Jumatano, 10 Februari 2016

Kontena laangukia magari saba.

Kama umeteseka kwa muda mrefu na tatizo la ugonjwa wa kisukari sasa suluhisho lako limepatikana, kutana na tabibu bingwa ndugu john lupimo wa lupimo sanitarium clinic kituo cha tiba asilia kuna dawa nzuri ambazo zitatibu kabisa kisukari na kuponyesha kabisa, mpigie sasa hivi tabibu John lupimo umwambie tatizo lako 0742120577,0769368546 au 0672666601.


Pg 1

WATU watatu wamejeruhiwa vibaya na magari saba kuharibiwa katika ajali iliyotokea jana eneo la Tabata, Dar es Salaam.
Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti, walioshuhudia ajali hiyo walisema ilitokea baada ya lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 463 DBR na tela yenye namba T 713 AMD lililokuwa kwenye mwendo kasi kupoteza mwelekeo.
Walisema lori hilo lililokuwa linafukuzana na lori jingine aina ya Scania, lilisimama ghafla baada ya kukutana na daladala iliyokuwa ikiingia barabarani kutoka katika kituo kilico jirani na taa za kuongozea magari.
“Yalikuwa magari mawili aina ya Scania ambayo yalikuwa yanafukuzana, yalipovuka taa za kuongezea magari, ghafla kukawa na daladala inaingia barabarani, na kufanya lori lililokuwa kulia likiwa na kontena kujaribu kusimama likiwa kwenye mwendo kasi, hivyo kuyumba na kupoteza mwelekeo.
“Baada ya lori lile kufunga breki ghafla, ilishindikana na kupoteza mwelekeo na kasha kontena lilifyatuka na kuangukia magari madogo yaliyokuwa barabarani na kuyaharibu vibaya,” alisema Imrani Musa.
Alisema katika tukio hilo, dereva wa lori hilo ambaye jina lake halikufamika mara moja alijeruhiwa na mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia aliyekuwa ndani ya gari lake dogo alivunjika mguu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Lucas Mkondya, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Alisema katika tukio hilo watu watatu walijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao na kukimbizwa Hospitali ya Amana kwa matibabu.

Kamanda Mkondya alisema lori hilo baada ya kuyumba, kontena lake liliserereka na kwenda kugonga magari mengine saba.
“Magari saba yaliharibiwa vibaya kutokana na kontena kugonga gari mojawapo na kusababisha kugongana yenyewe kwa yenyewe,” alisema Kamanda Mkondya.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx



VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,

kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni