Ijumaa, 26 Februari 2016

Zijue faida za juisi za matunda mwilini


[​IMG]
Celery (figili)

Juisi ni kinywaji bora na maarufu duniani, lakini ni vyema ukajua juisi ipi ina faida mwilini na ipi haina faida yoyote. Katika zama tulizonazo, kumezuka aina nyingi za vinywaji vinavyoitwa juisi, wakati si juisi bali ni vinywaji vyenye ladha ya matunda mbalimbali.

Juisi ni kinywaji kilichotengenezwa kutokana na tunda halisi au mboga na si mchanganyiko wa maji na kemikali nyingine zenye ladha ya matunda na kupewa majina kama juisi ya machungwa, nanasi, zabibu, n.k. Mara nyingi vinywaji hivyo huwekewa sukari na kemikali nyingine za kuhifahdia (preservertives) ili zisiharibike, ambavyo kiafya havikubaliki.


Licha ya kutumia jusi halisi kama kinywaji tu, juisi pia hutoa kinga na tiba kwa maradhi mbalimbali. Iwapo mtu atatengeneza mchanganyiko maalum wa matunda na kutayarisha juisi maalum na kuinywa, anaweza kupata kinga na tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya kama ilivyoanishwa hapa chini:


KAROTI+ KITUNGUU SWAUMU + EPO

Juisi ya mchanganyiko wa karoti, kitunguu swaumu na epo (apple) husafisha sumu mwilini na kuupa mwili nguvu.

EPO+TANGO+FIGILI

Juisi ya mchanganyiko wa tunda la epo, tango na mboga ya majani aina ya Figili (celery) hutoa kinga ya saratani, hupunguza mafuta ya kolestro mwilini na huondoa hali ya kuchafuka kwa tumbo na kuumwa kichwa.

NYANYA+KAROTI+EPO

Juisi ya mchanganyiko wa nyanya, karoti na epo huboresha rangi ya ngozi na huondoa harufu mbaya mdomoni.

CHUNGWA+TANGAWIZI+TANGO

Juisi ya mchanayiko wa machungwa, tangawizi na matango huboresha ngozi na hushusha joto la mwili.

NANASI+EPO+TIKITI MAJI

Juisi ya mchangayiko wa nanasi, epo na tikitimaji huondoa mlundikano wa chumvi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo pamoja na figo. Hii ina maana kwamba juisii hii ni kinga tosha dhidi ya magonjwa ya kibofu cha mkojo na figo.

KAROTI+EPO+PEASI+EMBE

Juisi ya mchangayiko wa karoti, epo, peasi na embe hushusha joto la mwili, huondoa sumu mwilini, hushusha shinikizo la damu na hupambana na matatizo ya kupumua.

PAPAI+NANASI+MAZIWA

Mchanganyiko wa papai, nanasi na maziwa, ambao una kiwango kikubwa cha vitamin C, E na Chuma (Iron), huboresha rangi ya ngozi na kuifanya iwe nyororo na husaidia mmeng’enyo wa chakula tumboni (metabolism).

NDIZI+NANASI+MAZIWA

Nao mchangayiko wa ndizi, nanasi na maziwa una vitamin nyingi na virutubisho vingi na huondoa tatizo la ukosefu wa choo.

Kwa ujumla, juisi ya mchanganyiko wa matunda hayo ukitumia kama ipasavyo hutoa kinga tosha dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mwili na huweza pia kuwa tiba ya magonjwa yaliyotajwa hapo awali. Ili uone faida za matunda katika suala zima la afya ya mwanadamu, jenga mazoe ya kula matunda hayo kabla hujapatwa na maradhi, kwani kwa kufanya hivyo utaupa mwili wako ile kinga yake ya asili ya kupambana na adui maradhi. 



kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni