Jumapili, 15 Novemba 2015

KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI.

Kuziba kwa mirija ya uzazi ya mwanamke ni tatizo kubwa na ndiyo linaloongoza kusababisha ugumba kwa mwanamke ingawa hata matatizo ya vichecheo au homoni pia huchangia.Wanawake wengi wanaohangaika kutafuta watoto hugundulika na tatizo la mirija kuziba.
Matatizo ya mirija ya uzazi kwa wanawake yapo mengi, mfano mirija inaweza kuvimba na kupoteza uhalisia hivyo kushindwa kutungisha mimba. Mirija inaweza kujaa usaha au maji. Tatizo hili ni kubwa lakini ukifuatilia utakuta linaweza kuzuilika.
Kuziba kwa mirija ni athari za matatizo katika kizazi.

Jinsi tatizo linavyotokea

Matatizo katika mfumo wa uzazi huanzia aidha ukeni au ndani ya kizazi. Maambukizi ya ukeni huweza kujipenyeza hadi ndani ya kizazi na kushambulia tabaka la ndani ya kizazi na mirija.
Maambukizi yanayoanzia ndani ya kizazi pia husambaa hadi ndani ya mirija. Mirija hushambuliwa kwa ndani na nje ya kizazi. Ikishambuliwa kwa ndani husababisha mirija kuziba na ikiwa nje ya mirija husababisha mirija kujikunja.

Matatizo ya kuziba mirija hutokea pale mwanamke anapopata maambukizi ya mara kwa mara ukeni yanayoambana na muwasho kutokwa na uchafu na usaha ukeni, maumivu wakati wa tendo la ndoa na kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa.
Maambukizi haya yasipotibiwa kikamilifu husambaa hadi katika mfuko wa uzazi na kushambulia tabaka la ndani la kizazi na kusababisha tatizo liitwalo ‘Endometriosis’ ambapo mwanamke hulalamika maumivu ya chini ya tumbo au chini ya kitovu mara kwa mara, kutokwa na uchafu ukeni na dalili nyingine tulizozielezea hapo awali.

Maambukzi toka ndani ya kizazi husambaa hadi katika mirija au chini ya kitovu mara kwa mara, kutokwa na uchafu ukeni na dalili nyingine tulizozielezea hapo chini.
Maambukizi toka ndani ya kizazi husambaa  hadi katika mirija ambapo hushambulia mrija mmoja au yote miwili, hapo mgonjwa huendelea  kulalamika maumivu chini ya tumbo au yanaweza kuwa yamekwisha lakini maambukizi yaliyojipenyeza huweza kutafuna mirija na kuziba au kusababisha usaha, maji na kuvimba.

Maambukizi yanaweza kutokea nje ya kizazi na mirija na kusababisha mirija ijikunje na kuziba kabisa hali iitwayo ‘Adhesions’. Maambukizi yanayoanzia ndani ya kizazi chanzo chake ni utoaji wa mimba au mimba kuharibika.
Mirija inaweza kuziba ambapo itakatwa kwa lengo la kufunga uzazi, inaweza kuziba kwa bahati mbaya wakati wa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye kizazi.
Upasuaji wa mirija kwa lengo la kuzibua pia inaweza kuongeza tatizo kwani itatengeneza makovu ambapo mirija itaziba tena. Maambukizi ya muda mrefu ukeni au katika mfumo wa uzazi huathiri mirija ya uzazi.

Dalili za kuziba mirija

Mwanamke anayedhaniwa mirija imeziba anakuwa na historia ya kutafuta ujauzito kwa zaidi ya mwaka mmoja bila mafanikio.Historia hiyo inahusiana na kuwa na historia ya kusumbuliwa na maumivu ya chini ya tumbo kwa muda mrefu iwe yameshatibiwa au la.

Wengine wanakuwa na historia ya kuzaa angalau mtoto mmoja au zaidi lakini anatafuta mwingine anashindwa kupata. Mwingine ana historia ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.
Wengi wenye tatizo hili wana historia ya kuharibikiwa na mimba au kutoa mimba hata moja tu inaweza kukuzibia mirija yako ya uzazi. Endapo mrija mmoja utazibika kabisa basi unaweza kuzaa hata watoto zaidi ya mmoja kwa kutumia mrija mmoja.

Nini cha kufanya?

Tatizo la kuziba kwa mirija linathibitishwa hospitali ambapo kipimo kinachoitwa ‘HGS’ hufanyika ili kuthibitisha. Kipimo hiki ndicho kinachoonyesha kwa usahihi jinsi mrija ulivyoziba, upo uzibaji ambao mrija baadaye unaweza kurekebishwa na mwanamke akapata  ujauzito. Picha nzuri ndiyo itakayomuelekeza daktari jinsi ya kuurekebisha mrija.

Mrija ukiziba nusu yaani ukiachia nafasi kidogo kama hautarekebishwa basi kuna hatari ya kupata mimba na ikabakia kukua kwenye mrija na hatima yake ni mrija kupasuka na kuupoteza.
kama unatatizo hilo usisite kutufikia lupimo sanitarium clinic katika vituo vyetu vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini kwani tatizo hili tunalitibu vizuri na hatimae kupata ujauzito,


MIKOA TUNAYOPATIKANA NI:


VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,

 kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni