Jumatatu, 4 Aprili 2016

FAHAMU AINA HIZI 6 ZA JUISI NA FAIDA ZAKE MWILINI



Leo ninayofuraha ya kukufahamisha aina za juisi za matunda na faida zake mwilini katika kutibu magonjwa au kutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Kumbuka kuna ule usemi usema chakula ni dawa, na kumbuka kwamba chakula unachokula leo ndicho ambacho huamua hali ya afya yako ya kesho.
Unaweza kuishi maisha marefu au bila kuugua endapo utazingatia kula vyakula muhimu katika kila mlo wako hivyo ni vyema kuzingatia milo yetu ya kila siku.
CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya husaidia kung’arisha ngozi na kuifanya kuonekana laini, huku pia ikisaidia kupunguza joto la mwili, lakini kwa wale wenye shida ya kuwa na ngozi kavu juisi hii huwasaidia sana.
KAROTI, TUFAHA NA TANGAWIZI
Mchanganyiko wa matunda haya hutoa juisi ambayo huwa na uwezo wa kuondoa sumu mwilini na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Tufani ni Apple kwa kiingereza. 
NDIZI, NANASI NA MAZIWA
Hii ni juisi yenye kiasi kingi cha vitamin na virutubisho mbalimbali vyenye faida mwilini, huku ikisaidia sana kuzuia tatizo la ukosefu wa choo.
KAROTI, EMBE, TUFAHA NA PEASI
Juisi hii inaelezwa kusaidia kuzuia athari ya sumu mwilini na hupunguza shinikizo la dmau na kuondoa mlundikano wa uchafu mwilini.
PEASI NA NDIZI
Juisi hii husaidia kurekebisha kiwango cha sukari katika damu na huwafaa zaidi wagonjwa wa kisukari.
NANASI, TIKITI MAJI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini na husafisha kibofu cha mkojo pamoja na figo. Hivyo juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo na hata kujikinga na magonjwa hayo.
Hata hivyo, pamoja na juisi hizo kuwa na manufaa mwilini pia unapaswa kuzingatia usafi wa matunda yanayotumika na usafi wakati wa matayarisho, huku matunda yakiwa ni yale yaliyoiva vizuri.
Pia zingatia kuweka sukari kiasi kidogo sana kuliko kuweka sukari nyingi maana huweza kuwa na madhara kiafya pia.
 
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic, instagram.com/lupimoclinic
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni