HIZI NDIO DALILI ZA TATIZO LA UVIMBE KWENYE KIZAZI
Lakini kwanza kabla ya kuzifahamu dalili ni vyema tufahamu kuwa uvimbe kwenye mfuko wa kizazi ni nini? Tatizo hili hujulikana kama 'fibroid'. Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi.
Tatizo hili huweza kumpata mwanamke yeyote katika maisha yake, lakini hasa huwapata zaidi wanawake walio katika umri wa miaka ya uzazi. Pia ni tatizo ambalo linashuhudiwa sana katika jamii kwa sasa.
Tatizo hili mara nyingi huwa halioneshi dalili za moja kwa moja hasa uvimbe unapokuwa mdogo, hivyo dalili zake hutegemea sehemu ulipo kwenye mfuko wa uzazi na pia ukubwa wake.
Pale inapofikia hatua ya kuonesha dalili mhusika (mwanamke) hutokwa na damu nyingi kwa muda mrefu wakati wa hedhi ikiambatana na mabonge mabonge isivyo kawaida, au kutokwa damu isiyo ya kawaida katikati ya mwezi au hedhi zisizokuwa na mpango. Kufuatia hali hiyo baadhi ya wanawake hujikuta wameingia katika tatizo la upungufu wa damu mwilini 'anemia.'
Dalili nyingine ni kupata maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi, maumivu makali ya tumbo, maumivu wakati wa tendo la ndoa, maumivu ya mgomgo na kukojoa mara kwa mara kwani uvimbe hukandamiza kibofu cha mkojo.
Dalili nyingi za 'fibroid' ni mwanamke kushika mimba lakini huharibika na kuishia kutoka na wengine hushindwa kabisa kushika mimba na wakati mwingine kuwa wagumba.
Tatizo hili pia huweza kuambatana na matatizo ya kukosa choo, matatizo ya figo
Kama unasumbuliwa na tatizo hili au umeona dalili moja wapo kati ya hizo hapo juu ni vyema ukawahi kwenye kituo cha afya kilicho karibu na wewe au unaweza kutufikia katika vituo vyetu vya lupimo sanitarium clinic tutakutibu bila kukufanyia upasuaji.
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu
namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni