Ijumaa, 4 Machi 2016

Faida za mmea wa aloe vera au mshubiri

Mshubiri ni mmea wenye Miujiza ya kutibu maradhi sugu kama ugonjwa wa Saratani (Cancer), ugonjwa wa Kisukari, kolesto , ugonjwa wa kuvimba sehemu ya mwili na magonjwa mengine mengi.

faida ya mu aloe vera au mshubiri
Mshubiri

Faida za mmea wa aloe vera au mshubiri

1. Huondoa uvimbe katika jicho
Weka kiasi kidogo cha majimaji ya mu-aloe vera freshi kisha kuamka asubuhi, acha kwa dakika kadhaa kisha jisafishe. Uvimbe lazima ukimbie. Pia unaweza kuloweka pamba katika majimaji ya mualoe vera na kisha jisafishe katika jicho lenye uvimbe.
2. Huzuia na kuondoa michirizi ya tumbo itokanayo na ujauzito
Anza kwa kupakaa majimaji ya mualoevera juu ya tumbo lako na ufanye kama masaji hivi taratibu juu ya tumbo mara 2 kwa siku katika kipindi chote cha ujauzito na baada ya kujifungua kwa miezi michache mpaka michirizi ipotee yote.
3. Hutibu bawasiri
Ile ile sifa moja iliyonayo ya kutibu uvimbe ambayo inaweza pia kutibu malengelenge na uvimbeuchungu kwenye mwako wa mwili, ndiyo hiyo hiyo pia husaidia kutibu au kupunguza maumivu ya bawasiri. Chana tawi la aloe vera freshi na upate jeli yake, kisha pakaa eneo linalosumbuliwa na bawasiri mara mbili mpaka tatu kwa siku kwa wiki kadhaa hasa kama bawasiri imejitokeza sehemu ya nje hadi hapo uvimbe huo utakapopotea.
4. Ni tiba kwa matatizo ya tumbo
Kama utainywa, hutibu vidonda vya tumbo na kiungulia, na kwa ujumla ni kuwa husafisha mfumo wote wa mmeng’enyo wa chakula. Chukua jeli ya aloe vera nusu kikombe (ml 125) changanya na maji ya kawaida nusu kikombe tena kupata ujazo wa  robo lita, changanya vizuri mchanganyiko huu na unywe kutwa mara 2 kwa siku 3 hadi wiki 1 kujitibu matatizo ya tumbo kama kuum, kuondoa sumu, kuunguruma, kuhara na hata kutibu malaria.
Madhara ambayo yameripotiwa kutokana na kunywa aloe vera ikiwa freshi ndani ya tumbo ni pamoja na kuharisha na matatizo kwenye figo.
Faida za mmea wa aloe vera au Mshubiri
Mshubiri

5. Huziimarisha kucha dhaifu
Kwa taratibu pakaa majimaji ya aloe vera juu ya kucha zako sehemu zote juu na chini kila siku na uzitazame baada ya siku kadhaa uone zitakavyokuwa zimerudisha ule uzuri na ugumu wake wa mwanzo.
6. Huondoa Makeup
Kwa usalama kabisa huondoa makeup kwenye jicho na ni nzuri kwa ngozi laini inayozunguka jicho lako.
7. Husafisha ngozi na kuondoa alama zitokanazo na kuungua na jua
Chunusi, ukurutu na kuungua kwa ngozi kutokana na jua vyote hivi vinatibika kirahisi kwa kutumia aloe-vera. Pakaa mara 2 hadi 3 kwa siku katika ngozi mpaka uone umepona kabisa. Mu-aloe vera pia una sifa ya kupoza kama ilivyo menthol ambayo unaufanya Mu-aloe vera kuwa dawa ya asili nzuri zaidi katika kutibu alama zitokanazo na kuungua na jua.
8. Ni jeli ya asili ya kunyolea na baada ya kunyoa
Aloe Vera ni dawa ya asili katika kutibu michubuko asante kwa vimeng’enya vyake ambavyo huwa na kiasi kingi cha maji ambayo ni mhimu kuzuia kukauka kwa ngozi. Wakati unanyoa ndevu pakaa jeli ya aloe vera na hata baada ya kunyoa pakaa kama after shave jel kuzuia na kuponya michubuko itokanayo na kunyoa.
9. Huondoa makunyanzi na mikunjo ya ngozi
Ngozi hupenda sana Vitamini C na E ambazo zote zinapatikana katika aloe vera na kusaidia kuboresha unene wa ngozi na kuiacha katika hali ya umajimaji. Ikiwa utachanganya jeli ya aloe-vera na mafuta ya asili ya nazi utapata krimu nzuri ya kuongezea viinilishe, mafuta mhimu na unyevunyevu katika ngozi.
Jeli ya Aloe Vera hupenyeza katika ngozi kwa haraka mara nne zaidi ya maji ya kawaida na sifa yake ya kulainisha ngozi husaidia ngozi kubaki na unyevunyevu muda wote.
10. Hutibu homa na mafua
Jeli ya Aloe Vera huongeza kinga ya mwili. Mu-aloe-vera una viinilishe vingi sana mhimu kwa afya ya binadamu. Ina Vitamini A, B, C, na E. Mmea huu una orodha ndefu ya madini mhimu kwa mwili na vimeng’enya vingine mhimu.
11. Vitamini B12 kwa wale wasiotumia nyama (Vegans)
Matumizi makuu ya aloe vera kimatibabu ni kusaidia na kuboresha uundwaji wa bakteria wazuri. Kwa kuongezea aloe vera huwa na jumla ya madini ambayo bakteria huyahitaji katika kutengeneza Vitamini B12.


kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni