Alhamisi, 31 Machi 2016

UNAPOSEMA HUPENDI MTINDI, BASI FAHAMU UNAZIKOSA FAIDA HIZI


Leo ninayofuraha kukujuza kuhusu faida za kutumia maziwa mtindi. Mtindi upo katika ‘list’ ya vyakula bora kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa binadamu.

Miongoni mwa virutubisho ambavyo vinapatikana kupitia mtindi ni pamoja na vitamini B2, vitamin B12, calcium, hosphorus, , Iodine, Vitamini B5, zinc na Potassium.

Mbali na virutubisho hivyo, ndani ya mtindi pia kuna 'bakteria hai' ambao ni muhimu kiafya kwa mwili. Utafiti umeonesha kuwa, kunywa mtindi mara kwa mara, hasa kwa wazee huongeza uwezo wa mwili wa kupambana na magonjwa pamoja na kuufanya mfumo wa kinga ya mwili kuwa imara zaidi.

Vilevile mtindi unauwezo mkubwa wa kutoa kinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza ukeni

Faida nyingine inayopatikana kwenye mtindi ni kuwa na uwezo wa kupunguza mafuta mabaya mwilini yaani ‘cholesterol’ na wakati huo huo kupandisha kiwango cha mafuta mazuri mwilini.

Mtindi pia husaidia kupunguza uzito na unene. Jambo la muhimu ni kuzingatia unywaji wa mtindi halisi uliotengenezwa kutokana na maziwa halisi ya ng'ombe na sio mtindi uliotengenezwa kutokana na maziwa ya unga.

Unaweza kuutambua mtindi asilia kutokana na ladha yake ya uchachu unaotokana na 'bakteria hai' wanaopatikana baada ya maziwa kuganda na kuchachuka ambao wana faida nyingi katika tumbo pia.


 kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni