Jumatano, 27 Januari 2016

HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUPATA UGONJWA WA KISONONO



Vijidudu vya kisonono

Magonjwa ya zinaa ni miongoni mwa magonjwa ambayo huwakabili vijana wengi na ni moja ya magonjwa hatari sana.

Leo tutaanza kuzungumzia kwanza ugonjwa wa kisonono, huu ni ugonjwa ambao unasababishwa na vijidudu au bakteria waitwao
'Neisseria gonorrheae.'
Moja ya madhara yanayoweza kutokea endapo mgonjwa wa kisonono hata pata matibabu sahihi ni pamoja na kusababisha ugumba.

Ugonjwa wa kisonono huambukizwa kwa kufanya ngono zembe na mtu mwenye maambukizi tayari.


Ngono hiyo inaweza kuwa ni ngono ya mdomo au ukeni na hata kinyume na maumbile pia, kwa kawaida vijidudu vya ugonjwa huu hukaa kwenye majimaji ya sehemu za siri kama vile majimaji ya ukeni na shahawa.


Majimaji hayo yanapopenya kupitia ngozi laini za sehemu za siri husababisha maambukizi kutokea na ikumbukwe kwamba hata kufanya ngono mara moja na mtu mwenye kisonono huweza kusababisha mtu anapata maambukizi.


Hivyo ndivyo namna maambukizi ya ugonjwa huu ya kisonono yanavyoweza kuenea, endelea kuwa karibu nasi na nitakuleta dalili za ugonjwa, tiba yake na namna ya kujikinga, lakini kwa sasa kama unaswali unaweza kuwasiliana nasi au kutufikia lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini

 
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni