HUU NDIO UWEZO WA KABEJI KATIKA KUTIBU VIDONDA VYA TUMBO
Ugonjwa wa vidonda vya tumbo si tatizo geni miongoni mwa watu wengi kwani wengi wetu tunalifahamu tatizo hili huenda kutokana na kuwa nalo sisi wenyewe au ndugu zetu, marafiki na wapenzi wetu kwa ujumla.
Ugonjwa huu hutokea mara baada ya mhusika kupata vidonda kwenye kuta za utumbo wa mwanadamu ambavyo hutokana na kuzidi kwa tindikali yenye kazi ya kuyeyusha chakula mwilini.
Kuna mambo kadhaa ambayo huweza kupelekea tatizo hili ikiwa ni pamoja na msongo wa mawazo, aina ya vyakula, kutozingatia muda wa kula na mfumo wa maisha yetu kwa ujumla.
Hata hivyo wataalam wa afya wanaeleza kwamba chanzo cha tatizo hili ni kutokana na bacteria anayejulikana kama 'Helicobacteria pylori'.
Ni wazi kwamba kuna mambo mengi sana ya kuzungumza kuhusu hili tatizo la vidonda vya tumbo, kwani naamini kuna baadhi ya watu wangependa kufahamu dalili zake na hata kujua mambo ya kufanya ili kujiondoa katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili naomba nikuahidi kwamba endelea kufuatilia tovuti hii ya www.lupimoclinic.blogspot.com na nitakuletea hayo yote siku zijazo, l akini kwa siku ya leo mimi naomba nikwambie kuwa kabeji inauwezo wa kuwa msaada wako kwa vidonda vya tumbo ikiwa utafanya haya yafuatayo:
Tafuta kabeji na uikatekate kisha isage kwenye mashine ya kutengenezea juisi, baada ya hapo chuja na kisha kunywa kikombe kimoja cha chai cha juisi hiyo mara nne kwa siku.
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu
namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni