FAIDA ZA TIKITI MAJI KIAFYA
Baadhi ya vyakula vimekuwa
vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti maji ni miongoni mwa vyakula
hivyo. Kwanza ule mchanganyiko wa rangi zake hulifanya sio tu kuvutia
bali kuwa kama ua lililochanua juu ya meza ya mlaji husika.
Kama vile haitoshi tunda hili limejaaliwa virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa katika afya ya mwanadamu.
Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina
faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi.
Zifuatazo ni baadhi tu ya faida chache kati ya nyingi za tunda hili la
tikiti maji:
Tikiti maji ni chanzo kizuri cha vitamini. Katika
tunda hilo kuna Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia
kuondosha sumu mwilini; Vitamin C, inayosaidia kuboresha kinga, kuponya
majeraha, kukinga uharifu wa seli, kuboresha afya meno na fizi; na
vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha protini
kuwa nishati.
Tunda la tikiti maji lina kiwango kikubwa cha lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani.
Ikiwa familia yako inaishi kwenye eneo lisilo na vyanzo vya madini ya
potasium, unaweza kuwapa tikiti badala yake. Lina uwezo mkubwa wa
kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.
Tikiti pia lina amino asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa yake.
>>>> Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili, ni ule
uwezo wake wa kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu
za kiume. Kwa kunywa juisi yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda
yake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo hilo. Wanasayansi wanasema kuwa
Tikitimaji lina virutubisho vinavyoweza kuleta mhemuko wa kimwili kama
mtu aliyemeza kidonge cha kuongeza nguvu za kiume cha Viagra. Tunda hili
limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya damu na kufanya mzunguruko wa
damu mwilini kuwa mwepesi bila athari yoyote mbaya.
Kwa kawaida
tunda hili huliwa peke yake au kwa kuchanganya na matunda mengine. Kwa
mujibu wa wataalamu wa mambo ya afya ya vyakula kila kitu kwenye tikiti
maji kina faida kiafya ukianzia kwenye majani tunda na hata nyama yake.
Huimarisha misuli, Vyakula vyenye kiwango kingi cha madini aina ya
‘Potassium’ kama vile Tikitimaji, huimarisha misuli ya mwili na huwafaa
sana wanamichezo. Ulaji wa kipande kimoja cha Tikitimaji baada ya
kufanya mazoezi makali, huondoa tatizo la kukaza kwa misuli ya miguu.
Pia husaidia kupunguza uzito mwilini, Tikitimaji lina kiwango kidogo
sana cha kalori lakini lina kiwango kikubwa cha maji, hivyo kwa mtu
anayetaka kupunguza uzito wa mwili linaweza kumsaidia kwa kula kwa wingi
ambapo atakuwa anajisikia tumbo kujaa lakini bila kuwa ameshiba sana,
hivyo kuwa rahisi kwake kujizuia na kula vyakula vingine hata kwa kutwa
nzima na bila kuathirika kiafya
Huimarisha kinga mwili,
Kirutubisho cha ‘arginine’ kilichomo kwenye Tikitimaji kina kazi nyingi
mwilini, mbali ya baadhi ya kazi zilizoainishwa hapo juu, pia huchochea
kwa kiasi kikubwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Kama unavyojua, kinga
ya mwili ndiyo msingi wa afya bora, kwani ukiwa na kinga imara huwezi
kusumbuliwa na maradhi hata siku moja.
Huondoa sumu mwilini,
‘Arginine’ vilevile hufanya kazi muhimu ya uponyaji madonda na kuondoa
‘ammonia’ na sumu nyingine mwilini ambazo zinapozidi humfanya mtu
kusikia uchovu na kusababisha ugonjwa wa ini na figo.
FAIDA NYINGINE
Faida za Tikitimaji kiafya ni nyingi, tunda hili hufaa kuliwa na
wagonjwa wa presha kwani hushusha shinikizo la juu la damu, huongeza
nuru ya macho, hutoa kinga kubwa dhidi ya magonjwa nyemelezi yakiwemo
yale hatari kama vile kansa ya matiti, kibofu cha mkojo, mapafu na kansa
ya tumbo.
KUMBUKA
Matunda kama haya hupaswa kuliwa mara kwa
mara na wakati ungali mzima ili kuupa kinga mwili wako ya kujikinga na
maradhi wenyewe, usisubiri mpaka upatwe na maradhi hayo na kwa kuambiwa
na daktari ndiyo uanze kula, kumbuka siku zote kinga ni bora kuliko
tiba!
Kwa ushauri zaidi tuwasiliane, pia matatizo yakizidi muone daktari kwa matibau zaidi au tufikie lupimo sanitarium clinic
kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana
nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni