Faida za kiafya za kunywa maji ya moto
NJIA SITA ZA KUNYWA MAJI YA MOTO ZINAZOTIBU MWILI WAKO.
Kunywa kikombe
kimoja cha maji ya moto kila asubuhi inaweza kukutibu mwili wako kwa kusaidia
umeng’enywaji wa chakula na kuzuia kuzeeka mapema kabla ya wakati.
Wengi
wetu huianza
asubuhi vyema kwa kikombe safi cha kawaha ya moto au chai ya moto kwa
lengo la
kuuchangamsha miili yetu baada ya kutoka kitandani. Pale tunakunywa
maji, basi
wengi wetu hupendelea kunywa ya baridi, lakini tunafanya makosa kufanya hivyo. Mara nyingi
unywaji wa maji moto au uvuguvugu, hususani majira ya asubuhi, inasaidia
kuiponya miili yetu na kuitibu,
kwa kusaidia
kuongeza nguvu katika mmeng’enyo wa chakula ma kupunguza taka mwili ambazo
zinaweza kuzuia kinga zetu kuwa katika hali yake nzuri ya mfumo sahihi.
kunywa maji moto ama uvuguvugu
nyakati za asubuhi, kila siku, sambamba na mchanganyo wa maji ya limao, au chai
ambayo haina madhara kwa mwili
Utumiaji wa maji moto ama vuguvugu huongeza ukuzwaji wa utumbo,
ambapo husaidia uondoaji wa vitu visivyotakiwa. Tofauti na maji moto, utumiaji
wa maji ya baridi yenyewe huzuia vitu muhimu ikiwemo madini ambayo huwa si
rafiki kwa mazingira hayo katika mfumo wa umeng’enywaji unapokula chakula.
Kwa wanywaki wa maji ya baridi,inashauriwa kutangulia
kunywa maji hayo ya baridi dakika 20 kabla ya kula hata kama maji hayo yanatoka
katika vyanzo vya asili vya maji. Wakati unywaji wa maji ya moto ama vuguvugu
yanaweza yasiwe mazuri kwa radha yanapokuwa mdomoni,
Hizi hapa zifuatazo ni sababu kwanini unywa maji haya ya
uvuguvugu,
1. Hurahisisha umeng’enywaji wa chakula,
Maji ya moto ama
vuguvugu katika kikombe uamkapo asubuhi inaweza kukusaidia mwili wako kuweza
kutoa nje sumu katika mwili wako. Maji na vimiminika vingine husaidia kuvunja
vunja chakula katika tumbo na kuweka mfumo wa chakula kuwa katika hali nzuri
ndani ya mwili. Maji moto au vuguvugu husaidia kuweza kuvunja vunja chakula
hicho kwa uharaka zaidi, na hivyo umeng’enywaji wa chakula kuwa mwepesi na kwa
haraka.
Unywaji wa maji ya
baridi baada ya mlo wako inaweza kusababisha kusaidia
kugandishwa kwa mafuta ambayo unayapata kupitia chakula na hivyo kusababisha
mrundikano wa mafuta katika utumbo.
Uongezwaji wa
barafu ili kutengeneza maji ya baridi hufanya kubadili mfumo halisi wa madini
na virutubisho katika mwili, anasema Metsovas, ambavyo madini hayo ni muhimu
ili kuweza kuuweka mfumo wa chakula katika hali ya afya, unaweza
kufanya njia mbadala kwa kunywa chupa ya maji ya baridi sambamba na chupa ama
glasi ya maji ya uvuguvu au moto ili kusaidia umeng’enywaji wa chakula,
hususani baada ya kula mlo wako.
3. husaidia kulainisha
choo
Kwa pointi moja au
nyingine, wengi wetu tunakabiliwa na vidonda hususani matatizo ya tumbo ambapo
huwa na choo kidogo au kukosa kabisa haja kubwa.
Vile vile ugumu wa
haja uendapo choo wakati wa kukitoa, husababisha kuchanika kwa eneo la haja
kubwa, haya yote yana letwa na ukosefu wa maji katika mwili. Unywaji wa maji
moto au vuguvugu nyakati za asubuhi wakati tumbo likiwa halina kitu inaweza
kusaidia utumbo mpana kuweza kusukuma uchafu/ kinyesi vyema na hivyo kusaidia
kuwe na choo laini {kinyesi chepesi} wakati wa uvunjwaji wa chakula na hata
usafirishwaji wake huwa mzuri kupita katika utumbo. Hivyo uchangamshwaji wa
utumbo na maji moto husaidia kuurudisha mwili katika ufanyaji wake mzuri na
wakawaida wa kazi vyema.
3. huodoa maumivu
Maji ya moto au vuguvugu, tukizingatia ni maji asilia ambayo
wengi wetu katika majumba hutumia, husaidia kuondoa maumivu ya tumbo la hedhi
kwa wakina mama na maumivu ya kichwa.
maji moto huweza kuwa na athari chanya katika
misuli ya tumbo, ambayo huweza kusaidia kuondoa papo kwa papo makazo na misuli
kujinyoosha. Kwa mujibu wa Healthline, maji moto au vuguvugu ni mazuri kwa maumivu, na
kimiminika cha moto huongeza mzunguko wa damu kwenye ngozi na hivyo kusaidia
kushusha maumivu ya misuli.
4. Husaidia kupunguza uzito
Kama uko katika mlo wako, unywaji wa
maji nyakati za asubuhi basi inaweza kukusaidia katika kupunguza uzito. Maji
moto ama uvuguvugu husaidia kuongeza joto la mwili, ambapo huongeza metabolic/
kiwango cha ufanisi wa kazi katika mwili. Kadiri kiwango cha ufanisi wa kazi
katika mwili kinapoongezeka huruhusu mwili kuweza kuchoma kalori nyingi katika
mwili. Hivyo husaidia figo na gastro
intestinal kufanya kazi vyema
katika mwili.
unywaji wa maji
moto nyakati za asubuhi, kila siku, pamoja na limao ndani yake, au chai huondoa
vitu hatari katika mwili, Unywaji wa glasi kadhaa za maji ya
moto au vuguvugu na limao ndani yake husaidia kuvunja vuja tisu za mafuta,
katika mwili na hivyo husaidia mmeng’enyo wa chakula.
5. Huboresha mzunguko wa damu
Mrundikano wa mafuta katika mwili
huondolewa wakati wa unywaji wa maji ya moto. Hii husaidia kuondoa sumu ambazo
huwa zimezunguka katika miili yetu kwa kufanikisha mzunguko wa damu.
Hakikisha
misuli inapumzika na hivyo wakati kunapokuwa na mzunguko mbovu wa damu katika
mwili wako.
6. Hupunguza hatari ya kuzeeka mapema
Hii inaweza kuzuilika kwa kunywa maji
moto ama vuguvugu, upatikanaji wa sumu katika mwili hupelekea kuzeeka mapema na
kwa haraka, lakini maji moto ama vuguvugu inaweza kusaidia kusafisha mwili kwa
kutoa hizo sumu, hata hivyo pia kuirekebisha ngozi kwa kuoneza SelI mpya maeneo
ya ngozi. wanawake siku zote
hunufaika kwa sababu wanakuwa na homoni nyingi zaidi ambazo huhusika kwayo
Kuweza
kuwa ama kuongeza uimara wa afya yako kupitia unywaji wa maji moto ama
vuguvugu, kunywa kila siku asubuhi maji pekee au yaliyochanganywa na limao kwa
kuongeza radha. wanywaji wa maji vuguvugu au moto kwa,
kadiri wanavyokunywa maji moto wanaweza
kuwa wana angamiza tisu za mdomo na hata maeneo ya kolomeo. Baada ya kuuguzwa na maji hayo ya moto,
Basi
huna budi kuyaacha yapoe kidogo kabla ya kuanza kuyatumia kwa kuyanywa.
kila mara mwone daktari kwa maelezo kabla ya kuanza
kunywa maji hayo ya moto, kama utakuwa
katika matumizi mengine ya dawa ambayo inaweza kuleta madhara katika ufanisi wa
dawa hiyo
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu
namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com,youtube.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni