UFAHAMU UGONJWA WA PRESHA YA KUPANDA NA MATIBABU YAKE..[HYPERTENSION]
Hypertension ni nini? Huu ni ugonjwa ambao hugunduliwa pale
presha ya damu inapokua juu sana kupita kiwango chake cha kawaida.
Kawaida damu inasukumwa na moyo kwenda sehemu mbalimbali za
mwili lakini nguvu inayotumika kusukuma damu hiyo kutoka moyoni kwenda sehemu zote za mwili na ile
ambayo inakuwepo kwenye mishipa ya damu
wakati damu inapita ndio inaitwa presha ya damu. Hivyo binadamu yeyote lazima
awe na presha ya damu lakini katika kiwango kinachohitajika ambacho ni
120\80mmhg mpaka 140\90mmhg zaidi ya hapo tunaita hypertension..
WALIOKWENYE HATARI YA KUPATA PRESHA..
umri mkubwa: wanaume wako katika hatari ya kupata presha
kwenye umri wa miaka 45 na kuendelea na wanawake miaka 65 na kuendelea.
Rangi ya ngozi: presha ya damu inasumbua sana watu weusi na
huweza kuanza katika umri mdogo zaidi na madhara makubwa kama kupooza, moyo
kusimama ghafla na kufa kwa figo hutokea kwa weusi kuliko weupe.
Familia; Koo zenye wagonjwa wengi kwa presha kwani ugonjwa huu
hufuata koo wakati mwingine
Unene: kadri unavyozidi kunenepa ndivyo mwili moyo unataka
nguvu nyingi kusukuma damu
mwilini hivyo kuongezeka kwa presha.
Kutofanya mazoezi
Kuvuta sigara: kemikali ya nikotini huharbu mishipa ya damu
na kuongeza hatari ya kuugua ugonjwa wa presha.
Kula chumvi nyingi; sodium hubakiza maji mengi mwilini na
kuongeza presha ya damu.
Kunywa pombe sana; kunywa zaidi ya bia mbili kwa wanaume na
zaidi ya bia moja kwa wanawake ni hatari kwa moyo na hupandisha presha ya damu.
Mawazo mengi; mawazo mengi humwaga homoni inaitwa adrenaline
kwenye damu ambayo huongeza presha ya damu hivyo maisha usiyachukulie serious
sana matatizo ni sehemu ya maisha.
Magonjwa Fulani Fulani: magonjwa kama kisukari na magonjwa
ya figo huongeza hatari ya kuugua presha ya damu.
Kuna aina mbili za presha ya kupanda..
Primary hypertension: ambayo inakumba zaidi ya 95% ya watu
na chanzo chake hakifahamiki.
Secondary hypertension: ambayo inakuwepo kwa 5% ya watu na
chanzo chake kinafahamika na ambavyo ni magonjwa ya figo, magonjwa ya mishipa
ya damu, magonjwa ya ubongo na mishipa ya fahamu na magonjwa ya mfumo wa
homoni.
dalili zake ni zipi?
Dalili za presha mara nyingi hua hazipatikani kirahisi na
ugonjwa huu hauna dalili maalumu na wakati mwingine huja kulingana na chanzo
cha presha hiyo kama nilivyoeleza kwenye secondary hypertension kama ifuatavyo.
- Kichwa kuuma
- Kutokwa damu puani.
- Kupumua kwa shida.
- Kuishiwa nguvu
- Moyo kukimbia sana
- Kutokwa jasho kwa wingi
Vipimo vinavyofanyika hospitali..
Kupima presha kwa kutumia kipimo cha presha kitaalamu kama
sphygmomanometer ambacho ikiwa mgonjwa atapimwa mara tatu kwa siku tatu tofauti masaa na kukutwa presha yake iko juu ya
kawaida atahesabiwa kama mgonjwa wa presha na matibabu yake yataanza haraka.
hata hivyo mgonjwa anatakiwa apimwe baada ya dakika tano za kupumzika kama
alikua kwenye mizunguko yake.
Vipimo vingine huchukuliwa na daktari kujaribu kujua chanzo
cha ugonjwa na madhara ambayo mgonjwa anaweza kua ameshayapata kutokana na
ugonjwa huo ni X ray ya moyo kuangalia ukubwa wa moyo, kuangalia wingi wa
lehemu kwenye damu{cholesterol}, ultrasound za figo zote kuangalia kama kuna
shida yeyote huku, kipimo cha maabara cha mkojo kuangalia kama figo zimenza
kupitisha vitu visivyotakiwa kutoka kama damu na kadhalika na kupima sukari
kuangalia kama mgonjwa ana kisukari kwani magonjwa haya huambatana mara
nyingi.
kama unasumbuliwa na tatizo hilo la presha tufikie lupimo sanitarium clinic ambapo sisi hatutakupiga x-ray wala ultrasound bali tutakupima kwa kutumia vipimo vyetu vya mwili mzima ambavyo vitabaini tatizo hilo limekuathiri kwa kiasi gani baada ya hapo tutakuanzishia dozi ambayo itarudisha presha yako kama ilivyokuwa awali, lupimo sanitarium clinic tunapatikana mikoa mbalimbali hapa nchini, unaweza kutufikia kati ya hii mikoa kwa matibabu zaidi.
VITUO VYETU
TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA
NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI
MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA
LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA
PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL,
MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,
kwa maelezo
zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na
0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni