JIKINGE AU JITIBU ‘PRESHA YA KUSHUKA ’ KWA CHAKULA
Leo
tunaangalia ugonjwa wa presha ya kushuka (Low Blood Pressure) ambao nao
ni hatari kama ule wa presha ya kupanda, ukitofautiana kidogo namna
unavyomsumbua mtu.
DALILI ZA MTU MWENYE PRESHA YA KUSHUKA
Mtu mwenye ugonjwa wa presha ya kushuka mara kwa mara husumbuliwa na uchovu, mwili kukosa nguvu, kuwa mnyonge na kusikia kizunguzungu. Hali hii hutokea baada ya mzunguruko wa damu kwenye mishipa kuwa mdogo kutokana na kupungua kwa msukumo wa damu hivyo viungo kama moyo, ubongo na viungo vingine kupungukiwa au kukosa damu kabisa.
SABABU ZA PRESHA YA KUSHUKA

sababu kubwa inayochangia
ugonjwa huu ni ukosefu wa virutubisho mwilini kunakosababishwa na ulaji
usio sahaihi. Mtu anapokuwa na upungufu wa protini, vitamin C au moja
kati ya Vitamin B hupatwa na tatizo hili. Aidha,
ugonjwa wa presha ya kushuka, wakati mwingine husababishwa na kuvuja
taratibu kwa damu mwilini kupitia kwenye utumbo, figo au kibofu. Mbali
na matatizo hayo, pia hasira, kupatwa na msongo wa maisha na mawazo
mengi, kunaweza kusababisha presha ya kushuka pia.
VYAKULA VINAVYOSAIDIA PRESHA YA KUSHUKA
VYAKULA VINAVYOSAIDIA PRESHA YA KUSHUKA
Kwa
mujibu wa watatifi wa vyakula, wamegundua kuwa juisi ya Bitiruti
(beetroot) ina saidia sana mgonjwa anayesumbuliwa na ugonjwa huu.
Bitiruti ni aina fulani ya viazi pori ambavyo vinabapatikana kwenye
masoko mbalimbali nchini. Mgonjwa anashauriwa kutengeneza na kunywa
kikombe kimoja cha juisi hiyo kutwa mara mbilli na anaweza kuona
mabadiliko ndani ya wiki moja tu.
KUOGA MAJI YA CHUMVI
KUOGA MAJI YA CHUMVI
Dawa
nyingine inayoweza kutoa nafuu na ya haraka kwa mgonjwa wa presha ya
kushuka ni kuoga kwa kujiloweka kwenye maji ya chumvi maalum. Chukua
kilo moja na nusu ya chumvi, kisha weka kwenye beseni kubwa la maji ya
uvuguvugu, koroga kisha ingia ndani ya beseni hilo na ukae kwa dakika 10
hadi 20. Fanya hivyo muda mfupi kabla ya kwenda kulala na usipatwe na
baridi.
VIRUTUBISHO KAMA TIBA
VIRUTUBISHO KAMA TIBA
Protini,
Vitamin C na Vitamin zote za kundi B, vimeonekana kuwa na uwezo mkubwa
wa kutoa kinga au ahueni kwa wagonjwa wa presha ya kushuka. Mlo kamili
wowote ulioshehemi vitamini B na virutubisho vingine, ni muhimu kuliwa
na mgonjwa wa presha ya kushuka mara kwa mara.
Matumizi ya chumvi nyingi kwa mgonjwa wa presha ya kushuka nayo ni muhimu. Mgonjwa anashauriwa kula vyakula vyenye chumvi nyingi. Aidha, anaweza kunywa maji yaliyochanganywa nusu kijiko cha chumvi kila siku, hadi hapo kiwango cha presha yake kitakaporejea katika hali ya kawaida.
Ili kuliondoa tatizo la presha ya kushuka moja moja, mgonjwa wa presha ya kushuka anatakiwa kuzingatia ulaji wa matunda kwa kiasi kikubwa. Kwa kuanzia, anatakiwa kula mlo wa matunda-matunda tu kwa muda wa siku tano mfululizo, huku akila mlo huo mara tatu kwa siku ukipishana kwa umbali wa masaa matano.
Baada ya hapo, mgonjwa huyo anaweza kubadilisha mlo na ukawa wa matunda na maziwa kwa muda wa wiki mbili hadi tatu. Na baada ya hapo, anatakiwa kuzingatia ulaji wa vyakula asilia vyenye virutubisho vya kutosha ili kuimarisha mfumo wa damu mwilini. Na hii ndiyo iwe staili yake ya maisha kila siku, bila kusahahu mazoezi mepesi mepesi, yakiwemo yale ya kuvuta pumzi na kushusha.

NB: Msomaji wetu ukiona bado tatizo hilo bado linaendelea unaweza kufika katika kituo cha afya kulichopo karibu na wewe au tufikie lupimo sanitarium clinic kwani tatizo hilo tunalitibu vizuri kabisa, kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana
nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 na 0742120577 pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na
www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania,www.lupimoclinic.blogspot.com.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni