Jumatatu, 20 Julai 2015

LA MUHIMU KUHUSU HOMA YA UTI WA MGONGO
Homa ya uti wa mgongo ni miongoni mwa magonjwa hatari sana ambao huua haraka. Ugonjwa huu hushambulia ubongo na uti wa mgongo hasa kwa mwatoto.

Unaweza kuanza kama tatizo la ugonjwa mwingine kama vile surua, kifaduro au kukohoa. Watoto ambao wana kifua kikuu (TB) mara nyingine hupata TB ya ubongo na uti wa mgongo (tubevculosis meningitis) wakiwa na umri wa miezi michache tu.
Dalili: Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo hutambulika kwa dalili zifuatazo. Homa, mkazo wa shingo, mgongo kupinda kwa nyuma. Kwa watot walio na umri chini ya mwaka mmoja utosi uvimba wakati mwingine degedege hutokea au kujitupatupa ovyo ovyo na hali inavyoendelea kuwa mbaya hupotewa na fahamu. TB ya ubongo huanza taratibu kwa muda wa siku au wiki. Aina nyingine zote za homa za uti wa mgongo huanza mapema zaidi kwa masaa au siku.

Kama una swali,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu  namba 0769368546,0719097574 na 0754301115 pia  www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni