Jumanne, 5 Aprili 2016

                            MDALASINI NA TIBA ZAKE




Mdalasini ni moja ya kiungo kizuri ambacho hutumika kuongeza ladha nzuri katika kinywaji.



Mdalasini unaweza kutumika kuanzia  magome, na mafuta yatokanayo na magome na kwenye majani.

Unapotumia unga wa magome yake huweza kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo matatizo ya ugumba ambapo mwanaume anapaswa kutumia vijiko viwili vya mdalisini pamoja na kuchanganya na asali katika mlo wa jioni.

Kwa kutumia mchanganyiko huo huo pia husaidia wanawake kuhamasisha kizazi.
Aidha, mchanganyiko huo wa asali na mdalasini husaidia kuondosha lehemu (cholesterol) mwilini

Pia mdalasini na asali husaidia kutibu mafua pamoja na kikohozi 

Mbali na hayo pia mdalasini husaidia kuzuia na kuondoa au kufukuza gesi tumboni, vidonda vya tumbo, kichefu chefu na kutapika, kuharisha , kutia joto tumbo lililopoa.

Hayo ni baadhi ya manufaa ya mdalasini endelea kuwa karibu nasi ili kupata elimu ya mimea tiba na masuala ya afya 
 
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic,instagram.com/lupimoclinic.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni