KWANINI UTESEKE NA TATIZO LA TEZI DUME? (PROSTATE CANCER) INATIBIKA BILA HATA YA OPERATION.
mpigie sasa hivi na tabibu john lupimo kwa namba 0759324414 au 0673750475.
Kwa ufahamisho tu ni kwamba neno saratani ni jina la ugonjwa ambalo hutokea wakati chembechembe za uhai au seli katika sehemu fulani ya mwili zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili na kutengeneza vijiuvimbe vidogo vidogo. Ugonjwa huu ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea, hata hivyo, satarani ya tezi dume kwa sasa inawapata sana wanaume kuanzia miaka 25.
Kwa kawaida seli huwa zinajigawa, kupevuka na baadaye kufa kwa kufuata taratibu za mfumo wa mwili. Lakini seli za saratani hazifuati mfumo huo, badala ya kufa, zenyewe huishi muda mrefu kuliko chembe chembe za kawaida na wakati huohuo huendelea kutengeneza seli nyingine na kuwa uvimbe wa saratani au tumour.
Tezi dume linapatikana katika mwili wa mamalia dume tu na pale seli katika kiungo hicho zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili hapo ndipo mtu huyo hupata saratani ya tezi dume.
Ugonjwa huu pia hujulikana kama saratani ya kibofu huwapata wanaume tu na hasa wenye umri wa takriban miaka 50 na kuendelea.
Saratani hii imethibitika kushika nafasi ya pili, ukiachia mbali saratani ya mapafu kwa kusababisha vifo vya wanaume wenye umri wa takriban miaka 50 na kuendelea.
Kuna vihatarishi vingi vinavyochangia mwanaume kupata saratani ya tezi dume. Vifuatavyo ni baadhi yake: Kwanza kabisa ni umri. Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume huongezeka sana hasa ukifikia umri wa karibu miaka 50 na kuendelea.
Nasaba ni kihatarishi kingine ambapo wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu huwa katika hatari ya kupata kansa hiyo kutokana na kurithi jeni za ugonjwa huo.
Suala jingie ni lishe ambapo wanaume wanaopenda kula nyama au (red meat) na walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama huwa katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume.
Pia wanaume wasiopenda kufanya mazoezi, wanene na wenye upungufu wa virutubisho vya Vitamin E wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya kibofu cha mkojo.
Nao wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali, wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza matairi na wachimbaji madini, hususan aina ya cadmium hao wamo hatarini kupata saratani hii.
Viungo vya uzazi ya mwanaume vimegawanyika katika sehemu kuu mbili. Kuna viungo vya uzazi vya nje na vile vya ndani.
Viungo vya uzazi vya nje ni vile tunavyoviona kama uume na mfuko wa korodani.
Viungo vya uzazi vya ndani ni mirija ya mbegu za kiume ambacho ni kifuko cha akiba cha mbegu na tezi dume au tezi ‘Prostate’.
TEZI HIZI ZINA SIFA ZIPI?
Ina umbo kama yai (oval shape)
Ina ukubwa wenye vipimo hivi, upana 4cm na unene 3cm ingawaje hivi vipimo vinatofautiana kwa kila mwanaume.
Tezi hii ipo inazunguka shingo ya kibofu cha mkojo na kuzunguka mrija unaopeleka mkojo nje(urethra)
Tezi hii hua yenye ukubwa wa kawaida lakini huongezeka ukubwa kadri ya umri.
Tezi hii hutengeneza majimaji yenye rutuba ya mbegu za kiume (shahawa)
Viungo hivi vyote vina umuhimu mkubwa kwa mwanaume katika kumfanikisha kuweza kufanya tendo la ndoa kwa ufanisi pamoja na uzalishaji wa mbegu za kiume.Matatizo yakitokea katika sehemu yeyote hapo humuathiri mwanaume inategemea wapi athari ilipo.
Athari ni kushindwa kufanya tendo la kujamiiana na kuzalisha mbegu au manii. Manii ni majimaji yanayolisha mbegu za kiume na kuzisafisha na huzalishwa na tezi dume.
Chanzo cha tatizo
Hutegemea mahali linapoathirika. Matatizo hutokea popote katika viungo vya uzazi vya mwanaume iwe nje au ndani.
Uume
Matatizo kwenye uume ni kupata maumivu katika njia ya mkojo kutokana na maambukizi au kuumia njia ya mkojo.Mwanaume mwenye tatizo hili hulalamika maumivu wakati wa kukojo, muwasho katika njia ya mkojo na mkojo kutotoka vizuri.
Kuumia kutokana na kuingiziwa mrija wa mkojo mara kwa mara katika njia ya mkojo.
Maambukizi inaweza kuwa Yutiai za mara kwa mara na magonjwa ya zinaa kama kisonono na mengine.
Ugonjwa wa kaswende huathiri sehemu ya nje ya uume zaidi ambapo vipele na vidonda vyenye muwasho na maumivu hujitokeza mara kwa mara.Tatizo hili hujitokeza kama tulivyoelezea hapo juu na huchunguzwa katika vituo vya afya.
Ni vema kuwahi hospitali endapo utahisi dalili hizo kwani ukichelewa itasababisha madhara makubwa mojawapo ni kuziba kwa njia ya mkojo, kusambaa kwa maambukizi katika viungo vingine kama kibofu cha mkojo, korodani na tezi dume.
Athari nyingine ni ugumba kwa mwanaume.
.Tezi dume hupatwa na matatizo mbalimbali kama maambukizi na kutanuka hadi kuwa saratani.
Kutanuka huanzia katika umri wa miaka arobaini na tano na huanza taratibu sana.
Maambukizi ya tezi dume hutokana na muendelezo wa maambukizi toka katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu cha mkojo na kufika kwenye tezi dume.
Tezi dume ikitanuka huanza dalili za uhafifu katika utoaji wa mkojo ambapo mkojo hautoki vizuri au unashindwa kabisa kutoka. Tezi hii inapotanuka inabana shingo ya kibofu cha mkojo.
Dalili dhahiri za ugonjwa huu hujitokeza kadiri umri unavyoongezeka, hasa zaidi ya miaka hamsini na sitini.
Endapo utachelewa kupata tiba hadi umri wa zaidi ya miaka sitini, kuna hatari ya tezi hiyo kuwa kansa au saratani.Uchunguzi wa awali wa tezi dume hufanyika kawaida katika kliniki kubwa kwenye hospitali za mikoa na wilaya kabla dalili hazijajitokeza rasmi.
Kuwa na tabia ya kufanya uchunguzi mara kwa mara hasa unapofikia umri wa miaka 45 na zaidi.
Kadiri umri unavyoongezeka ndipo dalili zinapojitokeza taratibu hadi tatizo linakuwa kubwa.
Endapo utawahi kufanyiwa uchunguzi mapema , basi tezi dume inaweza kutibika au kuzuia isitanuke na ukaepuka upasuaji na saratani.
SEHEMU KUU ZA TEZI YA KIUME
1.PERIPHERAL ZONE(SEHEMU YA NJE)
~Hii ni sehemu ya nje ya tezi ambayo madakari wengi hutumia hii tezi kubaina kama kuna tatizo kwenye tezi kwani ni virahisi kiugusa km daktari akiingiza ikiingiza index fingure(kidole cha kusontea) kwenye njia ya haja kubwa. Kukua kwa sehemu hii hakuwezi kuathiri utokaji wa mkojo.
2. TRANSITIONAL ZONE(SEHEMU YA KATI)
~ Hii ni sehemu ya tezi ambayo ikikua yani ikiongezeka ukubwa tunasema KUVIMBA KWA TEZI DUME kitalamu BENIGN PROSTATIC HYPERPLASIA (BPH) kuna uwezekano mkubwa wa tezi dume iliyovimba kuzuia njia ya mkojo kupita. Kwani ndio sehemu ya tezi iliyo karibu kabisa na njia ya mkojo. Mara nyingi hii sehemu ikikua ndio inayo sababisha matatizo ya kukojoa(obstructive symptoms). Tezi hii pia daktari anaweza kuibaini kwa kutumia kidole kipomo hiki huitwa DIGITAL RECTAL EXAMINATION(DRE)
hii ni kwa sababu ikikua inasukuma ile sehemu ya pembezoni yani peripheral zone kuelekea njia ya haja kubwa. Hivyo dakatri anaweza kubaini km tezi imekua au laa.
3. CENTRAL ZONE(SEHEMU YA KATI)
~Hii sehemu iko mbele ya transitional zone hivyo uvimbe katika sehemu hii ni vigumu kubaini kipitia kipimo hiki cha haraka cha kutumia kidole hivyo tunatumia vipomo vya picha kinaitwa CYTOSCOPY. Hiki ni kipimo cha picha kinacho angalia kipofu cha mkojo na njia ya mkojo na kutoa majibu katika mfumo ya picha au video.
KUKUA KWA TEZI YA KIUME
~Kukua kwa tezi ya kiume kitalamu tunaita BENIGN PROSTATIC HYPERPLASIA (BPH). Hili tatizo mara nyingi huanza baada ya miaka 40 hivi na dalili huja kujionesha uzeeni. Hivyo tezi inaweza ikawa kubwa sana lakini haina dalili hii ni kutokana na sehemu gani ya tezi iliyovimba au kuongezeka. Tezi inapoonesha dalili jua tatizo hilo ni sugu na liko ktk hali mbaya.
DALILI ZA KUVIMBA KWA TEZI
DALILI
Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani na zile za kuvimba kwa tezi dume au BPH. Dalili hizo ni pamoja na, kupata shida wakati wa kuanza kukojoa, kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa, kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu, kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku.
Dalili nyingine ni kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote na kutoa mkojo uliochanganyika na damu. Mwanaume anapoanza kuona na kuhisi baadhi ya dalili hizo anapaswa kuwahi hospitali kupimwa.
Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu nyigine za mwili, mgonjwa anaweza kuwa na maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni.
Dalili nyingine ni za kawaida ambazo zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu na kadhalika.
2. Kubakiza mkojo kwenye kibofu
3. Kukujoa sana usiku
4. Maumivu wakati wa kukojoa
5.Kupungukiwa nguvu za kiume
6. UTI ya mara kwa mara
7. Mawe kwenye kibofu kutokana na mrundikano wa mkojo.
8. Figo kujaa maji. Hii sababu mkojo huo unarudi nyuma kuelekea figo(hydronephrosis)
9. Kupoteza fahamu(uremia), HIZI DALILI NIMEZITAJA KULINGANA NA TATIZO LINAVYOKUWA SUGU KWA MGONJWA HIVYO UGONJWA HUU NI HATARI USIPO WAHI KUTIBIWA.
KWA MAWASILIANO ZAIDI, USHAURI NA MATIBABU WASILIANA NA TABIBU JOHN LUPIMO KWA NAMBA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni