Maumivu ya Tumbo ya Mara kwa Mara kwa Wanawake.
Wanawake wanaosumbuliwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu mara kwa
mara hupata athari nyingi baadaye endapo kama hawatagundua chanzo cha
maumivu hayo.
Katika tumbo la mwanamke kuna mfumo wa kawaida wa tumbo ambao ni tumbo
la chakula na mfuko wa haja kubwa, kuna kibofu cha mkojo na mfumo wa
mkojo.
Pia kuna mfumo wa uzazi ambao ndiyo tunaozungumzia leo kwa undani.
Mfumo wa chakula una matatizo yake mengi ambayo huambatana na
kichefuchefu na kufunga choo, mfumo wa mkojo nao una shida nyingi tu
ambazo ni maambukizi au ‘UTI’ au Yutiai ambayo huambatana pia na maumivu
katika njia ya mkojo.
Matatizo ya mfumo wa uzazi huambatana na dalili mbili, mojawapo ni ile ya kutokwa na uchafu ukeni.
Chanzo cha tatizo
Maumivu ya mara kwa mara ya tumbo kwa wanawake yanahusiana zaidi na
mfumo wa uzazi. Maumivu haya yanaweza kuwa maambukizi katika mfumo wa
uzazi ambayo huathiri kuta za ndani za uzazi, maambukizi yanasambaa hadi
katika mirija ya uzazi hali iitwayo ‘Salpingitis’ na huweza kusababisha
mirija kujaa maji ‘Hydrosalpinx ’ au kujaa usaha ‘Pyosalpinx’.
Maambukizi pia husambaa hadi katika vifuko vya mayai ‘Oophoritis’.
Maambukizi pia huwa ukeni na kitaalamu huitwa ‘Vaginitis’ na hushambulia
kuta za uke, yakifika katika mlango wa shingo ya kizazi huitwa
‘Cervicitis’.
Pamoja na kushambulia ndani ya uke na shingo ya kizazi, pia hushambulia
nje kabisa ya uke ambapo mwanamke hulalamika muwasho nje ya uke kwenye
midomo au mashavu ya uke na hata kutokwa vipele.
Dalili za tatizo
Mwanamke mwenye tatizo ukeni hulalamika muwasho ukeni na kutokwa na
uchafu ambao mara nyingi huwa na harufu kama shombo la samaki. Pia
hulalamika maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Mwanamke ambaye maambukizi yamefika katika mlango wa shingo ya kizazi
hupatwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa na wakati mwingine hutokwa na
damu wakati wa kujisafisha huona damu kidogo au kama hakuna damu
atahisi mdomo wa kizazi umevimba na kushika kitu kama kigololi ndani ya
uke.
Mwanamke pia hulalamika kama kuna kitu kinasukumwa wakati wa tendo la ndoa.
Maumivu ndani ya kizazi hasa katika kuta za ndani hupatwa na maumivu
baada ya tendo la ndoa, vilevile hupatwa na maumivu chini ya tumbo muda
wote yaani kila siku na kumnyima raha. Maumivu wakati wa hedhi na
kutokwa na damu nzito nyeusi na wakati mwingine hutoa harufu.
Maumivu yakiwa katika mirija ya uzazi husambaa chini ya tumbo kulia na
kushoto, maumivu pia huwa ya muda mrefu na hali hii humfanya mgonjwa
apate haja kubwa kwa shida.
Maambukizi katika vifuko vya mayai husababisha siku za hedhi zivurugike
na ziwe hazina mpangilio maalum, huathiri upevushaji na uzalishaji wa
mayai hivyo kushindwa kupata ujauzito.
Maambukizi nje ya kizazi humfanya mwanamke aumwe tumbo lote na kupata
hali iitwayo ‘Perionitis’, hupata homa za mara kwa mara na mwili kuwa
mnyonge.
Maumivu ya muda mrefu hudhoofisha afya ya mwanamke, hukosa hamu ya kula na kupoteza raha ya tendo la ndoa na uzazi husumbua.
Maambukizi hushambulia kwa njia ya kupitia ukeni, mfano magonjwa ya
ngono, kuharibika au kutoa mimba na hata kwa kufanyiwa upasuaji wa tumbo
pia huathiri mfumo wa uzazi.
Vyanzo vingine vinavyoathiri mfumo wa uzazi na kusababisha maumivu ya
chini ya tumbo mara kwa mara ni matatizo katika mfumo wa homoni au
vichocheo, uvimbe katika kizazi, mirija na vifuko vya mayai.
Athari za tatizo
Maambukizi sugu katika mfumo wa uzazi huathiri mzunguko wa hedhi,
uzalishaji mayai ya uzazi, kuziba mirija ya uzazi, kupoteza hamu na
uwezo wa kufanya tendo la ndoa.
Kwa ujumla mwanamke mwenye tatizo hili anaweza kupoteza uwezo wa kuzaa na kuwa mgumba.
Matatizo haya hutokea zaidi kwa mwanamke aliye katika umri wa kuzaa.
Uchunguzi
Matatizo haya hufanyiwa uchunguzi katika kliniki za magonjwa ya
kinamama. Vipimo mbalimbali vitafanyika kadiri daktari atakavyoona
inafaa.
Matibabu Tiba inaweza kuwa dawa, upasuaji au yoyote ambayo daktari ataona inafaa kutegemea aina na ukubwa wa tatizo.
nitumie nafasi hii kukukaribisha lupimo sanitarium clinic kama unatatizo hilo na matatizo mengine tunapatikana mikoa mbalimbali hapa nchini,
VITUO VYETU
TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA
NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI
MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA
LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA
PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL,
MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,
kwa maelezo
zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na
0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni