Msomaji wetu wa blog
hii ya lupimo sanitarium clinic karibu katika mwendelezo wa makala
mbalimbali zinazohusu afya yako zinazoletwa kwako na tabibu john lupimo
wa lupimo sanitarium ambapo leo anakuletea makala inayohusu ugumba kwa
mwanamke, lakini kama unaswali unaweza kuuliza kwa simu namba
0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinic. au unaweza kutufikia katika vituo vyetu
vilivyopo mikoani
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO.
IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA
UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA
MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI
WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA,
GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO
CHA KIJIWENI AU KALFONIA,
Msomaji wetu mara baada ya kukumbusha mali na mawasiliano yetu
tunapopatikana sasa moja kwa moja twende kwenye makala yetu juu ya
tatizo la ugumba kwa mwanamke
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzu
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzu
Msomaji wetu wa blog hii ya lupimo sanitarium clinic karibu katika mwendelezo wa makala mbalimbali zinazohusu afya yako zinazoletwa kwako na tabibu john lupimo wa lupimo sanitarium ambapo leo anakuletea makala inayohusu ugumba kwa mwanamme na mwanamke, lakini kama unaswali unaweza kuuliza kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic. au unaweza kutufikia katika vituo vyetu vilivyopo mikoani
VITUO VYETU TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL, MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,
Msomaji wetu mara baada ya kukumbusha mahali na mawasiliano yetu tunapopatikana sasa moja kwa moja twende kwenye makala yetu juu ya tatizo la ugumba kwa mwanamke, ambapo jana tuliangalia tatizo la ugumba kwa mwanamke lakini leo tuaangalia tatizo hili kwa mwanamme na mwanamke
Ugumba ni hali
inayotokea iwapo watu wawili, mwanaume na mwanamke wanapokutana kimwili (au
kujamiana) bila kutumia njia yoyote ile ya upangaji uzazi kwa muda wa miezi 12
na kutoweza kushika mimba au kupata ujauzito.
Kuna aina mbili za ugumba;
Ugumba wa asili (Primary
infertility) - Hii ni pale ambapo mwanaume na mwanamke hawajawahi
kutunguisha mimba kabisa maishani mwao hata baada ya kujamiana au kukutana
kimwili kwa muda wa mwaka mmoja bila kutumia njia yoyote ile ya kuzuia kupata
mimba.
Ugumba
unaotokea baadaye maishani (Secondary infertility) - Hii
ni pale ambapo wote wawili, mwanamke na mwanaume wameshawahi kupata ujauzito au
kutungisha mimba angalau mara moja maishani mwao na baada ya hapo
hawajafanikiwa kupata au kutungisha mimba tena.
Asilimia 30-40 ya
tatizo la ugumba huwakumba wanaume na asilimia 40-50 ya tatizo hili huwakumba
wanawake, wakati asilimia 10-30 zilizobakia ya tatizo hili husababishwa kwa
pamoja na matatizo kati ya wanaume na wanawake, hapa sababu halisi
hazijulikani.
Kwa wale wenye afya
njema, uwezekano wa kupata au kutungisha mimba iwapo watajamiana mara kwa mara
kwa mwezi ni asilimia 25-30. Wanawake hufikia kilele cha kupata ujauzito (peak
fertility) wakiwa kwenye miaka ya ishirini. Mwanamke aliye na umri wa zaidi ya
miaka 35 (au baada ya miaka 40) ana uwezekano wa kupata ujauzito kwa asilimia
10.
Je
mimba hutungwa vipi?
Mimba hutungwa baada ya
mwanamke kutoa yai kutoka katika moja ya viwanda vyake vya mayai ya kike
yaani ovaries,kitendo hiki hujulikana kama ovulation.
Yai husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ujulikanao kama uterus (womb)
kupitia kwenye mirija ya uzazi inayojulikana kama mirija
ya fallopian.
Mbegu moja ya kiume (sperm)
ni lazima itungishe au iungane (fertilize) na yai au mayai ya kike (ovum au ova)
wakati yai likielekea kwenye uterus. Baada ya mbegu ya kiume na yai
la kike kuungana, muunganiko uliotengenezwa yaani kiinitete (embryo)
hushuka mpaka kwenye mfuko wa uzazi na kujiwekeza hapo ili kiendelee kuwa
kiumbe.
Tatizo la ugumba
linaweza likawa ni la nwanaume au mwanamke pekee ingawa wakati mwingine wote
wawili wanaweza kuwa na tatizo hili.
Ni
sababu zipi zinazoleta tatizo la ugumba (infertility) ?
Kwa wanawake ;
Tatizo la ugumba
linaweza kutokea wakati wa;
Ø
Yai au kiumbe kilicho ndani ya mfuko (uterus) wa uzazi kushindwa kukua
hadi kufikia kuwa mtoto.
Ø
Mayai yaliyo ndani ya mfuko wa uzazi kushindwa kujishikiza kwenye ukuta wa
mfuko wa uzazi (uterus lining)
Ø
Matatizo kwenye njia ya kupita yai au mayai wakati yanakwenda kwenye mfuko wa
uzazi (uterus).
Ø
Matatizo ya mayai ya uzazi (ovaries) kushindwa kutoa mayai (eggs).
Ø
Tatizo la ugumba kwa wanawake husababishwa na;
Ø
Matatizo ya autoimmune disorders kama antiphospholipid
syndrome (APS)
Ø
Matatizo katika uterus na shingo ya kizazi (cervix) kama uvimbe (fibroids or myomas)
na birth defects
Ø
Matatizo katika mfumo wa kuganda wa damu (clottaing disorders).
Ø
Mazoezi kupita kiasi (excessive exercise), afya iliyodhoofika (poor
nutrition), matatizo ya kula (eating disoder).
Ø
Baadhi ya madawa au sumu.
Ø
Msongo wa mawazo (emotional stress)
Ø
Tatizo la kukosekana kwa usawa wa mfumo wa vichocheo mwilini (hormonal
imbalance)
Ø
Uzito uliopitiliza (obesity)
Ø
Unywaji pombe kupindukia (heavy alcohol intake)
Ø
Magonjwa ya muda mrefu kama kisukari (diabetes)
Ø
Magonjwa ya kina mama (Pelvic inflammatory infection, PID)
Ø
Ovarian cysts and polycytic ovarian syndrome
Ø
Magonjwa ya zinaa (sexually transmitted disease, STD) au endometriosis
Ø
Saratani
Ø
Uvutaji sigara, madawa ya kulevya kama kokeni,
bangi, hashishi nk.
Ø
Matatizo ya hedhi - wanawake wanaopata hedhi bila kutoa mayai (anovulatory
menstrual cycle)
Ø
Kuwepo kwa cervical antigens ambazo huua shahawa za mwanamume
na hivyo kusababisha kwa mwanamke kutopata ujauzito.
Ø
Tatizo la ugumba - linaweza kutokea kwa mwanamume wakati wa;
Ø
Kupungua idadi ya shahawa (decrease number of sperm)
Ø
Shahawa kuzuiwa kutolewa (blockage of sperm)
Ø
Shahawa ambazo hazifanyi kazi yake vizuri.
Ø
Kwa mwanamume, tatizo la ugumba husababishwa na;
Ø
Mazingira yaliyo na kemikali zinazoathiri uwezo wa mwanaume kumbebesha mimba
mwanamke (environment pollutants)
Ø
Kukaa sehemu zenye joto kali sana
kwa muda mrefu (exposure to high heat)
Ø
Matatizo kwenye mfumo wa viashiria vya asili (genetic abnormalities)
Ø
Unywaji pombe kupindukia, matumizi ya madawa ya kulevya kama
kokeni, bangi, hashishi nk, hupunguza idadi na kiwango (quality) cha
shahawa .
Ø
Kuzeeka (older age)
Ø
Kutumia dawa za vichocheo vya mwilini (hormonal supplements) ama
kukosekana kwa baadhi ya vichocheo mwilini (hormonal deficiency)
Ø
Kuasiliwa (impotance)
Ø
Magonjwa ya korodani (testicular infections) au kwenye mishipa ya
korodani (epididymis)
Ø
Historia ya matumizi ya baadhi ya dawa za saratani
Ø
Magonjwa ya zinaa (STD), ajali (trauma) au upasuaji
Ø
Historia ya mionzi (radiation exposure)
Ø
Retrograde ejaculation (matatizo ya kukojoa au kutoa shahawa)
Ø
Msongo wa mawazo (emotional stress)
Ø
Uvutaji sigara
Ø
Matumizi ya baadhi ya dawa kama cimetidine, spironolactone,
nitrofurantoin.
Ø
Varicocele
Ø
Mumps
Viashiria
na vipimo vya ugumba (infertility)
Kwa wanaume;
Ø
Semen analysis - Kipimo hiki kinahusisha uchukuaji wa shahawa kutoka kwa
mwanamume ambaye amekaa siku 2-3 bila kujamiana na kuzipima kujua wingi,
kiwango chake, shepu zake, viscosity of semen, motility and swimming speed.
Ø
Testicular biopsy - Kipimo cha korodani
Ø
Kwa wanawake;
Ø
Kipimo cha kiwango cha vichocheo kwenye damu (blood hormone levels)
Ø
Cervical mucus detection - Kipimo cha kuangalia kamasi za kwenye shingo ya
kizazi ili kupima jinsi zinavyovutika (stretch), na kama ni za majimaji (wet)
wakati wa mzunguko wa hedhi, na kama zina
utelezi ambao huusishwa naovulatory phase
Ø
Kipimo cha kiwango cha joto mwilini (body basal temperature) -
Kuongezeka kwa kiwango cha joto kwa 1 degree kutoka kiwango cha joto cha
kawaida cha binadamu (37 C) kinahusishwa na ovulation ambapo
mwanamke ana asilimia kubwa ya kushika ujauzito au yai limetolewa na ovaries.
Ø
Postcoital testing - Kupima kamasi za shingo ya kizazi (cervical mucus)
zilizochukuliwa masaa 2-8 baada ya wapenzi kujamiana ili kuangalia mwiingiliano
wa shahawa na kamasi za shingo ya kizazi.
Ø
Kipimo cha kichocheo aina ya progesterone kwenye damu (serum
progesterone testing)
Ø
Kipimo cha ukuta wa uterus (biopsy of uterine lining or endometrium)
Ø
Kupima kichocheo aina ya Luteinizing hormone kwenye mkojo ili
kuweza kutabiri lini yai litatolewa na ovaries ili kupangilia
siku za kujamiana kwa wapenzi.
Ø
Hysterosalpingography (HSG) - Kipimo cha X-ray kinachotumia dawa
maalum (contrast dye) inayoonyesha njia ya shahawa kutoka kwenye
shingo ya kizazi kupitia ndani ya mfuko wa kizazi (uterus) na kwenye
mirija ya uzazi(fallopian tubes).
Ø
Laparascopy - Direct visualization of pelvic cavity
Ø
Progestin challenge
Ø
Pelvic exam-hufanywa na daktari.
Tiba
ya tatizo la ugumba (infertility)
Tiba ni kama ifuatavyo;
Ø
Ushauri nasaha na kuwaelimisha wapenzi wawili - Matatizo mengi ya
ugumba hutokea kutokana na uelewa au ufahamu mdogo wa elimu ya uzazi na ya
kujamiana kwa wapenzi au wanandoa.Kuna wanaume wengi ambao hufika kilele haraka
wakati wa kujamiana na hivyo kutoa shahawa mapema (au kukojoa) kabla ya muda
muafaka (premature ejaculation), hii husababisha kutopata ujauzito
ambapo lawama zote hupelekwa kwa mwanamke pasipo mwanamume kugundua kuwa tatizo
ni lake. Ifahamike kwamba hakuna muda uliotengwa ambao ni muafaka wa kufika
kilele au kukojoa kwa mwanamume lakini watafiti wa mambo ya kujamiana
wanashauri angalau mwanamume afike au akojoe baada ya dakika 15 na kuendelea.
Hivyo ni bora kwa wapenzi kujiandaa kisaikolojia mwanzo na kuchezeana kabla ya
kuanza kujamiana ili kurefusha muda kwa mwanamume.
Ø
Tatizo jengine ni kutofahamu lini hasa ni muda muafaka wa kujamiana ili kushika
mimba kwa urahisi. Kuna wanawake ambao hawajui hata mzunguko wao wa hedhi
(yaani hawajui wanaanza na kumaliza hedhi lini na wakati wa hedhi wanatumika
kwa muda wa siku ngapi). Ongeza nafasi yako ya kushika ujauzito kwa kujamiana
angalau mara 3 kwa wiki kuelekea wakati wa ovulation au
kujamiana wakati wa kipindi chote cha ovulation. Ovulationhutokea
wiki 2 kabla ya mzunguko wako mwengine wa hedhi, kama una mzunguko wa hedhi wa
siku 28 (yaani kila baada ya siku 28 unapata hedhi), ni vizuri kujamiana
angalau kwa siku 3 kati ya siku ya 7-18 baada ya kupata hedhi.
Ø
Kupunguza kunywa pombe kupindukia, kuvuta sigara, kuacha matumizi ya bangi,
kokeni nk.
Ø
Kupunguza kiwango cha mazoezi kwa wanawake.
Ø
Kupunguza unene uliopitiliza
Ø
Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu kwani kuwa na wapenzi wengi huongeza athari ya
kupata magonjwa ya zinaa.
Ø
Kuacha tabia ya kuvaa nguo nzito au zenye kuleta joto kali sehemu za siri kwa
wanaume kwani joto kali sana hupunguza kiwango na kuathiri utolewaji wa
shahawa.
Ø
Kula mlo kamili na wenye virutubisho vyote muhimu kwa afya njema.
Ø
Dawa za kutibu magonjwa kwenye mfumo wa uzazi, magonjwa ya zinaa nk.
Ø
Njia za kitaalamu za kupata ujauzito zijulikanazo kama in vitro
fertilization na intrauterine fertilization.
kwa msaada zaidi unaweza pia kutufikia lupimo sanitarium clinic katika mikoa mbalimbali tunayopatikana,
VITUO VYETU
TUNAVYOPATIKANA LUPIMO SANITARIUM CLINIC NI KAMA IFUATAYO. IRINGA TUPO KIHESA
NJIA PANDA YA MTWIVILA, MBEYA TUPO SOWETO KARIBU NA UWANJA WA SHULE YA MSINGI
MWENGE, DAR ES SALAAM TUPO SINZA MORI AU SINZA MAPAMBANO NYUMA YA UKUMBI WA
LULU, DODOMA TUPO AREA C KARIBU NA MSIKITI WA AREA C, SINGIDA TUPO MANYONI NJIA
PANDA YA KUELEKEA CHIKOLA NA HEKA, GEITA TUPO MITI MIREFU KARIBU NA BICK HOTEL,
MWANZA TUPO NYEGEZI KITUO CHA KIJIWENI AU KALFONIA,
kwa maelezo
zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na
0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinic.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni