Jumanne, 23 Juni 2015

FAHAMU MASHAMBULIZI YA FANGASI YA SEHEMU ZA SIRI NA ATHARI ZAKE

https://www.dermquest.com/imagelibrary/large/037764HB.JPG
Kuna aina nyingi sana za magonjwa ya Fangasi,lakini kwa leo hebu tuangalie kuhusu Tinea cruris. Aina hii ya fangasi ndiyo inayofahamika na Watanzania wengi zaidi ya aina nyinginezo na waathirika huwashwa sana sehemu za siri.

Dalili zake
Kuna dalili nyingi sana za ugonjwa huu lakini kubwa kuliko zote ni kuwa fangasi hawa huambatana na muwasho mkali wa eneo lenye maambukizi hasa sehemu za siri, rangi ya ngozi ya eneo lenye maambukizi hubadilika na kuwa na muundo wa duara, mfano wa sarafu.

Dalili nyingine ni ngozi kukauka kisha kubanduka, na kama mgonjwa asipopata tiba mapema basi atatokwa na majimaji kwenye eneo la ngozi lililoathirika pamoja na kutoka kwa harufu mbaya kwenye eneo hilo.


UNAVYOAMBUKIZWA
Kuna njia nyingi zinazoweza kusababisha uambukizi wa maradhi haya, lakini ili uambukizaji huu uwezekane lazima kuwe na mazingira rafiki ya kuwezesha fangasi kuishi na kuhama kwa urahisi.

Mazingira haya rafiki kwa kuruhusu fangasi hawa kuweza kutoka kwa mtu mmoja au sehemu moja ya mwili kwenda kwa mwingine huhitaji uwepo wa hali ya joto pamoja na majimaji sehemu iliyoathirika na 
maambukizi hutokea kwa kugusana na mtu aliye na maambukizi tayari.

Mtu anaweza kupata maambukizi ya fangasi hawa kwa kushirikiana kimapenzi na mwenzake aliye na 
ugonjwa au kwa kushirikiana mavazi na mtu aliyekwisha pata maambukizi au kushirikiana taulo au hata 
sabuni na vifaa vya usafi wa mwili kwa mtu zaidi ya mmoja.

Watu ambao huweza kupata maambukizi ya fangasi wa sehemu za siri ni wale wanaofanya kazi 
zinazohusisha ukaaji kwenye maji yaliyotuama kwa muda mrefu, wanaoshiriki mapenzi na wenza wenye
maambukizi ya fangasi hao na wote ambao wana fangasi za kwenye vidole kwani fangasi wale wanaweza 
kuhamishwa kupitia kwenye kucha na kuhamia kwenye eneo hilo la siri;

Wengine wanaoweza kupata maradhi haya ni wale wanaofanya usafi wa mwili kwa kutumia maji yaliyobeba 

vimelea vya fangasi hao, wasiojikausha vizuri maungo ya sehemu za siri, watu wenye maradhi 
yanayosababisha kushuka kwa kinga, hususan kisukari, wanaovaa nguo zaidi ya moja hali inayosababisha 

mwili kushindwa kupunguza joto lake hivyo kutoa jasho, wanaovaa nguo za kubana sana hasa zile 
zinazobana sana kwenye maeneo ya maungo ya siri na wenye unene wa kupindukia;
Lakini watu wanaokunywa dawa za kuua vimelea (antibiotics) kwa muda mrefu au wenye ujauzito ambao 
huchangia kushuka kwa kinga ya mwili nao wanaweza kupata ugonjwa huu.

Kama una swali,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu 


namba 0769368546,0719097574 na 0754301115



pia 


www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni