Unaweza ukawa na estrogen ya ziada kama utakuwa umetumia vidonge/matibabu ya homoni za kutengenezwa maabara/zisizo za asili ambavyo mara nyingi hupewa wanawake wanaopitia menopause. Dalili kuu ni pamoja na:
— Tumbo kujaa gesi/kuvimba/kukaza
— Kuongezeka uzito ghafla
— Mabadiliko ya hisia mara kwa mara (Mood swings)
— Wasiswasi (Anxiety) au Msongo wa mawazo
— Kukosa usingizi
— Vipele vyekundu usoni
— Kuota kwa vinyama/vipele kwenye via vya uzazi
— Kuvimba kwa maziwa
— Utakaji mwingi wa damu wakati wa hedhi
— Maumivu ya kichwa ya mara kwa mara
— Kupoteza kumbukumbu na uzito wa kufikiria

UTAWALA WA ESTROGEN (Estrogen Dominance)

Hali hii hutokea pale mwili unaposhindwa kutengeneza homoni ya progesterone ya kutosha kuweza kuleta uwiano na estrogen. Dalili zake:
— Premenstrual syndrome (Hali inayomkumba mwanamke wiki moja hadi mbili kabla ya kuona siku zake kama uchovu, miwasho sehemu za siri, vipele vyekundu au vyeusi hasa usoni, pamoja na mabadiliko ya mood)
— Kutoka kwa mimba
— Kuongezeka uzito ghafla
— Wasiwasi (Anxiety)
— Kukosa usingizi
— Maumivu au Vimbe kwenye maziwa
— Kupata Kizunguzungu mara kwa mara
— Ugumba
— Tumbo kujaa gesi/kuvimba/kukaza
— Vipele vyekundu na chunusi hasa usoni na ngozi kuwa na mafuta sana
— Maumivu ya kichwa ya mara kwa mara
— Kupoteza kumbukumbu na uzito wa kufikiria

KIWANGO CHA JUU CHA ANDROGEN

Homoni ya Androgen ni homoni ya kiume. Wanawake wanaweza kupata tatizo la ongezeko la homoni hii kiwango kisichohitajika kwa kula vitu vyenye sukari sana au kwa kula wanga sana. Pia wanawake wanao kumbwa na tatizo la tatizo la polycystic ovary syndrome (PCOS) wako hatarini zaidi kupata tatizo la uwiano wa homoni hii ya androgen kuvurugika. Dalili zake ni:
— Vipele vyekundu na chunusi hasa usoni na ngozi kuwa na mafuta sana
— Mwanamke kuota ndevu, na vinyoleo vingi mikononi na miguuni
— Nywele nyepesi
— Ugumba
— Sukari kushuka (Hypoglycemia)
— Ovarian Cysts

UPUNGUFU WA HOMONI YA CORTISOL

Hali hii hutokana na tezi (adrena glands) kufanya kazi kupitaliza hali ambayo mara nyingi husababishwa na msongo wa mawazo wa muda mrefu-yani wale watu ambao muda mwingi huwa wenye mawazo. Dalili zake ni:
— Uchovu usioisha
— Uzito wa kufikiria na kufanya maamuzi
— Ngozi kuwa nyepesi na kavu
— Madoa doa usoni
— Sukari ya chini
— Wastani wa sukari usio imara (inapanda na kushuka mara kwa mara)
— Kushindwa/kutovumilia kufanya mazoezi
Kama unadalili mbili au zaidi kati ya zilizo ainishwa hapo juu unaweza ukawa na tatizo la mvurugiko wa uwiano wa homoni (Hormone imbalance). Ni vyema kupata ushauri kutoka kwa Daktari akaweza kukupendekezea tiba ya kukusaidia tatizo lako.

Kwa maswali na ushauri unaweza kumpigia tabibu john lupimo kwa namba 0759324414 karibu sana

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni