Ijumaa, 1 Aprili 2016

  

 
Bila shaka kila mtu analijua tunda aina ya tikitimaji (watermelon), ama kwa kuliona au kwa kulila. Lakini kuna umuhimu wa kuelezana faida zake kiafya. Mbali ya kuwa ni chanzo kikuu cha Vitamin A, B6, C, ‘Potassium’, ‘Magnesium’ na virutubisho vingine kibao, tunda hili pia lina virutubisho vingine vyenye uwezo wa kuamsha hisia za kimwili (Sex libido) na kuondoa matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume (Erectile Dysfunction).
KAMA VIAGRA
Wanasayansi wanasema kuwa Tikitimaji lina virutubisho vinavyoweza kuleta mhemuko wa kimwili kama mtu aliyemeza kidonge cha kuongeza nguvu za kiume cha Viagra. Tunda hili limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya damu na kufanya mzunguruko wa damu mwilini kuwa mwepesi bila athari yoyote mbaya.
UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UGUMBA
Kwa mujibu wa wanasayansi, Tikitimaji lina kirutubisho aina ya ‘arginine’, ambacho huchochea uzalishaji wa ‘nitric oxide’ kwenye mishipa ya damu na hivyo kuongeza nguvu za kiume kama ifanyavyo dawa ya Viagra.
Utafiti waliofanyiwa wanaume 50 waliokuwa na matatizo ya nguvu za kiume, ulionesha kuwa wanaume hao waliweza kufanya tendo la ndoa baada ya kupewa vidonge lishe (food supplement) venye kirutubisho aina ya ‘arginine’.

HUIMARISHA MISULI

Vyakula vyenye kiwango kingi cha madini aina ya ‘Potassium’ kama vile Tikitimaji, huimarisha misuli ya mwili na huwafaa sana wanamichezo. Ulaji wa kipande kimoja cha Tikitimaji baada ya kufanya mazoezi makali, huondoa tatizo la kukaza kwa misuli ya miguu.

HUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI

Tikitimaji lina kiwango kidogo sana cha kalori lakini lina kiwango kikubwa cha maji, hivyo kwa mtu anayetaka kupunguza uzito wa mwili linaweza kumsaidia kwa kula kwa wingi ambapo atakuwa anajisikia tumbo kujaa lakini bila kuwa ameshiba sana, hivyo kuwa rahisi kwake kujizuia na kula vyakula vingine hata kwa kutwa nzima na bila kuathirika kiafya.

HUIMARISHA KINGA YA MWILI

Kirutubisho cha ‘arginine’ kilichomo kwenye Tikitimaji kina kazi nyingi mwilini, mbali ya baadhi ya kazi zilizoainishwa hapo juu, pia huchochea kwa kiasi kikubwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Kama unavyojua, kinga ya mwili ndiyo msingi wa afya bora, kwani ukiwa na kinga imara huwezi kusumbuliwa na maradhi hata siku moja.

HUONDOA SUMU MWILINI

‘Arginine’ vilevile hufanya kazi muhimu ya uponyaji madonda na kuondoa ‘ammonia’ na sumu nyingine mwilini ambazo zinapozidi humfanya mtu kusikia uchovu na kusababisha ugonjwa wa ini na figo.

FAIDA NYINGINE

Faida za Tikitimaji kiafya ni nyingi, tunda hili hufaa kuliwa na wagonjwa wa presha kwani hushusha shinikizo la juu la damu, huongeza nuru ya macho, hutoa kinga kubwa dhidi ya magonjwa nyemelezi yakiwemo yale hatari kama vile kansa ya matiti, kibofu cha mkojo, mapafu na kansa ya tumbo.

KUMBUKA

Matunda kama haya hupaswa kuliwa mara kwa mara na wakati ungali mzima ili kuupa kinga mwili wako ya kujikinga na maradhi wenyewe, usisubiri mpaka upatwe na maradhi hayo na kwa kuambiwa na daktari ndiyo uanze kula, kumbuka siku zote kinga ni bora kuliko tiba!
 
 
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni