FAHAMU SABABU SABA KUU NA MATIBABU YA KUSAHAU SANA...
.
Kusahau sana ni hali inayoweza kumfanya mtu akajichukia
sana, kukosa raha na kua na mawazo sana afanye nini kupambana na adha hiyo..
Hii ni hali ambayo inaathiri watu wengi sana yaani wakubwa
na wadodo kulingana na chanzo lakini inakua mbaya zaidi mtu anavyozidi
kuongezeka umri kwani seli za ubongo zinazidi kupungua zaidi.
Kuna hali kitaalamu inaitwa dementia ambayo hutokea mara
nyingi katika umri mkubwa na huambatana na kusahau kuliko pitiliza yaani
kupotea katika mazingira unayoyafahamu, kusahau majina ya kawaida kabisa kama
embe, pazia, kiti na meza, kurudia kuuliza swali la aina moja kila siku, na
kuchanganyikiwa lakini hali huu huletwa na magonjwa Fulani mfano Alzheimer's
disease{hii hali ni hatari na hutibiwa kitaalamu}
Lakini watu wengi hawafiki huko, ila watu wengi sasa
wanasahau vitu vya kawaida sana yaani unakuta mtu kaenda na baiskeli au gari
sehemu afu karudi kwa mguu na kuvisahau huko, mtu anasoma sasa hivi afu
akifunika kitabu amesahau, unaweka pochi sehemu unasahau uliweka wapi, unameza
dawa afu baadae hukumbuki kama ulimeza au vipi, unasahau pesa mfukoni, unapewa
kazi afu unasahau kuifanya na kadhalika..
Hali hizi sasa zinawatesa watu wengi na hawajui wafanye
nini, lakini kuna tabia kadhaa ambazo zinaambatana na hali hizi kama
ifuatavyo..
Kukosa usingizi: binadamu anatakiwa apumzike mpaka masaa
nane kwa siku moja, lakini kutokana na ugumu wa maisha watu hujikuta wanalala
mpaka masaa manne kwa siku. Hii huathiri uwezo wa kufikiri na kusahau kirahisi
sana.
Madawa: dawa zinazotibu magonjwa mbalimbali hua na madhara
madogo madogo ambayo yanaleta kusahau.. mfano dawa za kutibu presha kama
captopril, dawa za kutibu madonda ya tumbo mfano cimetidine na dawa za kutibu
mgandamizo wa mawazo mfano amitriptyline.
Ulevi: unywaji wa pombe uliopitiliza huharibu uwezo wa
kumbukumbu za mda mfupi yaani kusahau kitu umekifanya mda huo huo hivyo
inashauriwa kunywa pombe kiafya. Yaani bia mbili kwa siku mwanaume na bia moja
kwa siku mwanamke ambazo hazina alcohol zaidi ya asilimia tano zinatosha kiafya.
Mgandamizo wa mawazo: kitu chochote kinachokufanya ushindwe
kutuliza akili, kitakufanya usahau sana na kushindwa kupata kumbukumbu
ulizoziweka siku za nyuma.
Upigaji wa punyeto: tatizo hili la kusahau kwasababu ya
punyeto ndio chanzo kikuuu kwa vijana wengi chini ya miaka 35 kwani tabia hii
huambatana na maumivu ya kichwa, uchovu mwingi na kusahau kusiko kwa kawaida.
Uvutaji wa sigara: sigara ina kemikali iitwayo nikotini
ambayo huenda kwenye ubongo na kuua seli za ubongo na kumfanya mtu asahau sana.
Kutokua makini; tatizo la kufanya mambo haraka haraka huleta
kusahau sana, kama wewe una mambo mengi amka mapema uyafanye ila ukianza
kukimbia kimbia njiani ndio chanzo kikuu cha kusahau mambo mengine, pia tabia
ya wanafunzi kusoma kwenye kelele sana au huku wanasikiliza mziki hujikuta
hawaambulii kitu baada ya kufunika daftari.
kwa matibabu ya tatizo hili kama unalo au ndugu yako rafiki yako tufikie katika vituo vyetu vya lupimo sanitarium clinic vilivyopo mikoani na utatibiwa na kurudi katika hali yako ya yakawaida.
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu
namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni