JUISI YA UBUYU NA MAAJABU YAKE KATIKA TIBA
Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi. Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.
Tukianza na unga wa ubuyu huu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi zaidi ya matunda mengine yoyote unayoyafahamu. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
Aidha, pia ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) zaidi ya kile ambacho hupatikana katika maziwa ya ng’ombe, hali kadhalika madini mengine ambayo hupatikana katika ubuyu ni madini ya chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo nayo hupatikana kwa kiwango kingi zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi.
Ubuyu pia husaidia kujenga neva za fahamu mwilini na ina virutubisho vya kulinda mwili na kuongeza kinga ya mwili hii ni kutokana na kuwa na kiwango kingi cha vitamini C.
Mbali na hayo, ubuyu pia huongeza nuru ya macho na kusaidia kuzuia kuharisha na kutapika, huku ukiwa umesheheni magnesiam ambayo husaida katika kujenga mifupa ya meno.
Juisi ya ubuyu |
Ni vizuri ukajitahidi kupata kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.
Ili kupata faida hizi za ubuyu na juisi yake kwa ujumla ni vyema ukatumia ubuyu ambao ni halisi (mweupe) ambao haujachanganywa na kitu chochote au kuongezwa ladha au rangi.
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu
namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni