Kila seli katika mwili wa binadamu inahitaji kupata hewa ya oksijeni na virutubisho vya kutosha ili viungo vya mwili viweze kufanyakazi yake ipasavyo, zikiwemo seli za ubongo (Brain Cells).
Kwa kuwa hewa ya oksijeni na virutubisho hupita kwenye mfumo wa damu, kitu chochote kinachozuia upitaji huo wa damu
husababisha seli kuathirika. Ni ukweli ulio wazi kwamba moyo unapokuwa na afya njema ndivyo ubongo nao unavyoweza kufanya kazi yake vizuri.
husababisha seli kuathirika. Ni ukweli ulio wazi kwamba moyo unapokuwa na afya njema ndivyo ubongo nao unavyoweza kufanya kazi yake vizuri.
Ili ubongo wa mtu ufanye kazi vizuri, ni lazima hali ya moyo iwe nzuri pia. Hatua ya kwanza ya kuchukua ili kuwa na moyo wenye afya ni kujipima shinikizo lako la damu, kama haliko sawa, unatakiwa ulishughulikie tatizo hilo kwanza.
Zifuatazo ni hatua unazoweza kuchukua ili kujenga afya bora ya moyo wako na hatimaye ubongo kuwa na kumbukumbu nzuri:
PIMA SHINIKIZO
Pima hali ya shinikizo lako la damu pamoja na kiwango chako cha kolestro mwilini. Ubongo wenye afya unatokana na moyo wenye afya nzuri na vitu hivyo vinategemeana.
PATA MUDA WA KULALA
Pata muda wa kutosha kulala. Utafiti unaonesha kuwa kukosa muda wa kulala huathiri mfumo wa kumbukumbu ya ubongo.
FANYA MAZOEZI
Fanya mazoezi mara kwa mara. Mazoezi ya mara kwa mara yameonesha kupunguza uwezekano wa mtu kupatwa na magonjwa mbalimbali. Fanya mazoezi angalau kila siku kwa dakika 30 tu.
CHANGAMSHA UBONGO
Usiulaze ubongo wako, upe changamoto kwa kufikiri na kutatua mambo kadhaa ya kimaisha, kwa kufanya hivyo utauchangamsha.
USIVUTE SIGARA
Usivute sigara, kwa sababu uvutaji wa sigara huongeza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa wa moyo na husababisha madhara makubwa iwapo damu itashindwa kwenda kwa wingi kwenye ubongo kama inavyotakiwa.
JIPUMZISHE
Pata muda wa kupumzisha akili kwa kutafuta njia za kuondoa msongo wa mawazo katika kichwa chako.
VYAKULA VINAVYOSAIDIA KUONGEZA KUMBUKUMBU
Utafiti ulio angalia uhusiano kati ya kumbukumbu na vyakula, umeonesha kuwa kadri mtu anavyokula aina nyingi ya vyakula asili ndiyo uwezo wa kumbukumbu yake unavyoimarika.
Utafiti wa muda wa miaka 25 uliofanywa katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Havard nchini Marekani, uliowahusu zaidi ya watu 13,000, umeonesha kuwa watu waliokula kiasi kikubwa cha mboga mboga kwa miaka mingi, walikuwa na athari ndogo ya kupungukiwa na kumbukumbu baada ya kuzeeka.
Miongoni mwa mboga zenye kiasi kikubwa cha virutubisho vinavyoongeza kumbukumbu ni pamoja na Brokoli, kabichi na maua ya maboga. Zingine ni mboga za kijani kama vile mchicha, majani ya maboga, nk.
Kwa upande wa matunda, aina zote za ‘beri’, zabibu za rangi ya papo (Purple Grapes), tufaha nyekundu (Red Apples) na matunda yanayojulikana kama vitunguu vyekundu (Red Onions).
Halikadhalika vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Folic Acid, husaidia sana katika kuongeza kumbukumbu. Mfano wa vyakula hivyo ni pamoja na nafaka zisizo kobolewa, maharagwe meusi, brokoli, ngano, machungwa, n.k.
SAMAKI
Watafiti wa Rush University Medical Centre, Chicago nchini Marekani, walifuatilia watu 3000, wake kwa waume, kwa muda wa miaka sita kuona ni kwa kiasi gani lishe huathiri kumbukumbu ya mtu.
Utafiti huo ulionesha kuwa watu waliokula samaki angalau mara moja kwa wiki, walionesha kupoteza kumbukumbu taratibu kwa asilimia 10 ukilinganisha na wasiokula samaki. Kiasi hicho kiliwapa uwezo wa kufikiri na kuwa na kumbukumbu sawa na kijana waliyemzidi umri wa miaka mitatu.
Kama una swali,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu
namba 0769368546,0719097574 na 0754301115
pia
www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinic
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni