Jumapili, 10 Julai 2016
MKURUGENZI WA LUPIMO SANITARIUM CLINIC TABIBU JOHN LUPIMO AMEKABIDHI MADAWATI 50 YENYE THAMANI YA SHILLINGI MILLION 7 KATIKA HALMASHAURI YA KIDONDONI.
Serikali nchini imetakiwa kuhamishia nguvu waliyotumia katika upatikanaji wa madawati kwenye shule mbali mbali nchini na kuelekeza katika ujenzi wa maabala na madarasa ili kuweza kumaliza tatizo hilo kwenye shule mbali mbali hapa nchini.
Ombi hilo limetolewa na tabibu John Lupima ambaye ni Tabibu Bingwa wa tiba mbadala kutoka kwenye kituo cha sayansi ya Tiba asili na tiba mbadala cha Lupimo Sanitarium Clinic wakati alipokuwa anakabidhi madawati 50 yenye thamani ya milioni 7 katika Halmashauri ya Kinondoni, Ambapo amesema kwa licha ya serikali kuwekeza nguvu hadi kufanikiwa kukalibia kumaliza tatizo ukosefu wa madawati basi akaitaka serikali kuhamisha nguvu hiyo kwenye kumaliza tatizo la ukosefu wa madarasa pamoja na maabala ya kufundishia wanafunzi wa masomo ya sayansi jambo analodai litaweza kuikuza elimu nchini.
Amesema kwa sasa kumekuwa na changoto kwenye baadhi ya shule kukosekana kwa madarasa ya kufundishia pamoja na Maabala ya kufundishia hadi kupelekea wanafunzi kufanya vibaya kwenye matokeo ya kidato cha nne, huku akibainisha kuwa njia sahihi ya kuweza kuinua elimu nchini na kuondoa changamoto ya wanafunzi kufanya vibaya kwenye matokea ni serikali kuongeza bidii katika kutatua tatizo hilo, Ameeleza kuwa hatua yake ya kusaidia madawati hayo yametokana na jitihada alizozionyesha Rais John Magufuli aliyoiweka katika kuhakikisha kuiboresha elimu hapa nchini.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni