Jumatano, 4 Mei 2016

ZIFAHAMU SABABU AMBAZO HUCHANGIA KUHARIBIKA KWA MIMBA MARA KWA MARA NA UZIEPUKE

Mother with serious abdominal pain during her pregnancy

Tatizo la kutoka kwa mimba ni moja ya mambo ambayo huweza kumkuta mwanamke yoyote kutokana na sababu mbalimbali.

Kimsingi kuna sababu nyingi zinazoweza kubabisha mimba kutoka lakini leo hapa nitaeleza baadhi tuu kama ifuatavyo:

Kwanza kabisa kuna baadhi ya magonjwa yanapompata mama mjamzito huweza kupelekea tatizo hili endapo hayatatibiwa vizuri mfano wa magonjwa hayo ni pamoja na malaria, magonjwa ya ngono pamoja na magonjwa yanayoshambulia mfumo mzima wa njia ya mkojo.

Mbali na magonjwa hayo pia kuna matatizo mengine ambayo huathiri moja kwa moja na huweza kuleta madhara ya mimba kutoka kirahisi sana mfano wa magonjwa hayo ni uvimbe wa ndani ya kizazi,ulegevu wa mlango wa uzazi na kadhalika.

Matumizi ya dawa mama anapokuwa mjamzito hapaswi kutumia dawa yeyote bila kuandikiwa na daktari.

Pia matumizi ya pombe na sigara kipindi cha ujauzito ni hatari sana kwani huingilia mfumo wa homoni na uzazi na kusababisha mimba kuharibika.

Sababu nyingine ambayo huweza kuchangia tatizo hili ni umri mkubwa, kubebe mimba kwenye umri mkubwa huchangia sana mimba kuharibika kwani kipindi hiki viungo vya uzazi na mfumo wa homoni unakua umepungua nguvu sana hivyo mimba za ukubwani sana hasa zaidi ya miaka 35 hutoka kirahisi kuliko mimba za vijana lakini pia mimba za utotoni sana si nzuri pia.



kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni