Jumatatu, 25 Julai 2016

MATATIZO YA HEDHI YANAWAKOSESHA RAHA WANAWAKE WENGI, FAHAMU NAMNA YA KUKABILIANA NAYO


Mzunguko wa hedhi ni mzunguko wa kila mwezi ambao mwanamke huupata, hali ambayo huleta kutokwa na damu ukeni kutokana na mimba kutotungwa. Kwa hali ya kawaida hedhi ya kwanza hutokea katika umri wa miaka 12 -13 na kuendelea.

Hedhi hutokea pale ambapo tishu za ukuta wa mji wa mimba zinapobomoka na kutoka kama damu ukeni.

Kila mwezi ovari za mwanamke katika utaratibu wake wa kawaida kabisa huzalisha yai moja la uzazi na pale inapotokea yai hilo halitarutubishwa yaani kukutana na mbegu za kiume basi ukuta wa mji wa uzazi hubomoka na kusababisha kutoka kwa damu kwa njia ya uke hali ambayo huitwa hedhi.

Mzunguko wa hedhi huanza kuhesabiwa siku ya kwanza mwanamke anapoanza kupata siku zake. Mzunguko wa hedhi huwa na siku 21 hadi 35, chini ya hapo au zaidi ya hapo huashiria uwepo wa tatizo.

Kwa kawaida mwanamke anatakiwa kuwa katika hedhi kwa wastani wa siku 3 hadi 7 na endapo zitazidi hapo pia hali hiyo huashiria uwepo wa tatizo.

Kwa kawaida katika hedhi damu inayotoka haipaswi kuwa na mabonge na nyeusi . Ikitokea hali hiyo huashiria kiasi cha damu anachopata mwanamke ni kingi zaidi ya ilivyokawaida, hivyo ni vyema kuonana na wataalam wa afya kwa ushauri zaidi.

Aidha, kuna hali mbalimbali zinazoweza kujitokeza wakati wa kipindi hiki cha hedhi, ikiwa ni pamoja na maumivu ya tumbo wakati wa hedhi hususani chini ya kitovu, kupata hedhi kwa muda mrefu na mara nyingine kukosa hedhi kwa kipindi fulani.

Maumivu ya tumbo chini ya kitovu husumbua wasichana na wanawake wengi wakati wa hedhi zao. Maumivu haya yanaweza kuwa kidogo au wakati mwingine kuwa makali sana kiasi cha kumfanya ashindwe kufanya shughuli nyingine.

Kama wewe ni binti ambaye umekuwa ukipata maumivu sana wakati wa kipindi cha hedhi unaweza kutumia tangawizi kama moja ya tiba ya kuzuia maumivu hayo.

Tabibu john lupimo wa lupimo sanitarium clinic anasema matumizi ya tangawizi husaidia sana kutuliza maumivu wakati wa hedhi na kinachotakiwa kufanyika ni kutafuta tangawizi kiasi kisha utasaga ili kupata unga wake.

Baada ya kupata unga wa tangawizi utachemsha maji na kupata kiasi cha kikombe kimoja halafu utachukua unga wa tangawizi kijiko kimoja cha chakula na kuweka kwenye kikombe cha maji ya moto kisha koroga vizuri halafu utakunywa mchanganyiko huo asubuhi na jioni.

Mchanganyiko huo wa tangawizi utapaswa kuanza kutumia siku tatu kabla ya kuingia hedhini kwani husaidia sana kuifanya misuli kujiachia na hivyo kuepuka maumivu makali amabayo hujitokeza wakati wa siku za hedhi, lakini kama utahitaji maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Tabibu john lupimo kwa namba 0769368546 au 0672666601 pia unaweza kutufikia katika vituo vyetu vilivyopo mikoani kwa matibabu na ushauri zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni