Jumatatu, 7 Novemba 2016

  Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi

  KWA SWALI LOLOTE JUU YA MAKALA HII YA UZAZI NIPIGIE SIMU KWA NAMBA 0759324414

 


 
MIMBA inayotungia nje ya mfuko wa uzazi kwa kitaalamu inafahamika kama ectopic pregnancy. Hii mimba inayotungia nje ya mfuko wa kizazi huwa inakaa ndani ya mirija ya uzazi. Mimba kama hii huwa anaipatapa mwanamke kwa njia ya kawaida au anaweza kuipata kwa njia ya upandikizaji.
 
 Mimba hii inaweza kutokea ndani ya mirija ya uzazi ila wataalamu wanasema kwamba zaidi ya asilimia 97 huwa inatokea kwenye mirija ya uzazi.
 
Sababu
 
Uharibifu wa mirija ya uzazi
Mara nyingi uharibifu wa mirija ya uzazi kwa njia yoyote ile ndio huwa inapelekea kutokea kwa utungaji wa mimba nje ya mfuko wa uzazi ambayo hujiotesha katika mirija ya uzazi na hatima yake huleta shida na matatizo makubwa.
 
Kwanza ieleweke mwanamke anaweza kupata mimba hii bila sababu yoyote na si kila mwanamke ambaye anapata ectopic pregnancy aliwahi kuwa na kisababishi fulani.
Lakini wanawake wengi wanapata hizi mimba kutokana na sababu nyingi mbalimbali. Mara nyingi mwanamke ambaye alishawahi kupata mimba ambayo imetunga nje ya mfuko wa uzazi ana hatari tena ya kupata tatizo hili.
 
Kujaa maji kwa mirija ya uzazi
Tatizo la kujaa maji kwa mirija ya uzazi linaweza kusababisha mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi. Kama mrija mmoja wa mwanamke utakuwa na maji ukazuia yai moja kupita na mimba ikatunga pale pale hata kama mrija huo utakatwa maambukizi yatakuwa tayari yamehamia katika mrija wa upande wa pili. Kwa hiyo mwanamke ana hatari ya kupata tena mimba itakayotunga nje ya mfuko wa uzazi.
 
Kutokea kwa vimbe mbalimbali katika mfuko wa kizazi
Kuna vitu vingi ambavyo huweza kusababisha tatizo hili ikiwemo pia kutokea kwa vimbe katika mirija ya uzazi nazo huweza kusababisha mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi.
Maambukizi ya magonjwa ya ngono
Tatizo jingine ambalo linaweza kusababisha mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi ni maambukizi ya magojwa ya ngono kama gonorea na magonjwa ya zinaa.
Hivyo mwanamke ambaye ameugua magonjwa haya huko nyuma ana hatari kubwa ya kupata ectopic pregnancy kwa sababu madaktari wanasema kitendo cha kuugua magojwa ya ngono kinamsababishia wanamke kupata tatizo la PID.
Lakini si magojwa ya ngono pekee hata yale ambayo hayaambukizwi. Wako bacteria mbalimbali ambao mwanamke anaweza kuwapata kupitia njia mbalimbali nao wanaweza kufanya tatizo hili.
Lakini pia kisababishi kingine ni utoaji wa mimba wa mara kwa mara sambamba na mimba kutoka

Dalili za mimba kutunga nje ya kizazi
Kwa kawaida mimba ambayo inatungia nje ya uzazi muda mwingi huwa haionyeshi dalili hadi pale zinapokaribia wiki sita au nane baada ya mwanamke kuona hedhi yake ya mwisho.
Kwa ukubwa wa mimba ile inaweza kuwa tayari ikawa imeshazidi uwezo wa kuhimili uwezo wa mirija ya uzazi na hivyo kumfanya mwanamke kupata maumivu makali tumboni chini ya kitovu.
Kuona siku wakati ni mjamzito
Dalili nyingine ni mwanamke kupata matone ya damu wakati mwanamke ni mjamzito.
Hii ni moja ya dalili lakini dalili nyingine ambayo ni mbaya zaidi ni pale mwanamke ambapo anakuwa na mimba ambayo imetungia nje ya mfuko wa uzazi na ikaendelea kukua hufikia wakati ikapelekea kupasuka kwa mirija ya uzazi na kusababisha mshipa mkubwa wa damu ambao ni Ateri kupasuka na hatimaye kumwaga damu nyingi tumboni.
Maumivu haya huweza kuwa makali na yanayokata kama kisu. Yanaweza kuwa upande mmoja zaidi wa nyonga ingawa si lazima yawe upande ulio na mimba. Na muda mwingine mwanamke hupoteza fahamu.

kwa ushauri zaidi juu ya halii ambayo ni hatari kwako wewe mama ambae unatarajia kushika ujauzito au unaujauzito na unaziona dalili nilizozitaja nipigie simu sasa hivi kwa namba 0759324414 karibu sana

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni