Leo hii tutazungumzia kuhusu maradhi ya kutazama
maradhi yanayoathiri watu wengi zaidi nayo si mengine bali ni pumu ya
ngozi au kwa kitaalamu huitwa Eczema.
Pumu ya ngozi (Eczema)
Pumu ya ngozi au kwa kitaalamu Eczema (atopic
dermatitis au atopic eczema) ni maradhi ya ngozi ambayo yamefanyiwa
utafiti muda mrefu sana na kusema ukweli andiko langu hili halitoweza
hata kuandika robo ya yale yanayofahamika kitaalamu kuhusiana na pumu ya
ngozi.
Maradhi haya kwa kifupi yamekuwa yakiathiri watoto
wengi ulimwenguni na yamekuwa yakisumbua akili za wanasayansi na
watabibu kote ulimwengu kwa muda mrefu.
Neno Eczema ambalo ndio jina la maradhi haya kwa
kitaalamu ni neno la Kigiriki na linamaanisha kututumka sehemu ya nje ya
ngozi, hali ambayo huonekana pale mtoto anapopata maradhi haya.
Maradhi haya ya ngozi yanachangia asilimia arobaini (40) ya maradhi yote ya ngozi yanayoripotiwa hospitalini.
Shambulizi lake
Maradhi haya hushambulia zaidi watoto na huweza
kupitiliza mpaka ukubwani, pia lakini kwa wengi huwa yanapungua kadri
mtoto anavyokua. Watafiti mbalimbali wanasema kuwa kumekuwa na ongezeko
la maradhi haya katika kipindi cha miaka ya usoni hali inayoashiria kuwa
maradhi haya ni ya kurithi (atopic eczema)
Karibu asilimia themanini (80) ya wagonjwa wa pumu
ya ngozi huanza kuugua maradhi haya wakiwa chini ya umri wa miaka
mitano (5). Wagonjwa wengi pia huonyesha dalili za maradhi haya wakiwa
na umri chini ya mwaka mmoja.
Maradhi haya pia huweza kujitokeza ukubwani ingawa ni mara chache sana hali hii huonekana.
Maradhi haya huathiri watu wa jinsia zote kwa uwiano sawia yaani wanaume na wanawake.
Dalili zake
Maradhi haya ni ya muda mrefu nikimaanisha kuwa
mtu huweza kukaa nayo kwa muda mrefu, ingawa si kuwa muda wote ngozi
huonyesha dalili za maradhi. Watu wenye maradhi hupitia vipindi ambavyo
ngozi hututumka na kuonyesha dalili za maradhi na vipindi ambavyo ngozi
huonekana kama imepona ovyo kutoonyesha dalili yoyote ya maradhi.
Dalili za pumu ya ngozi ni kama zifuatazo:
-Sehemu ya ngozi iliyoathirika huwa inakuwa kavu (inaonekana kavu),
-Sehemu ya ngozi iliyoathirika huwa inatutumuka,
-Ngozi huwasha na kama ukikuna kwa muda mrefu basi hupasuka na kuweza kusababisha vidonda.
-Eneo la ngozi lililoathirika mara nyingine huuma.
-Ngozi huwa inakua na mipasuko inayoweza kuruhusu vimelea vya maradhi kushambulia sehemu za ndani za ngozi.
-Muwasho wa ngozi huwa mkali zaidi nyakati za usiku
-Maeneo yenye athari huwa yanavimba (au kututumka) na kuwa na joto.
-Maeneo ya ngozi yaliyoathirika huweza pia kuwa na malengelenge na hata kutoa majimaji.
Kama una swali,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu
namba 0769368546,0719097574 na 0754301115
pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni