HAYA NDIO MADHARA SITA YA KUTOA MIMBA….
Kutoa mimba ni nini? Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake
mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake.
Kutokana kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani
na kutotumia njia za uzazi wa mpango kwa watu wengi walioko kwenye mahusiano,
wasichana wengi kwa sasa wanatoa mimba.
Utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba zaidi ya
asilimia tisini ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume zaidi ya
mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote ndio wanaamua
kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka tano. Sasa
unajiuliza bado kuna mtu humo au mfu?
Hata hivyo hao wanaozaa pia hujikuta wamebeba mimba zingine
wakati watoto wao wakiwa wadogo na kulazimika kuzitoa. Najua watu wengi wanatoa
mimba kukwepa aibu, kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika lakini ni bora
kutumia njia za uzazi wa mpango kama sindano na vijiti.
Hebu tuyaangalie madhara ya kutoa mimba kama ifuatavyo…
Uwezekano mkubwa wa kufa:
Utafiti uliofanywa na madaktari wa
finland mwaka 1997 umegundua kwamba wanawake wanaotoa mimba wanauwezekano wa
kufa mara nne zaidi kuliko ambao hawatoi mimba. Vifo hivyo vimekua
vikisababishwa na kujiua wenyewe kutokana na kujuta kwa maamuzi yao na madhara
ya mda mrefu ya kimwili yatokanayo na kutoa mimba. Vifo ndani ya wiki moja
baada ya kutoa mimba hutokana na kuvuja damu sana, madhara ya dawa za usingizi,
mabonge ya damu kwenye mishipa ya damu na mimba iliyotunga nje ya uzazi. Utafiti
pia uliongeza kutoa mimba moja uwezekano wa kufa unakua 45%,
mimba mbili 114%, mimba tatu 192%.
Ugumba kwa wanawake wengi:
Miaka hii ya karibuni wanawake
wengi ambao wanalia kutopata watoto wana historia za kutoa mimba miaka
iliyopita, na wengi wao nilionana nao wanajuta sana kwa maamuzi yao. Hii
inatokana na madhara makubwa waliyoyapata kwenye mfuko wa uzazi baada ya mimba
kutoka.
Mimba kutunga nje ya kizazi:
Mfuko wa uzazi una utando maalumu
amaboa hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija iitwayo fallopian kuwezesha yai
kushuka hadi kwenye mifuko ya uzazi. Lakini utoaji wa mimba huambatana na
magonjwa ya mirija hiyo na kupoteza utando huo na kusababisha mimba kukulia
huko.matibabu ya tatizo hili ni kukata mrija husika tu hivyo kuongeza hatari ya
ugumba..
Kuzaa watoto wasio na akili nzuri:
Utoaji wa mimba kuharibu mlango wa
mfuko uzazi kushindwa kushika vizuri na matokeo yake mwanamke huyu hujikuta
akizaa kabla ya mda husika akibeba mimba nyingine. Lakini pia watoto hawa
wanaozaliwa kabla ya muda maalumu na
viungo ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kua wagonjwa wa akili
maisha yao yote.
kansa ya mlango wa uzazi
Wanawake wanaotoa mimba wana hatari
kubwa ya kupata kansa ya mlango wa uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba.
Hii ni kwasababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa
vya kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya homoni za uzazi.
Kuathirika kisaikolojia;
Hakuna mwanamke ambaye hatakaa ajutie maamuzi yake ya kutoa mimba siku za usoni hata kama hakupata madhara yeyote hii itamfanya aishi kama ana deni Fulani maisha yake yote na itakua inamuumiza usiku na mchana. Zingine ni kukosa hamu ya kula, kusikia sauti ya mtoto anayelia wakati hayupo, kua na hasira sana…
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni