Jumanne, 8 Machi 2016

FAIDA ZA MATUMIZI YA JUISI YA EMBE KIAFYA ZOTE ZIPO HAPA




Embe ni moja ya tunda lenye ladha nzuri sana na asilimia kubwa ya watu wamekuwa wakilipenda sana tunda hili kutokana na kuwa na ladha nzuri, lakini swali linakuja je, tunafahamu umuhimu wa tunda hilo?

Hapa ninazo faida za juisi ya embe kwa afya zetu karibu tuzipate zote hapa chini>>>

Juisi ya embe husaidia sana kuleta uoni mzuri kwa sababu juisi hiyo ina vitamin A ambayo huimarisha sana afya ya macho na kuwasaidia wale wenye macho makavu na wenye uoni hafifu wakati wa usiku 'blindness'.

Matumizi ya juisi ya embe pia huwa na faida kubwa kwa afya ya ngozi, unachopaswa kufanya ni kupaka makapi ya embe usoni na kukaa nayo kwa muda usiopungua dakika kumi, baada ya dakika hzio kupita utaosha uso kwa maji yanayotirirka husani yanayotoka bombani. zoezi hilo litakusaidia sana kuonekana na ngozi nzuri pamoja na kutibu shida ya chunusi pia.

Juisi ya embe inapotumika bila kuwekwa sukari huwa ni nzuri sana kwa watu wenye shoda ya kisukari kwani huenda kusaidia kurekebisha sukari ya mwili kuwa vizuri na kurekebisha mapigo ya moyo kuwa sawa na kuondoa sumu hatari mwilini

Juisi hii pia inasifika kwa kuimarisha mfumo wa umeng'enyaji wa chakula mwilini, pamoja na kusaidia sana kuondoa shida ya ukosefu wa choo hasa pale unapopata juisi yenye mchanganyiko wa embe na nanasi huwa nzuri zaidi kwa shida hiyo.

Ndani ya juisi ya embe huwa kuna vitamin C, na vitamin A pamoja na 'carotenoids' ambazo zote zinapokuwa kwa pamoja husaidia sana kuimarisha kinga za mwili.

Pia ndani ya juisi ya embe hupatikana vitamin B, E. K pamoja na madini calcium, potassium, magnesium, phosphorus na iron.
 
 kwa maelezo zaidi,maoni au ushauri wasiliana nasi kwa simu namba 0769368546,0719097574 0672666601na 0742120577 pia www.facebook.com/lupimoclinic,www.twitter.com/lupimoclinic na www.hulkshare.com/lupimoclinictanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni