- Tezi ya prostate ni tezi yenye umbile la donati, iliyoko chini ya kibofu cha mkojo.Tezi hii huzungukwa na mirija ya mkojo na huhusika na urutubishaji wa mbegu za kiume ( semen). Mabadiliko ya kimaumbile katika tezi dume kwa mfano; uvimbe, huleta hitilafu katika mfumo mzima wa mkojo kutokana na ukaribu wa maumbile hayo. Uvimbe katika tezi dume husukuma mirija ya mkojo au kuifinya na kufanya mkojo upite kwa shida, ukwame au kuchuruzika bila kukusidia. Hali hii humpelekea mgojwa uhitaji wa kutumia bafu mara kwa mara na zaidi huwa ni vigumu kwa mgojwa kuzuia mkojo kuchuruzika wakati wowote au kukwama). Maumbile yote mwilini, yamekadiriwa kulingana na nafasi, hivyo umbile linapoongezeka ukubwa huleta hitilafu kwa mfumo mwingine.
BAADHI YA MATATIZO YA TEZI YA PROSTATE
- Prostate Cancer ( Saratani ya tezi ya Prostate ) Saratani ya prostate ni saratani inayowashambulia wanaume hasa kuanzia umri wa miaka 50 na kuendelea.Saratani hii huweza kutibika kwa mionzi (radiation), upasuaji, chemotherapy au hormonal therapy.
- Prostatitis (Uvimbe wa tezi ya Prostate); Hali hii ya uvimbe wa tezi ya prostate au eneo la karibu husababishwa na maambukizi (infection) na hutibika kwa dawa za Antibiotics chini ya mwongozo wa daktari.
- Enlarge Prostate au Benign Prostate Hypertrophy (BPH) Ongezeko la ukubwa wa tezi ya prostate Hali hii hutokea kwa wanaume wengi hasa waliopita umri wa miaka 50 na kundelea na huwa chanzo cha kusababisha hitilafu katika mfumo mkojo. Ongezeko la size ya umbile la tezi ya prostate hufinya njia ya mkojo na hupelekea kizuizi katika mrija na kibofu cha mkojo (Chronic Bladder Obstruction) . Hali hii hutibika kwa dawa au upasuaji
Dalili za ongezeko la ukubwa wa tezi ya prostate;
- Maambukizi ya mfumo wa mkojo mara kwa mara ( Urinary Tract Infection,UTI); Mabaki ya mkojo kwenye kibofu au mkojo uliosimama kwa muda mrefu ni chanzo cha maambukizi ya mfumo wa mkojo
- Mawe katika njia ya mkojo
- Mkojo wenye matone ya damu
- Kukojoa mara kwa mara(mabaki ya mkojo katika kibofu hupelekea mtu kuhisi anahitaji kukojoa mara kwa mara japo mkojo unaopatikana ni kidogo sana
- Mkojo unaosita
- Mkojo unaoshindikana kuzuia wa haraka na ghafla
- Kuvuja kwa mkojo kidogo kidogo
- Mkojo unaokatika katika
- Mkojo wa mara kwa mara usiku( Nocturia)
- Mkojo unaokulazimu kujikakamua
BAADHI YA VIPIMO VYA SARATANI YA TEZI YA PROSTATE
- Prostate Specific Antigen (PSA); Kipimo hiki huchunguza kiwango cha antigen za prostate kwenye damu ambacho kwa mtu wa kawaida, huwa kati ya 4 mg/ml. au pungufu. Testi hii huhitaji ushauri wa daktari
Prostate Specific Antigen (PSA); Kipimo hiki huchunguza kiwango cha antigen za prostate kwenye damu ambacho kwa mtu wa kawaida, huwa kati ya 4 mg/ml. au pungufu. Testi hii huhitaji ushauri wa daktari
Digital Rectal Exam ni testi ambayo hufanyika ili kugundua mabadiliko ya ukubwa au hitilafu inayoleta mabadiliko katika maumbile ya tezi ya prostate
Mara nyingi Prostate cancer haina dalili pale inapoanza lakini baadaye dalili zifuatazo huweza kujitokeza.
- Damu kwenye mkojo
- Ongezeko la ukubwa wa tezi ya prostate
- Kupungua uzito wa mwili
- Uchovu
- Anemia (Upungufu wa chembe chembe nyekundu za damu)
- Mkojo wa mara kwa mara usiku
- Kuvuja kwa mkojo kidogo kidogo
- Maumivu wakati wa kukojoa
Saratani ya Prostate yaweza sambaa katika mifupa na tishu za jirani na hata kubana mishipa ya mgongo na kuleta maumivu sehemu za mgongo,hip na pelvic .
Dalili nyingine ;
- Maumivu wakati wa kukojoa
- Kuhisi uhitaji wa kukojoa kwa ghafla
- Damu kwenye mbegu za kiume (bloody semen)
- Ugumu wa kufanya tendo la ndoa au kupungukiwa na nguvu katika uwezo huo
- Maumivu katika utoaji wa mbegu za kiume
- Uvimbe katika sehemu ya miguu au hip na sehemu za uume au pelvic
- Kuhisi ganzi na maumivu ya mgongo, hip au miguu
- Maumivu ya mifupa ya mda mrefu na yasiyo na nafuu.
Kama una swali,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0754301115 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni