Alhamisi, 26 Novemba 2015

KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

 Wanaume wengi hapa duniani huamini kuwa, mwanaume hasa ni yule anayeweza kufanya tendo hilo kwa muda mrefu na mara nyingi ndio maana vijana wengi utawasikia wakijisifu kuwa, mpenzi wake hakulala usiku mzima kutokana na dozi ya maana aliyompa na ukimuuliza mtu wa namna hii atakwambia kuwa alikwenda mizunguko sita usiku mzima.
 

Hata hivyo, ukweli ni kuwa, watu wengi hufikia hatua ya kusema uongo ili waonekana kuwa ni wanaume hasa mbele ya wenzao huku wangine wakigubikwa na nadharia kuwa ukubwa wa uume unaashiria jinsi gani walivyo wanaume kitu ambacho si kweli.

Ni mtazamo huu ndio unaowafanya wanaume wakitaniwa au kuambiwa kuwa wako kama wanawake wanaweza waue mtu. Tunaamini kuwa uanamke ni udhaifu na uanaume ni ushujaa fulani hivi.
 

Wakati hali ikiwa hivyo, hivi sasa wanaume wengi wamekuwa wakihangaika na jambo moja kubwa, kutafuta dawa za kuongeza nguvu za kiume ili kujiongezea heshima faragha!
 

Ukitaka kuthibitisha hili jaribu kuangalia karibu katika kila gazeti utakalo soma, ni nadra sana kukosa tangazo dogo la biashara lililotolewa na mganga wa kienyeji anayejigamba kuwa anazo dawa za kuongeza nguvu za kiume, na matangazo hayo hayaishii magazetini tu, bali hata redioni pia yapo.
Mbaya zaidi dawa zinazoongelewa hupewa majina mengi ya `kusisimua` kama kombora, simba na nyati siushasikia mziki wa nyati akikasirika sasa jenga picha nuvu ya hiyo dawa, hata hivyo, dawa nyingi ni uzushi tu na hupewa majina hayo ili kuwavuta wateja na kuwashawishi kuzijaribu, enewei ndivyo biashara zilivyo.

Wingi huu wa matangazo umeanza kuonekana katika miaka ya hivi karibuni, na kadiri siku zinavyozidi ndivyo idadi ya waganga wanaojigamba kuwa na dawa hizo inavyozidi kushamiri, kuna waganga wenye dawa za Kiswahili, Kiarabu na za Kichina ndio usiseme!
Binafsi utitili wa matangazo haya umenifanya niamini kuwa, kuna tatizo kubwa la wanaume kupungukiwa nguvu hizo, na ingawa hakuna utafiti wa kitaalamu uliofanywa rasmi, lakini inaonyesha kuwa tatizo hilo kwa sasa ni kubwa sana na si Tanzania tu, bali ni dunia nzima.

Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi moja ya biashara ya dawa za aina hiyo nchini Uingereza, imebainika kuwa asilimia 46 ya wanaume nchini humo hutumia dawa hizo, hata hivyo wengi wao huzitumia bila ya kupata ushauri wa daktari na maduka mengi ya dawa yametozwa faini kwa kuwauzia dawa hizo bila ya kuwa na vyeti vya daktari.
Kupungua kwa nguvu miongoni mwa wanaume wengi kumesababisha wengi wao waishi katika maisha na hali ya usononekaji na wengine wamekumbwa na umauti kutokana na hali hiyo ya kuishi na sononi kwa muda mrefu.

Kuna mambo mengi yanayosababisha wanaume wengi wajikute wakipungukiwa nguvu za kiume, wataalamu wa masuala ya saikolojia wanaamini kuwa mara nyingi suala hilo, hasa kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 45, husababishwa na msongo wa akili kuliko ufanyaji kazi wa misuli ya mwili.

``Watu wengi wanaofikiri kuwa wamepungukiwa na nguvu hizo huwa hawako hivyo,`` inasema sehemu moja ya utafiti uliofanywa na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Havard, nchini Marekani na kufafanua kuwa:

``Tatizo la watu hao huwa ni kushiriki tendo hilo kwa wakati usio muafaka kwao, wanashiriki wakati bado hawajajitayarisha kiakili au wanapokuwa wamejitayarisha, basi `njiani` hukutana na wenzi ambao hawaafiki mwelekeo wa `safari` yao``.

Wataalamu wa masuala ya vyakula nao wanaeleza kuwa tatizo hilo huwapata wanaume wengi kwa sababu ya utumiaji wa vyakula vyenye kuongeza kiwango kikubwa cha mafuta mwilini ambao hawashiriki katika mazoezi ya viungo ambayo huifanya misuli ya damu mwilini kutokufanya kazi vizuri na hivyo kusababisha matatizo mengi ya mwili kushindwa kufanya kazi zake vizuri.

Kumbukumbu yangu inaonesha kuwa, Mheshimiwa Mbunge wa Viti maalumu kuputua tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Janet Bina Kahama, 10 Aprili 2007 katika kikao cha saba cha bunge aliulizwa swali ambalo lilikuwa namba 8 lenye kipengele a, b, na c ambapo kwenye kipengele b aliuliza: Je, serikali inafahamu ni sababu gani zinasababisha kupungua kwa nguvu za kiume kunakotangazwa sana na waganga wa jadi?

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Homeli Mwakyusa alijibu kuwa, Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi, baadhi yao ni lishe duni hasa mboga za majani, kutokula aina mbalimbali za jamii ya karanga (nuts), matumizi yasiyofaa ya ulevi kama pombe, sigara na dawa za kulevya, dawa zinazotibu baadhi ya magonjwa kama kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya akili na vilevile kutopumzika kunakosababishwa na shughuli nyingi za kijamii hivyo kusababisha uchovu.

Lakini ni kweli dawa hizi za asili zinauwezo wa kutatua tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Pro. Mwakyusa anathibitisha kwa kusema kuwa, dawa nyingi za tiba asili ni virutubisho ambavyo muhitaji angeweza kuvipata endapo angekula vyakula vyenye virutubisho hivyo.

Pamoja na kuwa dawa hizo hazijafanyiwa utafiti wa sayansi ya leo na kutokana na unyeti wa usiri wa watumiaji wa dawa hizo zingekuwa na madhara zisingetumiwa na wananchi hata huko zinakotoka yaani maeneo yake ya asili.

Na kusisitiza kuwa, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii haijapokea taarifa ya tukio kutoka kwa walalamikaji wanaotumia dawa hizo za kuongeza nguvu za kiume.

Hata hivyo, hali ni tofauti kidogo katika nchi zilizoendelea kama Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya, matumizi ya dawa hizi hutolewa kwa watu baada ya kuandikiwa cheti na daktari, na watu wenye matatizo ya msukumo wa ndamu (BP), mara nyingi wamekuwa wakishauriwa kutotumia dawa hizo kwa sababu ni hatari kwa maisha yao.

Hii ni kwa sababu dawa nyingi, kama Viagra, Ciallis, Levitra, Yohimbine na nyingine mbali ya kuwa na nafasi ya kusababisha magonjwa ya moyo, kwa watu wasiokuwa nayo, pia yana madhara mengine kama vile kusababisha upofu na kuleta hali ya mwili kuwa na kitetemeshi.

Madhara mengine ya dawa hizo ni pamoja na kumsababishia mtumiaji hali ya kuumwa na kichwa mara kwa mara, macho kuwa mekundu, kuziba kwa hewa puani na maumivu ya tumbo pamoja na kuharisha.

Haya ni aina ya madhara yanayotokana na dawa za kizungu, ambazo kabla ya kuingia madukani kufanyiwa utafiti wa kina kuangalia madhara yake kwa watumiaji, na ingawa hayo yote yanafanyika lakini bado athari zake kwa watumiaji zinaonekana.

Mwandishi na muandaaji mkongwe wa filamu nchini ambaye kwa sasa anaishi Marekani, Chemi Che-Mponda alishawahi kuandika makala isemayo ‘kukosa nguvu za kiume si mwisho wa dunia!’ na katika makala hiyo kulikuwa na hadithi hii isome ili ujue kinachoweza kukutokea kwa kujifanya mjuaji na kuagiza dawa za kuoneza nguvu kwenye mtandao.

Chemi alianza hivi: “Jamani, jamani, jamani, kuna jirani yangu kafa hivi majuzi. Alikuwa ni baba wa makamu, mmarekani mweusi. Alikuwa mcheshi na ilikuwa kila tukionana lazima tusalimiane.
“Mara ananinunulia kahawa halafu tunakaa namsimulia kuhusu Afrika. Yule baba, alionekana mzima na mwenye afya fiti kabisa. Nilibakia kushangaa kusikia kafa na si kwa ajali. Mke wake alifariki mwaka juzi, lakini miezi ya karibuni alikuwa anaonekana mwenye furaha kwa vile alipata mpenzi, dada mwenye miaka 25 hivi.

”Story niliyosikia ni hivi: Kumbe jamaa alikuwa na matatizo ya moyo. Alifia kitandani akiwa kwenye shughuli ya kufanya tendo la ndoa na mpenzi wake. Tena wanasema alifariki mara alipofikia kilele cha tendo.“Navyosikia ilikuwa ni ‘massive heart attack’. Kama ni massive bila shaka na utamu wa shughuli hakujua kuwa yuko hatarini. Mpenzi wake alipiga sana kelele, majirani walipigiga simu 911 (polisi) kwa vile walidhania wameingiliwa na majambazi.

“Kumbe jamaa alikuwa mtumizi wa Viagra, yaani vile vidonge vya kuongeza uume, na kumpa mwanaume uweza wa kufanya tendo la ndoa. Ndugu zake wanalamika kweli, maana hakuzipata kwa prescription (maelezo) ya daktari, alizaiagiza kwenye mtandao (internet).
Hiyo ni baadhi ya mifano hai inayoonesha wazi madhara unayoweza kupata kwa kuamua kutumia tu dawa bila maelekezo kutoka kwa daktari!

Binafsi nina hofu juu ya dawa ‘za kienyeji’ zinazotengenezwa na waganga na kuuzwa kama karanga kila kona ya miji mbalimbali ya Tanzania bila ya kufanyiwa utafiti wa kina, ni wazi kama kanuni za kiafya zinavyosema, kuwa kila dawa ina madhara yake, lakini je, ni nani anapima madhara mabaya yatokanayo na dawa hizi za kienyeji zinazouzwa kama njugu?

Ukiacha madhara yatokanayo na dawa hizo, pia wanaume wengi hukumbwa na tatizo hili la kupungukiwa nguvu kwa sababu ya uvutaji wa sigara kwa wingi, utafiti mbalimbali wa kitabibu duniani unaonyesha kuwa matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku huwasababishia wanaume upungufu wa nguvu hizo.

Ni kweli ulio wazi kwamba tatizo la wanaume wengi kupungukiwa nguvu za kiume nchini kwetu na duniani kote linazidi kushika kasi na tiba mbadara zinahitajika ili kurudisha heshima na furaha miongoni mwa wanaume wengi duniani, lakini utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu haupaswi kufanyika kiholela kwa kuzingatia kuwa matatizo yake kiafya ni makubwa kuliko faraja ya muda mfupi anayopata mtumiaji!

Siku moja nilikuwa nimekaa kwenye kijiwe cha kahawa Kariakoo jijini Dar es Salaam nikachokonoa wazee kwa kuchomekea mada hii, mambo mengi walinieleza lakini kubwa zaidi ni kuwa, vijana wa siku hizi wanakubwa zaidi na tatizo hili kutokana na kufakamia vyakula visivyo vya asili na kusahau kuwa, miogo, asali, karanga na pweza huweza kukusaidia ukawa na nguvu kama nyati. Vyakula vingi vinavyoingizwa nchini vikiwa vimesindikwa ambavyo vijana wengi hukimbilia na kujiona kuwa, babu kubwa wakivila hivyo na kumcheka mzalendo anayepata muogo wa kuchoma na chachandu huku akishushia na juisi ya mua pale Kariakoo bila kujua kuwa sehemu kubwa ya aina nyingi ya vyakula wanavyokula ni sumu yenye ladha nzuri inayonenepesha! Madhara yake ni mengi na miongoni mwake ni kuwasababishia watumiaji kukosa nguvu za kurudia tendo.

Hata hivyo, kuna wakati pia upendo unapopungua na mvuto unapungua baina ya wanandoa, mwanaume anaweza kujikuta kila akiwa faragha anashindwa kuendesha gari kwa muda mrefu na anaweza kudhani kuwa ana matatizo kumbe hali hiyo inamkumbwa kutokana na kutokuvutiwa na mwenzi wake.

Tatizo kama hili linaweza kutatuliwa kwa kumueleza wazi mkeo ama mpenzi wako jinsi gani anaweza kujipanga na kuonekana na mvuto wa hatari utakaokufanya uchanganyikiwe kila umuonapo na hata mkiingia kwenye mambo fulani basi kwa hakika utahamasika na kutoa dozi ya maana.

Uchovu wa kazi za ajira
Mkufunzi wangu wa saikolojia katika Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa ambaye ameshatanulia mbele za haki, Pro. Samuel Mshana (Mungu amlaze mahali pema peponi) aliwahi niambia kuwa wanawake wanataka security kutoka kwa mwanaume nami nikamtania Pro. Sasa mbona mimi na mwili mdogo nitampa ulinzi gani mwanamke akacheka kisha akaniambia ulinzi naouzungumzia ni wa jumla ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mambo yanakwenda sana ndani ya nyumba yani watoto wanakwenda shule na mambo ya mlo wa uhakika.

Hivyo ni wazi kuwa wanaume huhangaika kwa kiasi kikubwa kuhakikisha wanamudu majukumu yao ya kila siku na huko makazini kuna mauzauza mengi na usiombe ufanye kazi kwenye kampuni binafsi kila kukicha wewe upo roho juu sasa katika hali kama hiyo ukikutana na mwenzi wako kunako majambozi utahisi una upungufu wa nguvu za kiume kwani mara tu baada ya kumaliza mshindo wa kwanza hutoweza kurudia tena! Hali ni hivyo hivyo kwa watu wanaofanya kazi nzito zinazosababisha wajikute wanarudi majumbani wakiwa wamechoka.

Hivyo basi, endapo nawe ni miongoni mwa watu wanaokumbana na tatizo la kushindwa kurudia majambozi kwa sababu ya uchovu na msongo wa mawazo kutoka kazini hakikisha unapanga muda muafaka na mwenzi wako kupeana raha.

Mfano kama Jumamosi unafanya kazi nusu siku ukitoka usiende kulewa kama ni mtu wa kinywaji bali nenda kapumzike kisha kesho yake waweza kumtoa out mama na kwenda mazingira tofauti kupeana kitu roho inapenda hakika utajishangaa jinsi utakavyomudu majambozi.

Kuchacha
Nakumbuka vema miaka ya 1990 enzi hizo Redio Tanzania pekee ndio ilikuwa ikitupa burudani na moja kati ya nyimbo ambazo ilikuwa ikinikuna ni ‘kuchacha usiombee’ iliyoimbwa na Juwata Jazz na hichi ni kibwagizo chake ‘Maradhi yote ugua lakini kuchacha usiombe…’ ebwana usije ukawa katika hali mbaya kifedha na kila jambo unalolipanga linakwenda ndivyo sivyo hali inayokusababishia uchache kisha mwenzi wako akakuomba unyumba hapa kuna mawili ama kuchelewa sana kufika safari yenu ama kumaliza halaka kisha jamaa analala chapchap na hataki tena kuonesha ushirikioano hata mamaa akimbembeleza vipi!

Hivyo basi, si vema kukutana kimwili na mwenza wako kipindi ukiwa umechacha kwani wanaume wengi pindi wanapokuwa na msongo wa mawazo hukimbilia kuomba unyumba kwa wenzi wao wakiamini kuwa, wao ndio watawasaidia kuwapunguzia mawazo badala ya kutafuta njia mbadara ya kumaliza tatizo.

Kuishiwa hamu ya nyama na mapishi yale yale kila siku
Uzoefu wangu unanionesha kuwa wanaume wengi hujikuta wakikosa hamu ya kurudia tendo la ndoa mara bada ya kumnaliza mzunguko wa kwanza kutokana na wake zao kutowaonesha ubunifu yaani kila siku ni kifo cha mende tu hakuna jipya linaloongezwa hata nakshi za miguno ni ile ile hali inayosababisha wanaume wakose hamy ya kuendelea mara baada ya kumaliza mzunguko wa kwanza.

Wanaume wengi hujikuta wanalazimika kutafuta kimada ili kupata radha mpya na huko mambo huwa mulua kwani hufanikiwa kwenda raundi hadi tatu na bado akawa na hamu kwa vile tu amekutana na vitu adimu hivyo basi, mwanaume anapaswa kumueleza wazi mkewe kuwa anahitaji wakutane faragha ambapo anataka vutu hadimu vya kabatini na si kumsaliti mwenza wako kwani uwezo wa kumfanya awe bora kunako majambozi unao wewe mnwenyewe mwanamme.

Mfano siku akikwambia anakwenda kwenye kitchen party mruhusu kisha akiwa huko mtumie meseji kuwa, “mpenzi najiandaa kumalizia sehemu ya pili ya soma ulilojifunza yaani la vitendo, hakika leo nitafaidi” asikdanganye mtu hapo hata kama bi. Harusi mtarajiwa hakufundishwa mambo fulani ya kumpagawisha mumewe atahakikisha hakuangushi atakuja na mambo mapya na hapo ndipo mwanaume hujikuta akiganda kifuani.

inawezekana kabisa unasumbuliwa na tatizo hili na ndoa iko ukingoni kuvunjika na hujui ufanye nini tufikie lupimo sanitarium clinic na sisi hatuuzi dawa mitaani bali tuna vituo vya kudumu katika baadhi ya mikoa hapa nchini, tufikie katika vituo vifuatavyo



VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA, 

kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.




Maoni 1 :

  1. Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma,

    Kwaheri Gerd Ulrich

    JibuFuta