Jumamosi, 14 Novemba 2015

Ujue Ugonjwa Wa Pumu


ugonjwa wa pumu (asthma)


 Pumu Ni Nini?

Pumu ni ugonjwa wa muda mrefu (wa kudumu) wa mapafu ambao husababisha njia za kupisha hewa kuvimba na kupunguza kipenyo cha njia za kupitisha hewa. Hali hii humfanya mwenye pumu kurudiwa na vipindi vya kubanwa na kifua, kushindwa kupumua vizuri, kutoa sauti kama ya filimbi wakati akipumua na kukohoa. Hali hii ya kubanwa na pumu hutokea zaidi usiku au mapema asubuhi.

pumu ni nini

Ili kulielewa vizuri tatizo hili la pumu tutatazama namna njia hizi za kupitishia hewa zilivyoumbwa na jinsi zinavyofanya kazi. Njia za kupitishia hewa zimeumbwa kwa mfano wa tyubu (tubes) na zinafanya kazi ya kupeleka na kurudisha hewa kutoka kwenye mapafu. Njia za hewa za mtu mwenye pumu huwa zimevimba na zenye usikivu wa hali ya juu sana ambapo huhisi kwa haraka sana pale ambapo baadhi ya vitu vitakuwa vimevutwa ndani pamoja na hewa mtu huyu anapopumua. Kuvimba kwa njia hizi tayari huwa kumepunguza uwezo wa kuingiza hewa kwa wingi ndani ya mapafu kwa sababu ya kupunguzwa kwa kipenyo cha tyubu hizi. Mtu huyu akivuta hewa yenye baadhi ya vitu, njia hizi hukaza na kupunguza zaidi kipenyo cha njia hizo. Seli za njia hizo zinaweza pia kutengeneza ute (mucus) kuliko kawaida na kufanya njia ya hewa kuwa ndogo zaidi. Ute huu ni majimaji mazito yanayonata.
Hali hii ya kuvuta kitu kisichotakiwa na mwili wa mgonjwa huyu na kusababisha kukaza kwa misuli ya njia za hewa kukiambatana na utengenezaji wa ute kwa wingi na hivyo kumsababishia mtu huyu apumue kwa shida, ndiko tunakokuita kushikwa na pumu au kubanwa na pumu. Mara nyingine hali hii hutokea na isiwe mbaya sana na inaweza ikaondoka yenyewe au baada ya tiba ndogo. Wakati mwingine inaweza ikatokea na hali ikawa mbaya zaidi na kuhitaji tiba na uangalizi wa juu zaidi. Ni muhimu kuchukua hatua zinazofaa mara baada ya dalili hizi kujitokeza kuzuia hali isiwe mbaya zaidi.

Kubanwa Na pumu
Kubanwa Na pumu

Bahati nzuri ni kwamba ugonjwa huu sasa umeeleweka vizuri sana na una njia nyingi sana za kupunguza makali yake. Watu wengi wameweza kuishi maisha ya kawaida baada ya kuelewa namna ya kudhiti tatizo lao. Wamekuwa wakisumbuliwa mara chache sana na wameweza kupata usingizi mzuri bila ya kusumbuliwa na ugonjwa huu. Kinachotakiwa ni mtu mwenye tatizo hili kushiriki kikamilifu katika kuulinda mwili wake na kudhibiti ugonjwa huu na kujenga mahusiano ya karibu sana na madaktari na wahudumu wa vituo vya afya.

Aina Za Pumu


Child-Onset Asthma: Pumu ya aina hii huanza utotoni ambapo mtoto huwekwa kwenye mazingira ya vitu ambavyo mwili wake huviona kama ni vitu visivyofaa kwa mwili wake (allergens) kwa sababu za kiurithi. Mwili wa mtoto huyu huwa umerithi tabia ya kubagua vitu fulani na kinga zake za hujikinga na vitu hivyo.
pumu inayoanza utotoni
Kila mtu ana vitu vyake ambavyo mwili wake hutambua kama ni vitu visivyofaa kwake, ambavyo mara nyingi huwa ni protini ya wanyama, fungus, poleni ya mimea, vumbi la nyumbani na vumbi za aina nyingine. Seli za njia za hewa huwa sikivu kwa vitu vya aina fulani na endapo mtoto atawekwa kwenye mazingira hayo kwa muda mrefu sana, anaweza kuanza kujijengea hali ya pumu kupambana na vitu hivyo.
Adult-Onset Asthma: Aina hii ya pumu huanza kutokea mtu anapokuwa na umri wa miaka 20 au zaidi. Hii ni aina ya pumu inayowapata wanawake zaidi kuliko wanaume na wagonjwa wa aina hii ya pumu ni wachache kuliko wale wa aina ya kwanza hapo juu. Chanzo cha aina hii ya pumu kinaweza kuwa ni kuwa ni mzio (allergy) wa kitu fulani pia, ambapo inakadiriwa kuwa kama asilimia 50 ya watu wanaopata pumu wakiwa wakubwa sababu kubwa ni allergy. Asilimia iliyobakia ambayo chanzo chake cha pumu hakihusiani na allergens, tunasema wana pumu iitwayo non-allergic adult-onset asthma au intrinsic asthma. Kuwepo kwenye mazingira ya kitu au kemikali fulani ya plastiki, chuma, dawa au vumbi la mbao kunaweza kuwa ndiyo chanzo cha  Adult-Onset Asthma.
Exercise-Induced Asthma: Hii ni aina ya pumu ambayo humpata mtu kwa sababu ya kufanya mazoezi au mwili wake kuchoka. Kuna watu wengi ambao hupatwa na pumu pale tu wanapoanza kufanya mazoezi, hili huwatokea hata wanamichezo wakubwa kwenye mashindano kama ya Olympiki. Njia zake za hewa husinyaa kati ya dakika tano hadi ishirini baaada ya kuanza mazoezi hivyo kumfanya apumue kwa shida kunakoweza kuambatana na sauti za filimbi au kukohoa. Daktari anaweza kumshauri mwanamichezo huyu kutumia asthma inhaler kabla ya mazoezi. Asiimia 80 ya watu wenye pumu husikia dalili za exercise-induced asthma wanapofanya mazoezi lakini watu wenye exercise-induced asthma huwa hawasikii dalili za pumu pale wasipofanya mazoezi.
Cough-Induced Asthma: Dalili za pumu ya aina hii ni kukoa sana ni ni ngumu sana kuigundua na kuitofautisha na matatizo mengine ambayo yanasababisha kukohoa kama postnasal drip, sinusitis, chronic bronchitis n.k. Mtu ataanza kukohoa bila kuonyesha dalili nyingine za pumu na kukohoa huku kunaweza kutokea muda wo wote wa mchana au usiku.
Occupational Asthma: Ugonjwa huu hutokana na vitu vilivyopo kwenye eneo la kazi au vitendea kazi. Ni ugonjwa unaompata mtu pale tu anapokuwa kazini ambapo atashindwa kupumua vizuri na kuonyesha dalili nyingine za pumu.
pumu kutokana na kazi
Watu wengi wanaoathirika na aina hii ya pumu hutoa kamasi mfululizo, kuwashwa macho au kukohoa. Kazi ambazo husababisha sana aina hii ya pumu ni ufugaji, ukulima, kunyoa nywele, unesi, kupaka rangi na useremala.
Nocturnal Asthma: Pumu ya aina hii huitwa pia Nighttime asthma. Pumu ya aina hii humshika mtu kati ya saa 6 usiku na saa2 asubuhi na husababishwa na vitu kama vumbi,manyoya ya wanyama au mazingira ambayo hayaruhusu upatikanaji wa hewa ya kutosha. Pumu aina hii mara nyingine haiambatani na kuwa na dalili za pumu wakati wa mchana. Mtu anaweza kupumua kwa shida kukiambatana na sauti fulani bila yeye mwenyewe kujielewa hadi atakapojisikia vibaya usiku wa manane – kati ya saa 8 hadi saa 10 za usiku. Hali hii inaweza kuwa ni ya mara moja moja au mara kadhaa kwa wiki. Mtu mwenye pumu ya kawaida mchana anaweza pia kupatwa na aina hii ya pumu.


Dalili za Pumu
Baadhi ya dalili za kawaida za ugonjwa wa pumu ni kama zifuatazo:
-Kikohozi: Mara nyingi kikohozi cha pumu huwa kikali nyakati za usiku au alfajiri na hivyo kumfanya mwathirika kutolala vizuri
-Kutoa sauti ya mfano wa mtu anayepiga mluzi au filimbi wakati wa kupumua
-Kifua kubana: Mgonjwa husikia kama kitu kinakandamiza kifuani au wakati mwingine husikia kama mtu amemkalia kifuani.
-Kukosa hewa: Baadhi hujisikia kama hawawezi kupumua na kukosa hewa ya kutosha inayoingia au kutoka kwenye mapafu.
-Kupumua haraka haraka
Ikumbukwe kwamba si watu wote huwa na dalili zilizokwisha tajwa hapo juu na dalili zaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu.
Wengine hupata dalili mara moja tu kwa mwezi, wengine kila wiki na wengine hupata dalili kila siku.
Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa sugu lakini unaotibika. Unaweza kudhibitiwa kama vile ugonjwa wa kisukari na moyo unavyoweza kudhibitiwa.

Msomaji wetu kama unasumbuliwa na tatizo hili la pumu au ndugu yako tunakukaribisha lupimo sanitarium clinic tutakupatia matibabu ambayo yatamaliza tatizo hilo ambapo lupimo sanitarium ni clinic ya tiba mbadala inayotibu kwa kutumia mimea na matunda.



MIKOA TUNAYAOPATIKANA,
 
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA, 
  
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic.

 

IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA, MAWASILIANO YETU: 0769368546 AU 0719097574 KARIBU LUPIMO SANITARIUM CLINIC TUKUHUDUMIA NA UEPUKE KIFO KISICHOKUWA CHA LAZIMA.

Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
 
IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA, MAWASILIANO YETU: 0769368546 AU 0719097574 KARIBU LUPIMO SANITARIUM CLINIC TUKUHUDUMIA NA UEPUKE KIFO KISICHOKUWA CHA LAZIMA.

Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA, MAWASILIANO YETU: 0769368546 AU 0719097574 KARIBU LUPIMO SANITARIUM CLINIC TUKUHUDUMIA NA UEPUKE KIFO KISICHOKUWA CHA LAZIMA.

Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni